ACACIA haikusajiliwa kimkakati ili kukwepa wajibu wowote kisheria iwapo itadaiwa chochote

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,404
2,000
ACACIA imeundwa kimkakati ili ikitokea chochote haswa kesi za ukwepaji kodi au utoroshwaji wa maliasili iwe ngumu kuiwajibisha kisheria. Ni dhahiri kuna watu ndani ya Tanzania wamevuta pesa ndefu ili kampuni hii ifanye kazi kimtegomtego.

Naam, tumeyagundua haya baada ya Raisi Magufuli kuamuru ukaguzi wa shughuli zake n madhara yake kiuchumi na kisheria.

Inaikitisha sana kwani ni ngumu kumdai huyu 'mtu' anayeitwa ACACIA kwa hasara atakayosababisha.
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,210
2,000
Mkuu umeandika kitu cha maana ambacho kinahitaji tafakuli lisilo na papara.
Kuna uwezekano wengi wanaoitwa wafanyakazi wa acacia au mali za acacia wasiwe acacia...
Tutaanza kujifunza mengi vizuri baada ya siku kama nne hivi watu wakiacha kujadili kwa hasira...
 

MANTONGA

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
527
250
Kutoandikishwa BRELA ni mkakati wa makusudi kwa nia lengo lilowekwa wazi na Kamati jana.Ifikie mahala wasomi wetu wawonee huruma Watanzania.Pamoja na Sifa ya kisomi (phd na Masters).Mh.Raisi sifa ya uadilifu/Uzalendo iwe Kigezo cha mtu kupewa kitengo .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom