ACT-Kigoma wararuana kisa ubunge

ACT-Kigoma wararuana kisa ubunge

Huyo jamaa hamna kitu yupo huwa anashinda awimo bar tu na ni mwanafunzi wa sauti campus ya mwanza na alimalizia Newman college/kihinga form six kwa manati atamuongoza Nani?kwanza ni promo tu hiyo mxiuuuuuuuuuuw
Mkuu iweke sawa kidogo aka minofu.
 
`nyoka aliyejificha ni mbaya na hatari sana kuliko nyoka anayeonekana'
ACT ni nyoka anayeonekana,hivyo tutamuua hata kwa mabua!!
 
Tunashukuru kwa taarifa , swali la nyongeza , kwahiyo kwa mujibu wa hayo makubaliano serukamba ndio ataenda kugombea kigoma kaskazini ? Hakika laana ya usaliti ni mbaya mno !
 
Duh ikifikia hatua mpinzani anabadilishana jimbo na chama tawala basi ni disaster

Eti anasema Kigoma kas walimpa kura chache 2010 coz ya dini yake,nao wakamwuliza 2005 walikuwa hawaijui dini yke ?na kuahidi kumnyima kura 2015 that y Zitto kaamua kwenda kwa wenzake
 
Eti anasema Kigoma kas walimpa kura chache 2010 coz ya dini yake,nao wakamwuliza 2005 walikuwa hawaijui dini yke ?na kuahidi kumnyima kura 2015 that y Zitto kaamua kwenda kwa wenzake

Zitto kama alisema hvyo basi ni mtu hatari wa kuogopwa.
 
Wakazi wa jimbo la Kigoma mjini: Zitto tulia ujenge chama chako kipya,ubunge waachie wengine

Na Nicholaus Kilunga
-Kibondo Kigoma

Wakazi wa Kigoma mjini wamtaka Zitto Kabwe aachane -na siasa ya kugombania ubunge dhidi ya wanachama wenzake wa ACT na badala yake ajikite kwenye kukijenga chama chake kipya cha ACT-Tanzania,Hayo yamesemwa jana na wakazi wa manispaa ya Kigoma mjini walipozungumza na mwandishi wa habari hii,walisema kwa mda mrefu sasa kumekuwa na mnyukano wa ndani kwa ndani na wa kimyakimya ulioibuka miongoni mwa wanachama ACT wale wanamuunga mkono Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe dhidi ya mratibu wa ACT kanda ya magharibi bwana Wiston Andrew Mogha,mara tu ya wawili hao kutangaza nia ya kuwania jimbo hilo ambalo kwa sasa linaongozwa na Peter Serukamba wa CCM.
Jimbo la Kigoma mjini lenye takribani wapiga kura….linatajwa kuwa muhimu kimkakati na kisiasa kutokana na kuwa ndipo kunapoamua aina ya siasa ya mkoa wa Kigoma,na ndilo jimbo lenye rasilimali nyingi kiuchumi na ndio jicho la mkoa,lakini likitawaliwa hasa na siasa zenye mlengo wa Kumtazama nani anaegombea na si chama,dini na asili ,mwandishi wa habari hii aliepiga kambi jimboni humo kwa takribani wiki 2 sasa,alifanikiwa kufanya mazungumzo na watu wa rika na makundi mbalimbali ndani ya jimbo hilo,bwana Hamidu Hussein mkazi wa kilima hewa,alipozungumza na mwandishi yeye alisema,”ninachokiona ni kwenda kuipasua ACT Kigoma mjini ambapo ndipo ngome yetu ACT ilipo,Kabwe ni mwanasiasa mkubwa natambua,lakini ifike siku awaachie wenzie,wanasiasa wachanga ili nao wanyanyuke kama yeye alivyonyanyuliwa kipindi kile na Mh Mbowe na kufundishwa siasa”Bwana Hussein aliendelea kusema awali kipindi wanaianzisha ACT Kigoma,mtu wa kwanza kutangaza nia ya kupimana ubavu na mbunge wa sasa Peter Serukamba alikuwa ni Wiston Mogha na kwamba Zitto alikubali kumuunga mkono,lakini anashangazwa na Zitto kuibuka gafla na kusema wamebadilishana na Serukamba majimbo.

Mkoa wa Kigoma ambao mara zote umekuwa ngome imara ya upinzani,umekuwa ni miongoni mwa mikoa michache ya kwanza kupokea vyama vya upinzani na kuviunga mkono na hatimaye kutoa wanasiasa mahiri japo wamekuwa wakikengeuka na kuviacha vyama vyao kwa madai mbali mbali kama hujuma na usaliti,kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 mkoa wa kigoma wenye jumla ya majimbo 8,upinzani ulijinyakulia majimbo 5 kati ya hayo 8,huku CCM ikiambulia majimbo 3 ambayo nayo walishinda kwa tabu huku rafu na dosari za kiuchaguzi zikiwa nyingi,huku ukiwa ni ngome imara ya CHADEMA kwa sasa.

Sakata la Zitto kutaka kuvuliwa uanchama wake ndani ya CHADEMA lilipelekea -mtafaruku mkubwa mkoani hapa huku watu wengi wa Kigoma mjini wakihisi CHADEMA kumwonea,Zitto na wenzake walidaiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi ya kiuongozi kinyume na taratibu huku pia akidaiwa kukisaliti chama hicho kikuu cha upinzani kwa faida ya CCM,kufukuzwa kwa- Zitto kulipelekea uanzishwaji wa chama kipya cha ACT huku mizizi yake ikidaiwa ipo mkoani Kigoma,jambo liliumbuliwa -katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo hilo la Kigoma mjini chama hicho cha ACT kiliambulia viti Mitaa10 kati ya mitaa 68 huku CHADEMA wakipata viti 11,NLD 1 na CCM- viti 46,huku ACT ikishindwa kunyakua hata kiti kimoja katika majImbo ya Buyngu,Muhambwe,Manyovu nk,akiongelea hali imeaonza kujitokeza ndani ya chama cha ACT Juma Ismail ambaye pia ni kiongozi na mwanchama wa ACT anasema binafsi hali hiyo inamkatisha tamaa sana hasa ikizingatiwa kwamba mgogoro ulioibuka kati ya kundi la Mwenyekiti wa muda wa chama hicho ndugu Limbu na kundi la katibu mkuu limekivunja sana chama hasa kwa vijana,ambao wamefika mahala wanayajutia maamuzi yao ya kuachana na CHADEMA na kujiunga na ACT,chama ambacho kiliwahubiria kitakuwa mfano kwa demokrasia na badala yake wameanza mapema kugombania madaraka kama CCM.
Mwandishi pia alifanikiwa kufika kwenye eneo maarufu la siasa za Kigoma ,eneo la Meza ya Duara na kufanya mahojiano- na mzee mmoja maarufu kwa kuvaa kofia ya zambarau ambaye hata hivyo aliomba jina lake lisitajwe kwa madai yeye si msemaji wa chama na wahusika,lakini katika maelezo yake anasema
“Mogha na Zitto wote ni wapenda mabadiliko na wanachama wa ACT,tofauti yao mmoja ni mwanachama hai na anaeshiriki shughuri zote za kukijenga chama na mwingine ni mwanachama wa ACT aliejificha,akasema kwa mtazamo wake kwanza hayatambui makubaliano ya kuachiana jimbo kati ya Zitto na Serukamba ,lakini akasema kwa sasa Zitto akigombea jimbo la KIgoma mjini hawezi- kushinda kutokana na kwamba kwa sasa anachukiwa na watu wengi wa CHADEMA wanaomuona kama kiongozi wa usaliti wa chama hicho”mzee huyo aliendelea kusema tangu uibuke mgogoro wa kugombea madaraka kati ya Limbu na Mwigamba chama hicho kimepasuka,na mwandishi alipomtaka aweke shilingi yake kati ya Mogha na Zitto kwamba ni ypi anaeweza kushinda kiurahisi alisema yeye anamwunga mkono Mogha kutokana na kuwa Zitto kwa sasa anamaadui wengi,lakini akamtaka Zitto ajenge chama chao aachane na madaraka kwani mda aliokuwa madarakani kama mbunge wa Kigoma Kaskazini unatosha,na kwamba awaachie wengine.

Kwa upande wao bwana Mwema Kizinga mkazi wa katubuka na Peter Robart mkazi wa Gungu wanasema kwamba wao- hawaoni kama huo ni mgogoro mkubwa kwani Mogha hana uwezo wa kupambana na Zitto japo anaungwa mkono na wananchi wengi,lakini chama kitatumia busara,hasa kwa kuwa wanatarajia kumchagua Zitto kama mwenyekiti wa chama hicho mda wowote ule,hivyo kumpa wito wa kumtaka Zitto amwachie Mogha agombee nay eye ajikite kumsaidia na kukiimarisha chama,Bwana Robart yeye alisema Zitto na Mogha ni wote ni wahanga wa siasa, huku Mogha akiwa amewekwa ndani(polisi)mara nyingi kama Zitto kutokana na siasa za ACT na pia kuna taarifa amesimamishwa masomo yake ya shahada ya kwanza chuo kikuu SAUT Mwanza akiwa ndo anajiandaa kuingia mwaka wa 3 kutokana na mda mwingi kuutumia kuijenga ACT na kukosa vipindi vingi vya darasani.

Ili kubaini ukweli mwandishi wa habari hii alijaribu mara kadhaa kumpigia simu mh Kabwe ili kuongelea habari hii lakini simu yake haikupokelewa na hata pale alipotumiwa ujumbe wa simu kwa njia ya maandishi hakujibu lolote,kwa upande wake bwana Mogha yeye alijibu kwa kifupi tu kwamba “chama -kinataratibu zake na ndizo zitakazotumika kumpata mgombea,binafsi yeyote atakaepitishwa na chama nitamuunga mkono,japo namwomba Mungu chama kiniamini na sina ugomvi na kiongozi wake Zitto kwani- Kabwe ni kama kaka yangu”
Hata hivyo mwandishi wa habari hii anataarifa za ndani namna vita ya madaraka inavyoendelea kuitafna ACT huku wakitoa mwanya kwa CHADEMA kuendelea kuungwa mkono kwani alifanikiwa kuoneshwa kadi za ACT zilizorudishwa CHADEMA kutoka kwa wafuasi wa ACT,na zaidi ACT ni chama kilichojikita zaidi Kigoma mjini huku katika majimbo mengine mkoani humo kikiwa hakina hata tawi moja,watu wengi waliongea na mwandishi wa habari hii walisema wanapenda kumwona Zitto akikijenga chama hicho huku akiwasaidia wengine kupata ubunge nay eye kujiandaa kugomboe urais umri utakapomruhusu.
Pichana ni Wiston Mogha anaeraruana na Zitto Kabwe

heading mbovu kabisa hakuna mtiririko mzuri wa habari.yaani umepachika pachika tu maandishi utafikir hiyo degree hujasomea SAUT!?
 
heading mbovu kabisa hakuna mtiririko mzuri wa habari.yaani umepachika pachika tu maandishi utafikir hiyo degree hujasomea SAUT!?

We unafikiri kwa nini kila chombo cha habari kinakuwa na wahariri?hapa jeshi la mtu 1
 
Zitto akithubutu kugombea Kigoma ataibika siyo kawaida maana atashundwa kwa kishindo.

Kweli mkuu kwa sasa amepoteza mvuto sana kisiasa,kule kwake amemkimbia kamanda Dr Yaledi Mfubusa msomi wa kimataifa,Zitto alijiona kwamba yeye ndo mwenye ubongo wenye kuweza kufikiria kuliko wakazi wa Kigoma wote.sasa amebaki kubung'aa hajui aende wapi amebakia kumlaumu Mkumbo kwa kumshauri vibaya na kumlaumu Mwigamba kwa kufanya uzembe wa kukamatwa na Pc yenye doc za usaliti zote
 
Zitto kama alisema hvyo basi ni mtu hatari wa kuogopwa.

Wakristo wa Kigoma Kaskazini walimwuliza kwamba anasema hawamtaki kutokana na dini yake,je 2005 walikuwa hawaijui dini yake?walipomchagua kwa kishindo?imebidi akimbie tu
 
Mmeshindwa ile move ya Limbu,amekula pesa zenu na mwisho ACT imesimama.

Sasa ni tunamalizia uchaguzi ndani ya chama na tarehe 29/03/2015 tutazindua chama rasmi na kuanza oparation za uzinduzi wa chama.

Hayo ndiyo yanayowazwa na ACT kuliki huo upuuzi ulioandika
 
Jamaa nao wanatumia "kanda" kweli alieanza kaanza! Wana-copy na ku-paste toka kwa baba yao.
 
Mmeshindwa ile move ya Limbu,amekula pesa zenu na mwisho ACT imesimama.

Sasa ni tunamalizia uchaguzi ndani ya chama na tarehe 29/03/2015 tutazindua chama rasmi na kuanza oparation za uzinduzi wa chama.

Hayo ndiyo yanayowazwa na ACT kuliki huo upuuzi ulioandika


Uchaguzi gani huo unaoendelea wakati hapa wilayanu Kibondo hakuna ACT
 
Mkuu Ben ukimsoma vizuri mtoa mada hapo juu utagundua ni Mogha mwenyewe. Anyway tuwaache na siasa zao tuuone mwisho wao

Uko sahihi kaka!! Mogha Hana uzalendo wowote, ni Mpenda sifa na madaraka ya umri mdogo mwaka juzi alikua chadema Leo yupo Act, Mwambie arudi shule..... Ajipange upya
 
Back
Top Bottom