Aboubakar: Tunataraji ‘Backbanchers’ watatoa changamoto kwa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aboubakar: Tunataraji ‘Backbanchers’ watatoa changamoto kwa Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Mar 5, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
  Joyce Mmasi
  MWAFAKA wa vyama viwili vya siasa vya CCM na CUF huko Zanzibar ulioiwezesha nchi hiyo kubadili katiba na kuruhusu kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa umeleta sura mpya katika visiwa hivyo ambapo hali ni shwari na wananchi wa huko wanafanya shughuli zao bila hofu wala uhasama kama ilivyokuwepo kabla ya muafaka huo.
  Muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa, umetoa fursa kwa CUF kushirikiana na CCM kuunda serikali ambapo kama ilivyo serikali yoyote hii pia inafanya kazi ya kuwatumikia wananchi.
  Nilipopata fursa ya kuzungumza na mmoja wa mawaziri wanaotoka katika chama cha wananchi nilitaka kujua endapo ushirikiano huo utasaidia kukiimarisha chama hicho zaidi na kuwapa urahisi wa kujijenga zaidi ili kuweza kunyakua serikali katika uchaguzi ujao?
  Aboubakar Khamis Bakari, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba katika serikali mpya ya umoja wa kitaifa anasema ni kweli kila chama cha siasa kina lengo na makusudi ya kushika dola na kwamba kwa kuwa CUF bado hajafanikiwa kukamata dola bado malengo na mikakati yao ni katika kufanikisha hilo.
  Aboubakar anayetoka Chama Cha Wananchi (CUF) anasema licha ya malengo yao kuwa ni kushika dola, lakini uwepo wao ndani ya serikali hauwezi kuwa sehemu ya kampeni na badala yake kila aliyepata fursa ya uongozi ndani ya serikali mpya anahakikisha anawatumikia wananchi kwa nafasi yake.
  “Tunafanya kazi ‘as a team work’ hatusukumwi na itikadi, tunasukumwa na matatizo yetu Wazanzibari na jinsi ya kuyatatua, tunaunganisha mawazo yetu, malengo ni kuja na uamuzi wa pamoja wenye lengo la kuwakomboa wananchi na kuleta maendeleo ya Zanzibar,” anasema Aboubakar.
  Aboubakar anasema mawaziri waliopata fursa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa wanafanya kazi kwa maslahi ya Zanzibar na kwamba hakuna anayewaza au kufikiria maslahi ya vyama vyao.
  Anasema mawaziri wa vyama vya CCM na CUF wanapokuwa kazini ni vigumu kuwatambua kwa itikadi za vyama vyao kwa kuwa wamekubaliana kwa pamoja wajibu wao ni kuibadili Zanzibar na kuwaletea maisha mema Wazanzibari.
  Alipotakiwa kueleza changamoto wanazokutana nazo endapo kutakuwa na kutokuelewana katika jambo litakalowashirikisha mawaziri wote, Aboubakar anasema;
  “Tunakwenda vizuri sana katika serikali na katika vikao vyetu vya baraza la mawaziri tumekubaliana hatuamui jambo kwa kura tunafikia mwafaka wa jambo lolote kwa kueleweshana na kila upande kuridhika, hatutaki kura maana katika kura akitokea hata mmoja akasema no hilo tunaliona kama doa, tunataka tumridhishe na yule mmoja kisha wote tukubaliane ndipo utekelezaji ufanyike”.
  Anasema mpaka sasa hakuna mahali waliposhindwa kuelewana na kila upande unazingatia kuleta mabadiliko yatakayoijenga Zanzibar na sio yatakayovijenga vyama vyao.
  Je katika Ushirikiano huo, ni ilani ya Chama kipi inayotekelezwa, Aboubakar anasema; “kama nilivyokwambia, suala la vyama ndani ya serikali halipo, lakini suala la utekelezaji wa Ilani tulikubaliana kuwa chama kitakachoshinda nafasi ya Urais ndicho ambacho ilani yake itatekelezwa, lakini katika issue ya Ilani, ni kwamba zote ziwe za CUF au CCM zina lengo moja, na hata hivyo utekelezaji wa kila jambo tunaamua katika vikao vya baraza la mapinduzi” anasema na kuongeza kuwa kikibwa wanachozingatia ni nchi kwanza na vyama vya siasa vinafuata.
  Hata hivyo anasema suala la utekelezaji wa Ilani ya CCM haiwezi kuwakosanisha na wafuasi wa chama chao kutokana na kuwa kinachotekelezwa ni matatizo ya Wazanzibari na sio matatizo ya wafuasi wa vyama hivyo viwili.
  Je, kwa muundo huo wa serikali ulioondoa upinzani katika baraza, hauwezi kuwafanya wao kama serikali kulala usingizi baada ya kukosa changamoto za kupingwa, kuhojiwa na hata kusukumwa wanapoonekana kulegalega? Aboubakar anasema“Sisi tumewaambia wawakilishi wetu ambao hawakupata fursa ya kuwa katika baraza la mawaziri kuwa wajibu wao ni kuihoji serikali katika kila jambo bila kujali unamuhoji waziri kutoka chama kipi” anasema na kuongeza.
  “Tunataka wawakilishi wawe huru kuhoji, kukemea, kushauri na kuonya pale wanapoona inafaa, sasa tunatarajia upinzani mkubwa zaidi kutoka kwa ‘backbanchers’ (wawakilishi wa pande zote wasiokuwa mawaziri) kuliko hata ule uliokuwa ukitoka katika vyama vya upinzani kabla ya muafaka na kabla ya kuundwa kwa serikali hii ya umoja wa kitaifa.”
  Anasema upinzani anaousema unatokana na hali ilivyo sasa ambapo wawakilishi wanakuwa huru kusema lolote bila kujali itikadi za vyama vyao. “Ukipata ‘backbenchers’ wazuri wenye moyo, watahoji, wataibua mambo mapya, naamini baraza lililopo ni zuri na kutakuwa na hali ya kutikiswa katika utendaji mambo yakionekana kwenda sivyo na hii itasaidia mawaziri kuwa macho na wanaochapa kazi”.
  Anazungumziaje hoja na mitazamo inayotolewa na mahasimu wao kuwa CUF imeungana na CCM na kwamba imepoteza sifa ya kuwa chama cha upinzani Aboubakar anasema, kilichofanyika Zanzibar ni ushirikiano wa vyama viwili kuunda serikali yaani serikali ya umoja wa Kitaifa.
  Anasema ushirikiano huo unatambulika kisheria na kamwe sio makubaliano ya vyama kuungana na kuongeza kuwa ni vyema kwa wanaobeza serikali ya Zanzibar kutafakari mema yanayotokana na serikali hiyo badala ya kutoa shutuma.
  Anasema Wazanzibari wamenufaika zaidi na muafaka uliozaa serikali ya umoja wa kitaifa na wenyewe wanapongeza na kujuta kushindwa kufikia hali hiyo mapema.
  Aboubakar anasema viongozi wa serikali ya Zanzibar kwa umoja wao wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha wanawapa kile walichokiahidi kwa wananchi na kuyaainisha mambo makubwa wanayoyakabili ni suala la utawala bora ambapo anasema mambo yote yatakwenda sawa endapo utawala uliopo utakuwa bora na unaowajali wananchi wake.
  “Tunafahamu umoja ni nguvu, na sasa tunazungumza lugha moja, tunataka wananchi waone matunda ya umoja wetu. Maendeleo yaonekane, watu wakienda hospitali wapate huduma bora, matatizo yaliyokuwepo tushirikiane kuyamaliza na kila palipokuwa na kasoro tuboreshe, hii ndiyo mikakati ya serikali mpya ya umoja wa kitaifa” anasema.
  Anasema katika yote hakuna chama kinachoweza kujigamba kufaidika na mwafaka na badala yake waliofaidika ni wananchi Wazanzibari walioshiriki kupiga kura na kufanya mabadiliko ya katiba yaliyozaa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa.
   
 2. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mswahili mpe cheo atasema hata ambayo hayapo,cuf wameshasahau madhila yaliyowapata wafuasi wao....nonsense
   
 3. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kaaaz kwey kwey.

  Changamoto iliyopo kwa CUF huko Znz ni kuhakikisha kuwa bado inajitofautisha na CCM. Hii ni kama bado inataka kushinda chaguzi zijazo. Hii itakuwa ngumu, labda wabadilike, kwani kwenye Bunge la Muungano wameonyesha ushirikiano mzuri sana na CCM. Ikionekana kuwa sasa hawana kitu mbadala itakuwa issue...
   
Loading...