Acheni waseme, Vyuoni ndiko wasichana wengi wanakoharibikiwa

MWANAKB

Member
Jun 21, 2015
51
18
Vijana wanapo maliza elimu ya sekondari wenye bahati hujiunga na elimu ya kati na ya juu.

Ikumbukwe kuwa sekondari nyingi wanafunzi huishi chini ya sheria kwa uangalizi wa walimu, wazazi na matrons au patrons.

Vyuoni hakuna cha uangalizi huo. Wanapofika huko ni full kujiachia. Aliyekuwa wa kanisani kuimba kwaya na mapambio baadhi hugeuka waumini wa kumbi za starehe. Wale wa ushungi na nikabu hugeukia skin jeans na vitop kwenda na wakati

Aliyekuwa anasimuliwa ladha ya mapenzi naye hujikuta akibadilisha wanaume/wanawake kila kukicha akidhani atapata kitu cha ziada

Bahati mbaya sasa, hata baada ya kumaliza vyuo wanajisahau na kudhani hiyo ndo style ya maisha kumbe ni upotofu tu

Nilishuhudia mengi sana enzi hizoooooo na bahati mbaya sana maeneo yangu ya kazi ni karibu na mazingira ya chuo hivyo kila mara naishia kusikitika tu.

Kuna siku wanafunzi wa chuo fulani walimkosoa kiongozi fulani aliyekuwa anajaribu kuwasema kwa tabia kama hizi, waligadhabika kwamba wasitoe maelezo ya jumla, nami nikiri kuwa sio wote ila ki ukweli asilimia kubwa wako hivyo.

Usomi ni pamoja na kujitambua na kujithamini, kina dada chukueni hatua
 
Ni kweli ila Wengine tamaa tu ndo husababisha wengi tumeona Hasa Utakapo enda Field du Huwa Hawakataii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom