Achaneni na Lowassa Magufuli ndiye Rais!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,410
38,701
Vyovyote ilivyokuwa na ndivyo ilivyo, John Pombe Magufuli ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Wale wote ambao kila siku wanataka kuwaonesha watanzania kwamba Edward Lowassa kugombea Urais kupitia CHADEMA lilikuwa ni kosa la Karne, wanaturudisha nyuma ya wakati hali ambayo haitusaidii kwa lolote.

Hoja kwamba kama angekuwa Wilbroad Slaa ndiye mgombea Urais basi CHADEMA ingeshinda, ni ya uongo kabisa. Slaa aligombea Urais mwaka 2010 na hakushinda. Na hakushinda si kwa kuwa hakushinda, bali hakushinda kwa kuwa hakutakiwa kushinda. Hao wasiotaka vyama vingine zaidi ya CCM kushinda ni kitu gani kingewafanya wakubali Slaa ashinde mwaka 2015?

Kumshupalia Lowassa na kushupalia "kosa" la CHADEMA kumsimamisha kuwa mgombea wao wa Urais ni kupoteza wakati. Kama kuna Mkuu wa Mkoa kaghushi vyeti na inajulikana na hafukuzwi kazi wakati kazi yake sifa kuu ni kujua kusoma na kuandika tu, hapo tatizo si Lowassa kugombea Urais mwaka 2015 bali kosa ni mtizamo wa mamlaka ya uteuzi.

Kama watumishi wa umma hawaongezwi mshahara, hawapandishwi madaraja, fao la kujitoa linafutwa, fedha zao zilizoko kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zinatumiwa na serikali bila ya wao kushirikishwa wakati wao wanacheleweshewa Pensheni zao, wanazuiwa kubadili kazi, wanadhalilishwa na hata kufukuzwa kazi bila ya kufuata sheria na taratibu zilizopo, hapo chanzo si Lowassa kugombea Urais Mwaka 2015.

Kama kuna watu wanaona mambo hayaendi kwenye nchi yetu, wajue nchi hii ina serikali na serikali hiyo haiongozwi na Lowassa bali Magufuli. Kama kuna mtu anaona serikali haitendi kile kinachotarajiwa, basi wasikimbilie kusema kwamba kosa ni CHADEMA kumsimamisha Lowassa kuwa Mgombea Urais mwaka 2015.

Kama mnashindwa kumkosoa Magufuli hasira zenu msizihamishie kwa Lowassa.

CC: Mzee Mwanakijiji Nguruvi3 JokaKuu
 
Vyovyote ilivyokuwa na ndivyo ilivyo, John Pombe Magufuli ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Wale wote ambao kila siku wanataka kuwaonesha watanzania kwamba Edward Lowassa kugombea Urais kupitia CHADEMA lilikuwa ni kosa la Karne, wanaturudisha nyuma ya wakati hali ambayo haitusaidii kwa lolote.

Hoja kwamba kama angekuwa Wilbroad Slaa ndiye mgombea Urais basi CHADEMA ingeshinda, ni ya uongo kabisa. Slaa aligombea Urais mwaka 2010 na hakushinda. Na hakushinda si kwa kuwa hakushinda, bali hakushinda kwa kuwa hakutakiwa kushinda. Hao wasiotaka vyama vingine zaidi ya CCM kushinda ni kitu gani kingewafanya wakubali Slaa ashinde mwaka 2015?

Kumshupalia Lowassa na "kosa" la CHADEMA kumsimamisha kuwa mgombea wao wa Urais ni kupoteza wakati. Kama kuna Mkuu wa Mkoa kaghushi vyeti na inajulikana na hafukuzwi kazi wakati kazi yake sifa kuu ni kujua kusoma na kuandika tu, hapo tatizo si Lowassa kugombea Urais mwaka 2015 bali kosa ni mtizamo wa mamlaka ya uteuzi.

Kama watumishi wa umma hawaongezwi mshahara, hawapandishwi madaraja, fao la kujitoa linafutwa, fedha zao zilizoko kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zinatumiwa na serikali bila ya wao kushirikishwa wakati wao wanacheleweshewa Pensheni zao, wanazuiwa kubadili kazi, wanadhalilishwa na hata kufukuzwa kazi bila ya kufuata sheria na taratibu zilizopo, hapo chanzo si Lowassa kugombea Urais Mwaka 2015.

Kama kuna watu wanaona mambo hayaendi kwenye nchi yetu, wajue nchi hii ina serikali na serikali hiyo haiongozwi na Lowassa bali Magufuli. Kama kuna mtu anaona serikali haitendi kile kinachotarajiwa, basi wasikimbilie kusema kwamba kosa ni CHADEMA kumsimamisha Lowassa kuwa Mgombea Urais mwaka 2015.

Kama mnashindwa kumkosoa Magufuli hasira zenu msizihamishie kwa Lowassa.

CC: Mzee Mwanakijiji Nguruvi3 JokaKuu

Lowasa ni Fisadi na ataaongelewa mpaka siku ya mwisho anazikwa na hata baada ya hapo tutaandika kaburi lake RIH Fisadi Lowasa!
 
Acha ujinga wewe mleta mada.... Unamjadili mtu ambaye ni ugonjwa wa kudumu wa rais wako??? Na ulichofanya hapa ni kumpa air time tu.
 
Mkuu, Niliposoma Heading nilishandaa TUSI kubwa sana la kunipa BAN kabisa, ila niliposoma content nimekuelewa na nimeshaomba Msamaha kwa Mungu kwa nilichokua nawazia.

Uzi wako ni fikirishi sana, hawa akina Barbarosa wamesahau kabisa ufisadi wa mwenyekiti wao wanang'ang'ana na Lowassa, wakati mwengine hua najiuliza sana ukiwa KADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI ni lazima akili zirudi kwenye Masaburi(RIP)?
 
Back
Top Bottom