Kuna dogo mmoja alikuwa ametoka kwa bibi yake dar anarudi kwao mbeya. Walipofika mto ruvu akamuuliza konda tumefika mikubi konda akasema bado. Walipofika chalinze akauliza tena tumefika mikumi konda akasema bado. Safari ikaendelea walipofika morogoro gari liliposimama dogo akauliza tena tumefika mikumi konda akasema bado. Walipofika mikumi mbugani dogo akalala usingizi, akazinduka wakiwa wamepita mikumi mjini kama km 20 hivi. Akauliza kwa konda tumefika mikumi konda akasema ayaaa tumepita, dogo akaanza kulia. Kwa kuwa ilikuwa jioni konda akamshauri dereva wamrudishe mikumi. Wakageuza gari walipofika mikumi konda akamwambia dogo haya mikumi ndiyo hapa, dogo akasema eheeee bibi alisema tukifika mikumi nile mkate, abiria ahhhhhhhhhhhhhh.