Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
ACHA KUJIPIMA KWA UBIZE ULIONAO JIPIME KWA KILE UNACHOZALISHA
Kuwa bize na kuzalisha ni vitu viwili tofauti kabisa.Mara nyingi wale wanaoonekana kuwa bize sana huwa wanakuwa na uzalishaji mdogo sana, japo wao wanaweza kufikiri kinyume chake.
Kila mtu anaweza kuwa bize, lakini ni wachache sana wanaoweza kuwa na uzalishaji mkubwa.Unaweza kuwa bize kwa kufanya mambo ambayo hayana mchango mkubwa kwako na kwa mafanikio yako ila unapopima uzalishaji, unapima kile hasa ulichofanya ambacho kinakusogeza mbele zaidi.
Lengo langu leo sio wewe uache kuwa bize na uwe mvivu, bali ni wewe uache kukazana na ubize na badala yake ukazane na uzalishaji. Je ni kiasi gani umezalisha? Je ni wapi unaweza kuboresha zaidi?
Sehemu kubwa ya mambo yanayokuweka bize, sio muhimu sana kwako kiasi kwamba hata usingeyafanya bado maisha yako yangeendelea kuwa bora. Na hata kama kuna ambayo ni muhimu basi kuna wengine wangeweza kuyafanya vizuri na wewe ukabaki na muda akutosha kufanya yale ambayo ni muhimu kwako.
Kama unataka kufikia mafanikio makubwa unayotazamia, acha kujipima kwa ubize na anza kujipima kwa kile unachozalisha.