GE2025 ACHPR yaitaka Tanzania kukomesha ukiukaji wa Haki za Binadamu Kabla ya Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
TAARIFA KWA UMMA

TUME YA AFRIKA YAKUBALI AZIMIO KUHUSU HALI YA HAKI ZA BINADAMU NCHINI TANZANIA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinakaribisha na kupongeza kwa dhati kupitishwa kwa Azimio ACHPR/Res.640 (LXXXIV) 2025 na Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR), wakati wa Kikao chake cha 84 cha Kawaida kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 21 hadi 30 Julai 2025.

Azimio hili, lililopitishwa katika ngazi ya bara, linaakisi wasiwasi mkubwa wa chombo kikuu cha haki za binadamu barani Afrika kuhusu kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini Tanzania, hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Katika uamuzi wake, ACHPR imesisitiza wajibu wa kisheria wa Tanzania chini ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na mikataba mingine ya kimataifa ya haki za binadamu iliyoidhinishwa na nchi, na kueleza wasiwasi mkubwa kuhusu:

1. Matumizi ya nguvu kupita kiasi kuvunja mikutano na maandamano ya amani, ikiwemo tukio la tarehe 9 Aprili 2025 kufuatia kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, na tukio la tarehe 24 Aprili 2025 katika Mahakama ya Kisutu ambapo viongozi na wafuasi wa upinzani walizuiwa kuhudhuria kesi hiyo.

2. Tuhuma za kupotezwa kwa watu kwa nguvu (enforced disappearances), mateso na kukamatwa kiholela, ambazo zimelaaniwa kimataifa na wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na Bunge la Ulaya.

3. Kufukuzwa na kukamatwa kwa viongozi wa kigeni na wanaharakati wa haki za binadamu, wakiwemo aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria na aliyewahi kuwa Jaji Mkuu wa Kenya pamoja na timu yake (tarehe 18 Mei 2025), na siku iliyofuata wanaharakati kutoka Uganda na Kenya, bila kupitia mchakato wa mahakama.

4. Vikwazo dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa, ikiwemo kufungiwa kwa mtandao wa X (zamani Twitter) tarehe 4 Juni 2025, kuwekwa kwa vikwazo kwenye YouTube, na kutofikika kwa majukwaa ya Clubhouse na Telegram bila kutumia VPN.

---

WITO WA ACHPR KWA SERIKALI YA TANZANIA

Kupitia Azimio hili, ACHPR imeitaka Serikali ya Tanzania:

1. Kuheshimu na kutekeleza viwango vya haki za binadamu katika mchakato wa uchaguzi.

2. Kufanya uchunguzi na kukomesha vitendo vya kupotezwa kwa watu kwa nguvu, mateso, kukamatwa kiholela, na kukandamiza mikutano ya amani.

3. Kuhakikisha uhuru wa kujieleza na upatikanaji kamili wa mtandao bila vizuizi.

4. Kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki, wa amani na wenye uwazi bila vitisho na vurugu.

5. Kuwalinda watetezi wa haki za binadamu na kuwawajibisha wahusika wa ukiukaji.

6. Kufanya uchunguzi na kutoa fidia kwa waathirika wa ukiukaji, wakiwemo wanaharakati wa kigeni walioteswa na kufukuzwa Mei 2025.

7. Kutekeleza maamuzi ya lazima ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, ikiwemo kuruhusu wagombea binafsi na kurejesha mamlaka ya mahakama za ndani kusikiliza mashauri ya uchaguzi.

---

MSIMAMO WA CHADEMA

CHADEMA inaona Azimio hili kama uthibitisho wa kihistoria wa hoja ambazo tumekuwa tukizitolea wito kwa muda mrefu kuhusu kudorora kwa haki za binadamu, nafasi ya kidemokrasia, na utawala wa sheria nchini Tanzania.

Azimio hili linatuma ujumbe wazi na usiopingika kwa Serikali: dunia inatazama, na mfumo wa haki za binadamu wa Afrika hautakaa kimya mbele ya ukandamizaji.

Tunazihimiza mamlaka za Tanzania kusikiliza na kutekeleza mara moja wito wa ACHPR, na kuchukua hatua za haraka kufanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi ili kuhakikisha mazingira bora ya uchaguzi wa kuaminika, wa amani, na wa kidemokrasia mwezi Oktoba 2025.

---

Imetolewa leo, Ijumaa, 08 Agosti 2025
................
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi


 
Lingewekwa hapa azimio la hiyo tume ya Africa ingependeza
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepongeza hatua ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) kupitisha Azimio ACHPR/Res.640 (LXXXIV) 2025, lililolenga hali ya haki za binadamu nchini Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Azimio hilo limepitishwa katika kikao cha 84 cha kawaida cha ACHPR kilichofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 21 hadi 30 Julai 2025.

Kwa mujibu wa CHADEMA, azimio hili linaonesha wasiwasi mkubwa wa chombo hicho cha haki za binadamu cha Afrika kuhusu kuzorota kwa uhuru wa kisiasa na haki za kimsingi nchini.



Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa ni ukatili wa kuvunja maandamano ya amani, ikiwemo tukio la 9 Aprili 2025 baada ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Tundu Lissu, na tukio la 24 Aprili 2025 katika Mahakama ya Kisutu, tuhuma za kupotezwa kwa watu kwa nguvu, mateso, na kukamatwa kiholela, ambazo zimekosolewa kimataifa, kufukuzwa na kuteswa kwa wanaharakati wa haki za binadamu wa kigeni Mei 2025, na vikwazo kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ikiwemo kufungiwa kwa mtandao wa X (zamani Twitter) Juni 2025.

ACHPR imeitaka Serikali ya Tanzania kuchukua hatua saba muhimu, ikiwemo kuheshimu viwango vya haki za binadamu katika uchaguzi, kufanya uchunguzi wa ukiukaji, kulinda watetezi wa haki, kuruhusu upatikanaji wa taarifa bila vizuizi, na kutekeleza maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, amesema azimio hili ni uthibitisho wa hoja ambazo chama hicho kimekuwa kikisisitiza kwa muda mrefu.

“Tunazihimiza mamlaka za Tanzania kusikiliza na kutekeleza mara moja wito wa ACHPR na kuchukua hatua za haraka kufanya mabadiliko ya sharia na kanuni za uchaguzi ili kuhakikisha mazingira bora zaidi ya uchaguzi wa kuaminika, wa amani, na wa kidemokrasia mwezi Oktoba 2025”, ameeleza Brenda katika taarifa ya CHADEMA ya siku ya Ijumaa tarehe 8 Agosti 2025.

Chanzo: Jambo online tv
 
Samia akilazimisha kujipitisha kuwa Rais kupitia huu mchakato ulioja ushetani wa kila namna, kamwe asitarajie kuwa atakuwa mshindi dhidi ya wanaotaka haki. Lazima atatawala kwa taabu sana, hata kujutia na kuishia kumlaumu mzoga na kundi lake walioamua kumtumia katika uovu wake.

Rais Samia aisikiize zaidi dhamira na roho yake, la sivyo asubirie kugundua kuwa shetani hana urafiki, na atakapofika hapo atakuwa amechelewa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…