Acacia kuilipa TRA zaidi ya Sh40 bilioni

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,589
Reaction score
28,755
Baada ya kutuhumiwa kukwepa kodi kwa miaka mitatu mfululizo, kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Acacia imesema inatarajia kulipa kodi ya zaidi ya Sh40 bilioni mwaka huu wa fedha.

Mwishoni mwa Machi, Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT) iliitaka African Gold Mine (kwa sasa Acacia) kuilipa Serikali kodi ya Dola za Marekani 41.25 milioni (zaidi ya Sh89 bilioni), lakini kampuni hiyo ilikata rufaa na shauri hilo linasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Acacia inayomiliki Kampuni tatu ndogo za Bulyanhulu Gold Mining, North Mara na Pangea Minerals zinazoendesha shughuli zote za mapato ya mchimbaji huyo mkubwa kuliko wote nchini ambaye anaelezwa kukwepa kodi ya zuio la malipo ya gawio kwa wanahisa wake.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bradley Gordon ambaye aliwasili jana ili kutembelea miradi hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wake, alisema Acacia bado haijaanza kutengeneza faida za kulipa kodi ya Mapato ya Kampuni kwa kuwa bado haijarudisha mtaji wake wa awali.

“Pamoja na kwamba tunatengeneza faida kwa jumla, hiyo haitozwi kodi kwa sababu bado hatujarudisha mtaji wa Dola za Marekani 3.8 bilioni. Mkataba wetu na Serikali ya Tanzania unaonyesha kuwa tutatakiwa kuanza kufanya hivyo kuanzia mwaka 2018,” inasomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na Gordon.

Makamu wa Rais wa Acacia, Deo Mwanyika alisema kuwa kampuni hiyo inaanza kulipa kodi ya mapato mwaka huu baada ya kurejesha mtaji wake iliyowekeza kupitia kampuni yake ya North Mara. “Tumerudisha mtaji wetu na makadirio yanaonyesha tunaweza kulipa kodi ya Dola 20 milioni za Marekani (zaidi ya Sh40 bilioni). Nusu ya kiasi hicho tayari kimeshapelekwa TRA,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Naona 2018 tanzania itakuwa kwenye mwendo kasi wa KPH 80 toka KPH 30 magufuli on fire
 
Source: Mwananchi
Mbona taarifa za Mr Gordon na Mwanyika zinakinzana? huyu anasema 2018 huyu anasema mwaka huu washapeleka nusu, mnaweweseka sana na mtalipa, msitegemee ujanja wenu haujulikani. mnagawaje bonus bila kupata faida? taraibu ya bonus ni kwamba ukishatangaza faida gafi ukakata ushuru ikibaki faida halisi ndo huwa unatoa gawiwo, sasa ilikuwaje ikawa kinyume au mnahisi sheria za haya mambo mnazijua nyie tu? mlipe kodi zetu. period.
 
Unashangaa nini hapo, ni kawaida pale kibano kinapotembea watuhumiwa kuanza kukinzana kimaelezo, especially wanapokua wamebanwa kwenye vyumba viwili tofauti.

Anyways, nadhani huyo bw. Deo atakua amewaeleza wakuu wake wa London kua huyu Magu hataki mchezo ni bora tu kulipa.
 
mkuu inabidi magu achukue tahadhar sana na mabepari
 
Majizi tu,eti kulipa kodi had I mtaji urudi,sijaona hiyo popote duniani
Hiyo 2018 kabla haijafika watabadili jina
 
Baada ya kutuhumiwa kukwepa kodi kwa miaka mitatu mfululizo, kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Acacia imesema inatarajia kulipa kodi ya zaidi ya Sh40 bilioni mwaka huu wa fedha.

Mwishoni mwa Machi, Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT) iliitaka African Gold Mine (kwa sasa Acacia) kuilipa Serikali kodi ya Dola za Marekani 41.25 milioni (zaidi ya Sh89 bilioni), lakini kampuni hiyo ilikata rufaa na shauri hilo linasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa Tanzania.

Acacia inayomiliki Kampuni tatu ndogo za Bulyanhulu Gold Mining, North Mara na Pangea Minerals zinazoendesha shughuli zote za mapato ya mchimbaji huyo mkubwa kuliko wote nchini ambaye anaelezwa kukwepa kodi ya zuio la malipo ya gawio kwa wanahisa wake.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bradley Gordon ambaye aliwasili jana ili kutembelea miradi hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wake, alisema Acacia bado haijaanza kutengeneza faida za kulipa kodi ya Mapato ya Kampuni kwa kuwa bado haijarudisha mtaji wake wa awali.

“Pamoja na kwamba tunatengeneza faida kwa jumla, hiyo haitozwi kodi kwa sababu bado hatujarudisha mtaji wa Dola za Marekani 3.8 bilioni. Mkataba wetu na Serikali ya Tanzania unaonyesha kuwa tutatakiwa kuanza kufanya hivyo kuanzia mwaka 2018,” inasomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na Gordon.

Makamu wa Rais wa Acacia, Deo Mwanyika alisema kuwa kampuni hiyo inaanza kulipa kodi ya mapato mwaka huu baada ya kurejesha mtaji wake iliyowekeza kupitia kampuni yake ya North Mara. “Tumerudisha mtaji wetu na makadirio yanaonyesha tunaweza kulipa kodi ya Dola 20 milioni za Marekani (zaidi ya Sh40 bilioni). Nusu ya kiasi hicho tayari kimeshapelekwa TRA,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
daaah tanzania tunadanganywa sana
yaan et uwekezaji wa dola 3.8bilion
. huo uwekezaji ni mkubwa sana kiasai kwamba impact yake kwa jamii
lazima ionekane juzi haba tumepambana na kenye walau boma la mafuta kutoka uganda -tanga lipitie huku kwetu nadhani litagharim dolar 4B . sasa hao acacia hizo 3.8b usd zimejenga nini kwenye hio migodi
watu waache kudanganya watu
 
Hivi hili la ukwepaji kodi hawakukanusha??
 
Zitto kabla ya sakata la makinikia Serikali ilikuwa haina maarifa?
 
Mpaka leo NOAH gari za wa TZ bado mnaleta mpya tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom