Taarifa za uhakika ni kuwa,tawi la ccm yaani ACT watafanya mkutano wa hadhara na kikao cha ndani tar 25 mwezi huu,kijiji cha ndago wilayani iramba.Mkutano huu unaratibiwa na aliepata kuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya iramba,na baadae kununuliwa na mwigulu,na kisha kujidai kurudi tena chadema,ndugu Edgar EManuel Ntundu.Msakatonge huyu anawasiliana kwa karibu na mwenyekiti wa Chadema aliyepita kimangumashi wiki iliyopita ndugu Ally gesi msabaha.Utafiti unathibitisha bayana kuwa,kumekuwa na mawasiliano ya simu kati ya Ntundu na Ally juu ya ujio wa mkutano wa act iramba.Ikumbukwe kuwa ndago ndipo zilipotokea vurugu mwaka juzi kwenye mkutano wa Kitila Mkumbo na Mnyika,uliosababisha kifo cha mtu mmoja.Ndago ni moja ya ngome za chadema,hivyo ccm na hawara wao act,wanatafuta kila njia kuibomoa ngome hii.Taarifa zaidi zitatolewa