Achilia na Songa Mbele

Achilia na Songa Mbele

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610
Mambo ya nyuma yasikufanye ushindwe kuifurahia leo yako au kupanga mipango kwa ajili ya kesho yako. Hakuna ambaye hajawahi kuumizwa iwe ni maisha/ mtu / watu au hali. Kinachotofautisha ni uamuzi wa kuachilia maumivu na machungu ya nyuma na kusonga mbele. Kuendelea kuyashikilia na kuyabeba kama bango haiondoi uhalisia kuwa yametokea wala hakufanyi leo yako kuwa nzuri.

Tambua kuwa maisha yako ni jukumu lako na si mwingine yeyote. Haijalishi umeumizwa vipi, unawajibika kuishi maisha yako kwa furaha na kufanya bidii ili kesho iwe bora zaidi. Aliyekukosea au kukusababishia maumivu hawajibiki kukupa furaha wala kukuondolea maumivu, ni jukumu lako asilimia mia. Amka sasa, jikung'ute maumivu yote na uchungu wa yaliyopita na usonge mbele.

Si kwa uweza wala nguvu zetu bali kwa msaada wa Mungu.
 
Kuyabeba ni mzigo mzito wenye athari kwa afya ya ubongo na mwili mzima. Keepin movin
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom