Acheni siasa: Wakulima na Wafugaji Morogoro

bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,131
2,000
Kwanza nianze kwa kuwapa pole wakulima wanaopigwa na hata kuuliwa na wafugaji huko Kilosa na Ifakara. Jana imeripotiwa mtu mmoja kufariki dunia baada ya kucharangwa mapanga na wafugaji. Poleni sana wafiwa.
Jana wakati nikiangalia taarifa ya habari, nilikutana na taarifa toka Longido ambayo inasema, "njaa imekuwa kali kiasi kwamba, wafugaji wanabadilisha debe moja la mahindi kwa mbuzi"

Hii ilinikumbusha habari za Yusufu katika biblia (Mwa. 47:16) "Yusufu akasema, toeni wanyama wenu, nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu, kama fedha zenu zimekwisha". Ukisoma sura yote hiyo ya 47 utagundua ni jinsi gani njaa ilikuwa imeipiga nchi ya Misri. katika mambo haya nilijifunza maswala kadhaa:

1. Haiwezekani kuishi na njaa, uwe mkulima au mfugaji, ukipigwa na njaa kama huko Loliondo au Misri lazima ujiuze hata wewe mwenyewe.

2. Chimbuko la vyakula ni wakulima, siyo wafugaji. Tangu mwanzo Mungu alimuumba mwanadamu kula mbegu (Nafaka) na mimea - mboga, matunda, mizizi, magome, n.k Kula nyama au wanyama ni uroho tu wa Mwandamu. Hivyo haiwezekani kuishi bila mimea.

3. Ugomvi wa wakulima na wafugaji uko toka enzi (Abeli - mkulima, alipomuua Kaini - Mfugaji). Na hata Misri, ukoo wa Yusufu walikuwa wafugaji, (Mwa. 46) na wakapewa nchi ya pembeni sana.

4. Unaweza kuishi bila wafugaji, na maisha yakaenda vyema kabisa, lakini hauwezi kuishi bila wakulima na ukabaki salama, HAIWEZEKANI! ni sawa na kusema unaweza kuishi bila mimea.Hivyo basi, pamoja na umuhimu wa wakulima, haimaanishi kuwa hatuhitaji wafugaji. Lakini ukiweka vipaumbele, lazima mkulima awe kipaumbele kabla ya mfugaji kwasababu hata mfugaji anamtegemea mkulima kwa chakula. Mfugaji anaweza akafiwa na mifugo yote na bado tukaishi, lakini mkulima akifiwa na mimea yote, lazima tutapigwa na njaa tu!

Longido mahindi yamefikia 22,000kwa debe, Kilosa mpunga unakwenda 110,000 kwa gunia, bei ya mbuzi na ng'ombe imeporomoka sana minadani (Mnada wa mwaka mpya tulinunua mbuzi mpaka kwa elfu 30) n.k. hii yote inatokana na njaa iliyopo ambayo inaweza kuwa imechangiwa na ukame, na uharibifu wa mazao ya wakulima toka kwa wafugaji.

Wito wangu: Serikali ya mkoa wa Morogoro isipokuwa makini, siyo tu kwamba tutapoteza watu katika mapambano ya wakulima na wafugaji, lakini pia tutakumbwa na njaa kwasababu mazao yanaharibiwa, na mashamba yamegeuzwa malisho. Tatueni hii migogoro haraka. Wakulima wasisumbuliwe na wafugaji, aitha wafugaji watengewe maeneo yao nao wasisumbuliwe.

Asanteni
 
engmtolera

Verified Member
Oct 21, 2010
5,150
1,250
kwa upande wange,ningependelea yale maamuzi ya mwaka 2009,juu ya wafugaji kwenda LINDI na MTWARA yangesimamiwa,maana wafugaji wanaharibu ardhi ambayo ndio tegemeo la wakulima na hata wakitengewa maeneo wao hawaheshimu mipika iliyowekea,hawaheshimu matumizi bora ya ardhi lakini pia RUSHWA kwa watendaji imekuwa ni tatizo sugu na wafugaji wanajivunia uwezo wa pesa walio nao.Serikali itekeleze maamuzi ya mwaka 2009 ya kuwatoa wafugaji wote kilosa na mkoa wa Morogoro kwa ujumla,ili lile wazo la Morogoro kuwa GHALA la Taifa la Chakula litekelezwe kwa vitendo,huu ni wakati wa kilimo ni muda wakulima kulima sasa kama wafugaji wanatumia mwanya huu kuingiza ng'ombe ktk mashamba bado inamkatisha tamaa mkulima,tuache siasa za majukwaani,kuongea nao wafugaji haitoshi,walishaongea nao sana lakini si waelewa,maamuzi ya kuwapeleka Lindi yatekelezwe
 
naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,688

Kwa hiyo Lindi na Mtwara hakuna wakulima kweli mnawachukulia poa
 
Likambaku

Senior Member
Mar 23, 2015
177
250
Mimi naona wakulima wanajilegeza ndio maana wanaonewa, wasipobadilika na kutetea haki zao wataonewa hadi mwisho wa dunia.Maeneo yote ambayo wakulima walikaza hakuna uonezi huo tena.
 
bhikola

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,131
2,000
Mimi naona wakulima wanajilegeza ndio maana wanaonewa, wasipobadilika na kutetea haki zao wataonewa hadi mwisho wa dunia.Maeneo yote ambayo wakulima walikaza hakuna uonezi huo tena.
Mkuu kwa signature yako hiyo, mbona ngachoka kabisa!!
back to topic: Tatizo la wakulima ni ile feeling ya unyonge kuwa, kulima ni last class job/option
 
engmtolera

Verified Member
Oct 21, 2010
5,150
1,250
Mimi naona wakulima wanajilegeza ndio maana wanaonewa, wasipobadilika na kutetea haki zao wataonewa hadi mwisho wa dunia.Maeneo yote ambayo wakulima walikaza hakuna uonezi huo tena.
Nakubaliana nawe,katika kijiji cha Mvumi Kilosa,wakulima uvumilivu uliwashinda na kilichotokea ni kwamba kila mtu anafahamu.Lakini kama wakulima wakiamuwa kujilinda itakuwa ni vita kubwa na ndio maana wakulima wanaiachia serikali ifanye maamuzi ni jambo jema ili kuweza kuendeleza amani tuliyonayo,cha msingi hapa ni wafugaji kuheshimu mipaka na kufuata maeneo waliyotengewa
 
ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,436
2,000
Nawapa wana Longido,kuna maeneo maindi bado yana range 8000 mpaka 15000 kwa debe!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom