Abiria wote ndani ya basi walicheka !!!!

Abiria wote ndani ya basi walicheka !!!!

Qualifier

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
1,252
Reaction score
407
Habari za mchana wa jf. Ni kisa kilicho tokea hivi karibuni pale Nyololo kule Mufindi. Nilikuwa nasafiri kwa basi kutoka Mbeya kuelekea Dar, tulipofika nyololo basi lilisimama, kama kawaida ya wachuuzi wa biashara ndogondogo walikimbilia basi na kujaa madirishani huku wengine wakigonga madirisha kuwaashiria abiria wafungue madirisha yaliyo fungwa. Dirisha lililo kuwa mbele yangu alikaa abiria ambaye inaonekana alikuwa anahoma, mgonjwa huyo alipojisikia kutapika akafungua dirisha haraka wale wachuuzi wakakimbilia na kuelekeza biashara zao kwa kugombania mmoja wao aliyebeba sinia la samaki waliokaangwa akawazidi nguvu wenzie na kulielekeza sinia la samaki karibu sana na kichwa cha mgonjwa ambaye sasa alikuwa tayari anatapika na matapishi kujaa kwenye sinia lenye samaki. Ni kisa cha kusikitisha sana kwa sababu mwenzetu alikuwa anahoma na bado yule mchuuzi akaharibiwa biashara yake ambayo ninaamini mqlengo yake kwa siku hiyo yaliharibika. Pamoja na abiria kucheka lakini hizi ni changamoto zinazo wakumba wachuuzi kwenye vituo vya mabasi .
 
Bila kutegemea nini kitakutokea !! Kudra ina shinda jitahada....!
 
Ni stori yenye mafundisho kwa pande zote mbili lakini pia hata kwa wenye mabasi. nakumbuka scandinavia enzi hizo alikuwa anatoa mifuko ya rambo kwa wasafiri hususan wale ambao huwa wanatapika wawapo safarini hivyo hii stori inawafundisha na wenye mabasi kuwa na utaratibu huo halikadhalika na sisi wasifiri ni vema ukawa na akiba yako ya mfuko wa rambo kujiandaa kwa maaafa kama hayo
 
kuna baadhi ya mabasi hua yanagawa mifuko ya plastiki ya kutapikia kila mwanzo wa safari kwa kila abiria. lkn kwa ushamba wa waTZ hii mifuko wanaona ni zawadi. Scandinavia walikua na hii hudma na Bembea pamoja na Shambalai la Lushoto
 
Dah!!!! So sad!

Vp jamaa haku-mind lakini?

Nadhani palichimbika aisee
 
Mabasi yanayokwenda Songea pia nimeona yana utaratibu wa kugawa mifuko kwa abiria wake kwa ajili ya wale wenye shida ya kutapika wawapo safarini.
 
Back
Top Bottom