Abiria 20 wanusurika kifo

Abiria 20 wanusurika kifo

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
ZAIDI ya abiria 20 wamenusurika kifo kutokana na basi walilokuwa wakisafiria kuteketea kabisa chanzo kikiwa ni hitilafu katika mfumo wa injini.
Ajali hiyo ilitokea saa saba mchana jana ambapo basi hilo lenye namba za usajili T 717 AWK mali ya Ayubu Kabigi, lilikuwa likitokea maeneo ya Mwangata.
Shuhuda wa ajali hiyo, Anthony Zamilinga, alisema kuwa basi hilo ambalo hufanya safari zake kati ya Mkwawa na Kihesa Kilolo, lilipofika sehemu ya tukio alimwona dereva akishuka na kuanza kuchukua mchanga kwa lengo la kujaribu kuzima moto huo.
Alisema kuwa hali ilipokuwa mbaya, baadhi ya abiria walianza kuruka katika gari hilo na kupiga simu katika kikosi cha zimamoto, ambao walifika haraka eneo hilo kuzima kuzima moto huo huku basi hilo likiwa tayari limeteketea lote.
Msemaji wa Zimamoto, Sajenti Meja John Zakaria, alisema chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika magari yao.
Mmiliki wa basi hilo, Kabigi, alisema kuwa amepata hasara ya sh milioni nane kutokana na ajali hiyo na kuwashukuru wananchi waliojitokeza kusaidia kuzima moto huo.


h.sep3.gif


juu ​

[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Denis Mlowe, Iringa


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]
source.tanzania daima
 
Back
Top Bottom