Acheni kuwauliza wanandoa lini wanapata watoto

Mkuu;
Kwanza niseme; Sijawahi kupata shida katika kuzaa hadi nikawakataa mwenyewe kuwa sitaki tena. Ila, huwa napambana na mtu yeyote anayewasumbua wana ndoa kwa habari za kuzaa. Yaani wengine ni kero hadi wanawafanya wanandoa wanachepuka. Kisa, mmechelewa kupata mtoto. Hii ni dhambi mbele za Mungu. Haikubaliki.
Nilipoenda kuoa sikuenda kutafuta watoto bali mwenzi wa maisha. Anipende yeye nami nimpende yeye. Ningelitaka mtoto ningemzalisha kwanza ndipo nimuoe. Lakini neno la Mungu linatunyima kumjua kabla ya ndoa. Viongozi wengi wa dini haswa za Wapentekoste hawaifungi ndoa mwanamke akiwa na ujauzito unaoonekana. Sasa hapo si ni pata potea??
Yawezekana pia tumepanga uzazi kutokana na malengo mazuri tuliyo nayo. Labda, tumalize ujemzi kwanza na kama mwenzangu akiwa mbali nami, naweza nikatenda dhambi ya uzinzi. Sasa tukapatana tuoane, tuzuie mimba miaka 3 halafu ndo tuanze uzazi. Yawezekana mwenzangu anataka kusoma zaidi, hatuwezi kuchukua majukumu yote hayo kwa pamoja ila tuende kwa mpango. Swali; Wewe mama mkwe/mawifi/jirani mna shida gani na nyumba yangu??
Jambo hili ni la kukemea na kuwadharau hadi mwisho. Mnaopitia majaribu haya, wekeni pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao msiwasikilize hao wambeya.
Asante mkuu
 
Wenye tabia hizo ni waswahili wa kutupwa, kwani haiwezekani baada ya ndoa mtu akajipa hata miaka 3 bila kuzaa mtoto ili apate faragha na mda wa kula maisha na waifu kabla ya mtoto?
 
Daaah mie ni mmoja wao aisee kukutana na changamoto hizo kutoka kwa watu mpaka nikawa nazuga sasa kuwa tunakula ujana kwanza, ila namshukuru Mungu sasa mambo safii, watanzania utafikiri watakusaidiia kulea
 
Hahahahaha. Umenichekesha. Mimi nawambia hawajaja na wala sina peessure, wanaishia kuhuna
 
Hahahahaha. Umenichekesha. Mimi nawambia hawajaja na wala sina peessure, wanaishia kuhuna
Wanaboa balaaa yaani mpaka sometimes unashindwa attend Sherehe za Ndugu maana ukifika ndio swali lao la kwanza vip mtoto? haa haaa hawajui mzee mnapambana
 
Pole sana mkuu nakuelewa,mimi nilipo olewa nilipanga staki kuzaa nijipe kama 2-3 yrs ku enjoy na kujipanga,ila haikua hivyo nimerudi Honeymoon nakuta mtoto wa mume wa 3months nimeletewa na mzazi mwenzie,haya nikakubali kulea,baada ya hapo wakaanza mmm jamani mbona hajataga wala hajaengua ila uzazi upoo? nikienda kwao kusalimia unasikia vipi bado tuuuuu? mashemeji na wifi wanafikia kusema au bro una shuti njee goli unaliwacha? ilikua inanikera kua why wanataka kuingilia maisha yetu? wakati huyo wifi anaongea hivyo yeye ameolewa mwaka wa 3 hana mtoto sasa sijui mumewe ana sahau wapi sehemu husika,ilifikia ikawa kwao siendi,kukiwa na shughuli ukienda ndio mabibi zao tena vipi bwana ebu njoo nikufundishe umueweke mkao gani,mwisho nikasema wacha sasa nianza kujaribu,mimba ya kwanza nikazaa twins..
sasa wewe usikate tamaa,ni wakati haujafika hata mdogo wangu alikua na tatizo hilo kuna bibi Zanzibar ana tibu watoto wa changa na Wanawake anakupa dawa zakuchemsha zilimsaidia sana sasaivi Alhamdulillah amepata watoto na yuko kawaida..
 
Sijui ni Watz wanapenda kuzaa zaa hata sielewi mwingine ndio amekutana na mtu utasikia "unaitwa mama/baba nani?"

seriously!!
 
Pole sana mkuu nakuelewa,mimi nilipo olewa nilipanga staki kuzaa nijipe kama 2-3 yrs ku enjoy na kujipanga,ila haikua hivyo nimerudi Honeymoon nakuta mtoto wa mume wa 3months nimeletewa na mzazi mwenzie,haya nikakubali kulea,baada ya hapo wakaanza mmm jamani mbona hajataga wala hajaengua ila uzazi upoo? nikienda kwao kusalimia unasikia vipi bado tuuuuu? mashemeji na wifi wanafikia kusema au bro una shuti njee goli unaliwacha? ilikua inanikera kua why wanataka kuingilia maisha yetu? wakati huyo wifi anaongea hivyo yeye ameolewa mwaka wa 3 hana mtoto sasa sijui mumewe ana sahau wapi sehemu husika,ilifikia ikawa kwao siendi,kukiwa na shughuli ukienda ndio mabibi zao tena vipi bwana ebu njoo nikufundishe umueweke mkao gani,mwisho nikasema wacha sasa nianza kujaribu,mimba ya kwanza nikazaa twins..
sasa wewe usikate tamaa,ni wakati haujafika hata mdogo wangu alikua na tatizo hilo kuna bibi Zanzibar ana tibu watoto wa changa na Wanawake anakupa dawa zakuchemsha zilimsaidia sana sasaivi Alhamdulillah amepata watoto na yuko kawaida..
Asante sana.
 
ARCHBISHOP ,

Pole sana mkuu.

Ndiyo maana bongo ukiweka hata kituo kikuu (period/ full stop yaani nukta ) kwenye karatasi nyeupe maelezo yatanyooshwa hadi utashangaa.

Ni tabia mbaya sana.
 
Daaah mie ni mmoja wao aisee kukutana na changamoto hizo kutoka kwa watu mpaka nikawa nazuga sasa kuwa tunakula ujana kwanza, ila namshukuru Mungu sasa mambo safii, watanzania utafikiri watakusaidiia kulea
Shida Kweli.
Mimi Miezi 2 tu Baada ya ndoa walishaanza kuhoji:Tayari?
Hajaanza kula maembe machanga ?nk nk.
Inakera Sana.
 
Nakumbuka kaka yangu alikataza ndugu wote wenye fyoko fyoko kufka kwake kuanzia madada, mama wakubwa na wadogo, walikua wanajitia kuja kusalimia kumbe bro akitoka tu nikumkosesha shem amani kbsa, maneno meng ya kashfa kwa kukosa mtoto. Kumbe ilikua ni mipango tu wakae kwa mda flan.
 
Ndoa sio mali ya wanandoa tu,ni mali ya jamii pia.Ndio maana kabla ya ndoa walikuuliza utao lini,baada ya ndoa wanasubiri watoto.Mkizaa mtoto mmoja tu,watahoji kwanini mtoto mmoja tu.Mkizaa watoto wote wa kike tu,watahoji kwanini watoto wote ni wakike.Kifupi maswali hayaishi kwani nao ni wadau hiyo ndoa.
 
Back
Top Bottom