Bullshit
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 1,300
- 1,495
Huu ni ushauri kutoka kwa rafiki yangu.
Hello JamiiForums,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26. Nimeajiriwa na vilevile nina biashara yangu binafsi, lakini nina ndoto za kurudi shule ambayo inaweza kunichukua miaka saba hivi.
Nimepata pingamizi kutoka kwa rafiki wangu wa karibu akidai kuwa haoni kama nina uhitaji wa elimu.
Aliendelea kwa kusema kwamba ulimwengu wa sasa elimu iko mikononi mwako ni wewe sasa kuitumia maana watu wengi wanasoma ili waajiriwe na haoni sababu ya mimi kufanya hivyo, na pia nina mwanzo mzuri wa maisha naweza kutumia akili yangu kupanunua na kukuza biashara yangu.
Muda utakaopoteza shule ni muda wa wewe kuitwa millionea.
Aliniambia nifanyie tathmini miaka saba ya shule na miaka saba ya kufanya biashara. Alimaliza kwa kuniambia kwamba yeye binafsi alijutia sana muda alioupoteza chuo kikuu na elimu ya chuo haikumsaidia kitu, kilichomsaidia kufikia mafanikio yake ni akili yake binafsi, juhudi zake binafisi na kujiamini. Laiti asingeenda chuo miaka minne (4) pale chuo, ilitosha yeye kufanya kitu cha kumpa maandeleo.
Mwana JamiiForums, na wewe unaweza kutoa mtazamo wako.
Asante na karibu!