zeus
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 213
- 55
Kuna jambo moja linanishangaza na kuudhi. katika barabara nyingi ziendazo mikoani- up country- kuna vituo vya mizani kupima uzito wa magari -mabasi ya abiria na magari ya mizigo. sasa utakuwa wenye mabasi ya abiria yaendayo mikoani wanajaza abiria kupita kiasi halafu wakifika karibu na mizani wanashushwa watu waliokaa viti vya nyuma ili kuhadaa watu wa Measurement. Abiria hao wataambiwa watangulie mbele kwa miguu au watatafutiwa kausafiri fulani wakutwe kule mbele. gari inapita kwenye mizani na wataenda kupakiwa huko mbele. Huu ni upumbavu kiasi gani? hivi hii si kuhatarisha maisha yako mwenyewe na kwa faida ya nani?. kwa nini wasikatae halafu mwenye gari awe penalised ili asirudie?. Ajali ikitokea kwa sababu ya overloading nani alaumiwe? sijui abiria hawa wakoje.