USIOGOPE SHIKILIA HAPO HAPO.
Na, Mwl. Pasaka O. Rucho.
Aliyewahi kuwa Rais wa Marekani aliwahi kusema "the only thing we have to fear is fear itself" kwa lugha yetu jambo pekee tunalopaswa kuliogopa ni uoga wenyewe.
Kuna sintofahamu kati yetu Tanzania na ndugu zetu wa jumuiya ya Afrika Mashariki haswa kwa upande wa Kenya, ambako siku ya jana tarehe 16/05/2020 akilihutubia taifa Rais wa Kenya alisema ameufunga mpaka wake na Tanzania pamoja na Somalia kwa siku 30 kama njia ya kupambana na Corona.
Sitaki kuzungumzia sana mpaka wao na Somalia ila nataka nizungumzie mpaka wetu na Kenya, naomba niwakumbushe majirani zangu wa Kenya, Corona ilianzia China siyo Tanzania, wasitake kututendea kama wa China sisi bado ni ndugu zao.
Zoezi la kufunga mpaka na kuendelea kutaka kuitenga Tanzania ni miongoni mwa dhambi za usaliti ambazo zinaendelezwa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa wale wafuatiliaji wa habari 12/05/2020 aliyekuwa waziri wa mambo ya nje akihojiwa na DW alisema diplomasia yetu na dunia imeshuka sana kwa awamu hii imeshuka sana na nchi majirani zitaendelea kutufungia mipaka.
Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JPM, the only thing to fear is fear itself, hawa watu hawajaanza kututenga leo achana na upupu wa Membe, kwani mwaka 2013, mahusiano yetu na nchi hizo ulikuwa mzuri?, Membe alikuwa hatembei? Mbona mahusiano yaliharibika?
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mtu akizoea kula nyama ya mtu hawezi acha, majirani zetu wamezoea kututenga hawawezi acha hata kidogo.
Akilihutubia bunge Rais mstaafu Kikwete 2013 baada ya majirani zetu hawa kututenga kwa sababu kuwa.
.Tanzania imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya jumuiya
.Tanzania haina moyo wala dhamira ya dhati ya kuendeleza jumuiya.
Rais kikwete alisema "licha ya kuwa tunatengwa lakini sisi Tanzania hatupuuzi maazimio ya jumuiya ila yapo mengine yanakwaza" akaenda mbali na kusema kuwa "hakutukanaye hakuchagulii tusi " mwisho akamalizia kwa kusema "kinachotupa taabu ni msimamo wetu".
Tatizo hili la 2013,limejirudia tena 2020 kwa nchi hizo Marais wa nchi hizo bado ni wale wale sisi tulishabadilisha Rais, lakini usaliti wao umebaki pale pale.
Kinachotupa taabu ni msimamo wetu, majirani zetu wanataka tuwekwe lockdown kama maembe?
Tuwekwe lockdown kama mbuzi, ngombe na udagaa?
MH.JPM, wasikutishe sisi ungetuweka lockdown tungekufa wengi sana kwa mawazo na njaa, unawaona wanavyoteseka, kipindi nchi zingine zinafungua lockdown na mipaka wenyewe ndipo wanatufungia hapana usiwaze mh. Rais tuko kwenye mstari sahihi.
Mh.Rais Ulisema ugonjwa huu tunaweza kuishi nao kama surua na ukimwi, na WHO wakaufyataaa, sikiliza shikilia hapo hapo si mara ya kwanza kututenga hata mwl.Nyerere walimchokoza akawatandika.
Mh.Rais nashukuru mpaka wetu hujafunga,ila wao wamefunga mtu akifunga chumba chake acha afunge ila najua atafungua tuuu, usiogope kamatia hapo hapo.
Mwisho nitoe rai kwa Watanzania wenzangu tuungane na Mh.Rais katika mapambano haya tufanye kazi kwa bidii, tumwombe mwenyezi Mungu ambaye ndo tegemeo letu, na tusiogope kufungiwa mipaka, ipo siku wakijua thamani yetu watafungua.
0756231744.