Acha wafu wazike wafu wao


God'sBeliever

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Messages
5,863
Likes
2,617
Points
280
God'sBeliever

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2015
5,863 2,617 280
Habari za wakati huu wanaJF
Natumai kwema kabisa na wale wengine ambao mambo hayajawaendea vyema basi muongeze jitihada na kutatua matatizo hayo.

Husika na kichwa cha mada hapo juu.
Mimi kama mtanzania wa kawaida niliekulia maisha tuu ya kupambana mimi na wazazi namshukuru Mungu tumekua tukila ugali wa halali na ndio nitakaoupigania mpaka pale maulanaa atakapo niita kwenye makazi ya milele.

Tangu nimekua na sasa kijana nimekua nikisikia habari ziisizo za kibinadamu hasa uuaji wa raia na kuwapora, kuwatesa na kuwafanyia mambo mengine yasiyo ya kibinadamu.

Lakini kwa nini hii?
JIBU: Ni kutokana na haki na ukweli waliyokua wakiipigania. Wengi wao ni upinzani kama ilivyokawaida halafu ule upande mwingine ni hivyo hivyo ila kimaslahi zaid wanamalizana wenyewe.

Wapigania haki na usawa nchi hii wamekua watumwa na wanyama wakati wale mafisadi na wauaji wakiendelea kupongezwa na kupandishwa nafasi.

Hii inauma sana sana.
Lakini kama mnyonge ni lazima uitete haki yako... Ukicheka na nyani utavuna mabua..

Je kwa hali hii tutafika? Jibu No.

Sasa tufanyeje"
Sasa ni vyema watanzania kuamka, kuacha woga na kuwa jasiri! Sio kupelekeshwa tuu na kufanya vitu visivyo faa. Tuepuke kulishwa matango pori na vitu vingine visivyo na msingi.
Lazima watanzania muwe smart, mshikamane kwa hali na mali na mkiona kitu kisicho faa ni bora msishiriki kabisa. Maana hilo ndilo jambo jema kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.
Kumbuka zao la uoga ni unafiki, dhuluma n.k...

Wapo waliodhalilishwa, kwamishwa kwenye mambo mbali mbali ya kimaisha ila isiwe sababu ya nyie kulegea bali iwe mwanga kwa watanzania wengine wajue mambo yanavyokwenda.

Ni lazima kuwa makini na kuepuka vizawadi vya muda mfupi vyenye kunufaisha watawala.
Angalia kitu kitakacho nyanyua jamii nzima na iwe motivation kwa watanzania wote.
Usiwe mtu wa kusikiliza/kupumbazwa tuu na sifa za kijinga bali simamia uhalisia. Jali mamilioni ya watanzania wanaokufa kwa kukosa dawa hospitalini humo, wanaokosa haki yao ya msingi ya elimu, ajira, usafiri n.k yote hii sababu ya rushwa.

Vita ya rushwa ni yetu sote, laumu kwa nini mafisadi hao hawapigwi na mabomu, risasi au sumu na badala yake wanapora kodi yenu watanzania.

Kodi mnatoa nyinyi na lazima pesa itumike kwa maendeleo yenu sio iishie kwa matumbo ya majizi fulani.

Pingeni ujinga jikomboeni kifikra nasema hivi kwa sababu ukosefu wa maarifa ndo umetufikisha hapa. Jitambueni kwanza ndipo mchukue maamuzi sahihi. Msiwe punda kutembezwa tembezwa tuu kusikofaa. Tanzania ya kisasa inaanza na mimi na wewe sio unakua mtizamaji tuu bila kushiriki. Inashangaza watu timamu kuongozwa na wajinga sababu ya nidhamu yenu ya woga.

Unaweza kujifunza kwa mataifa kadhaa ya Asia yaliyoamua kuacha siasa za kijinga na kuzijenga nchi zao na sasa wako vyema kila idara. Mf vietnam, korea, china n.k

Mkiona wahusika wanasasimanga, wanawakejel hata wakiwatemea mate jifuteni na endeleeni na safari huku mkisimama imara bila kuyumbishwa na mtu au kitu chochote kile.

Imekua kama desturi mtu akiamua kuwa mpinzani basi vikwazo, matusi na mambo yote yasiyofaa anafanyiwa yeye, hili ni jambo baya sana watanzania msikubali kuendeshwa na wajinga humu.

Ndio maana yake ACHA WAFU WAZIKE WAFU WAO.
Tumechoka na huu utawala wa muda mrefu usiojali raia wake.
Ni lazima kutafuta njia sahihi tupate kuwakomboa watanzania wenzetu.
Long live upinzani, tutafika tuu Mungu yupo nasi.
 
Mwalimu kp

Mwalimu kp

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Messages
424
Likes
255
Points
80
Mwalimu kp

Mwalimu kp

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2011
424 255 80
Toa tongotongo kwanza mtoa post!
 

Forum statistics

Threads 1,235,504
Members 474,615
Posts 29,224,955