GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,285
- 6,729
Hili tukio ni la miaka minane iliyopita lakini nimelikumbuka sana na linanifanya
niwaone hawa viumbe kuwa ni tofauti na tunavyowafikiria.
Nilikuwa nimepanga nyumba fulani maeneo ya Malawi(Yombo) hapo kuna Derevaanaishi na mkewe pia tulikuwapo wapangaji wengine wanne. Wote tulikuwa Wahuni wanawake watatu na mimi mwenyewe.
Kabla ya tukio yule Bwana (Dereva) alikuwa amesafiri kuelekea Kongo ambapo aliadimika pale nyumbani zaidi ya mwezi mmoja,kama mara mbili hivi niliwahi kumshuhudia mkewe akiingiza mwanaume ndani(Usiku) wakati jamaa akiwa safarini.
Siku ya Tukio huyu dada alikuwa ameingiza mwanaume kama alivyozowea, kumbe siku hiyo mumewe alikuwa amerudi bila taarifa. Dada mmoja wa chumba jirani akanifuata na kuniambiayeye anaondoka kwa kuogopa ushahidi. Nikamuuliza ushahidi wa nini? Akaniambia yule mke wa dereva kaingiza mwanaume na mumewe karudi hayuko mbali kamuona dukani anapata mahitaji fulani na jinsi anavyomfahamu jamaa ana hasira sana anaweza kuua. kweli haukupita muda mrefu yule jamaa akaingia.
Huku nikiwa na hofu ya kitakachotokea nikasimama mlangoni na kuchungulia, haikunipa shida kwa kuwa vyumba vyetu vilikuwa vinatazamana. Yule Mwanamke alichelewa kufungua mlango kama dakika moja hivi. Alichokifanya sasa baada ya kufungua.!
Alimrukia mumewe huku akimfunika na shuka usoni akisema Waooooooo mume wangu! Wakati anamfunika ile shuka na mumewe anahangaika kuitoa huku akilalamika kwa kusema "Acha mke wangu mi nimechoka bana" Na ndio wakati huohuo mwanaume aliyeko ndani alitumia kupita mlangoni kwa kasi bila kushtukiwa.
Yaani tukio hili halinitoki akilini na limenifanya niyaogope mapokezi ya ajabuajabu.