Achaneni na Lowassa Magufuli ndiye Rais!

Vyovyote ilivyokuwa na ndivyo ilivyo, John Pombe Magufuli ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Wale wote ambao kila siku wanataka kuwaonesha watanzania kwamba Edward Lowassa kugombea Urais kupitia CHADEMA lilikuwa ni kosa la Karne, wanaturudisha nyuma ya wakati hali ambayo haitusaidii kwa lolote.

Hoja kwamba kama angekuwa Wilbroad Slaa ndiye mgombea Urais basi CHADEMA ingeshinda, ni ya uongo kabisa. Slaa aligombea Urais mwaka 2010 na hakushinda. Na hakushinda si kwa kuwa hakushinda, bali hakushinda kwa kuwa hakutakiwa kushinda. Hao wasiotaka vyama vingine zaidi ya CCM kushinda ni kitu gani kingewafanya wakubali Slaa ashinde mwaka 2015?

Kumshupalia Lowassa na "kosa" la CHADEMA kumsimamisha kuwa mgombea wao wa Urais ni kupoteza wakati. Kama kuna Mkuu wa Mkoa kaghushi vyeti na inajulikana na hafukuzwi kazi wakati kazi yake sifa kuu ni kujua kusoma na kuandika tu, hapo tatizo si Lowassa kugombea Urais mwaka 2015 bali kosa ni mtizamo wa mamlaka ya uteuzi.

Kama watumishi wa umma hawaongezwi mshahara, hawapandishwi madaraja, fao la kujitoa linafutwa, fedha zao zilizoko kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zinatumiwa na serikali bila ya wao kushirikishwa wakati wao wanacheleweshewa Pensheni zao, wanazuiwa kubadili kazi, wanadhalilishwa na hata kufukuzwa kazi bila ya kufuata sheria na taratibu zilizopo, hapo chanzo si Lowassa kugombea Urais Mwaka 2015.

Kama kuna watu wanaona mambo hayaendi kwenye nchi yetu, wajue nchi hii ina serikali na serikali hiyo haiongozwi na Lowassa bali Magufuli. Kama kuna mtu anaona serikali haitendi kile kinachotarajiwa, basi wasikimbilie kusema kwamba kosa ni CHADEMA kumsimamisha Lowassa kuwa Mgombea Urais mwaka 2015.

Kama mnashindwa kumkosoa Magufuli hasira zenu msizihamishie kwa Lowassa.

CC: Mzee Mwanakijiji Nguruvi3 JokaKuu
Ngoja mimi niendelee kubet ndio ajira pekee iliyobakia.
 
Teh teh teh
Huyu dikiteta aliyefuta ajira za watoto masikini? nimecheka sana kusikia wachumia matumbo wanasema bajeti itamuinua mtu wa chini. labda kama siyo chini ya dikiteta na siyo chama cha majambazi na wala rambi rambi.
 
tapatalk_1494143828235.jpeg
 
Kazi ni pamoja na kupitia mikataba mibovu inayoitia hasara Tanzania?
Tangia serikali ya ******** ifute ajira, niliiona hii serikali ya kifala sana. Na siwezi kuwa mzalendo hata kidogo.
Huyu dikiteta uchwara unayempigia upatu, angalia dhambi zake zikakutafuna hadi ww.
Huyo ******** ni raisi wako lkn mm kwa sasa namtambua km mwenyekiti wa ccm na siyo raisi
 
Tabaka la yaliyopita hari mbaya sana. Mlizoezwa vilaini laini tu na kumezeshwa, sahivi ni vigumu vigumu tu tena unatafuta na kutafuna mwenyewe. The past is history!
 
Tabaka la yaliyopita hari mbaya sana. Mlizoezwa vilaini laini tu na kumezeshwa, sahivi ni vigumu vigumu tu tena unatafuta na kutafuna mwenyewe. The past is history!
Kuna mtu kaja kukuomba umlishie familia yake? Hali mbaya si leo bali watu wanaangalia tuendako. Kila jambo la maana linafanywa kwa mkopo!
 
Back
Top Bottom