Justine_Dannie
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 1,963
- 1,617
ABEID KARUME: Aliuawa kulipiza kisasi au kumpindua?
Joseph Mihangwa
Toleo la 126
24 Mar 2010
APRILI 7, mwaka huu, Watanzania katika ujumla wao (angalia: kuna Watanzania na Wazanzibari) wataadhimisha kumbukumbu ya miaka 38 ya kifo cha mwasisi wa Taifa la Zanzibar, na pia mmoja wa waasisi wa Muungano wa Tanzania, hayati Abeid Amani Karume aliyefariki kwa kupigwa risasi na wanajeshi Aprili 7, 1972 mjini Unguja.
Bado kuna utata unaozunguka mazingira, sababu na namna alivyouawa kiongozi huyo, mwana mpendwa wa Tanzania na Afrika; ambaye, kwa kushirikiana na wanamapinduzi wengine Visiwani, aliwezesha kung’olewa kwa utawala wa Kisultani Visiwani katika mapinduzi ya umwagaji damu, Januari 12, 1964.
Wapo wanaoona kwamba Karume aliuawa na kikundi cha wauaji kwa lengo la kulipiza kisasi kutokana na chuki au uhasama wa kale, lakini pia kuna wanaoamini kwamba kiongozi huyo aliuawa katika jaribio la kijeshi lililoshindwa dhidi ya Serikali yake.
Lakini, kwa lolote liwalo kati ya dhana hizo mbili, bado hayati Abeid Amani Karume ni shujaa wa harakati za ukombozi wa Zanzibar, Tanzania na Afrika.
Katika mfululizo wa makala mbili, nitaelezea tukio zima la kifo cha shujaa huyu ili nawe msomaji wangu uweze kuona na kuamua kama mauaji hayo ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa chuki binafsi au lilikuwa ni jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililoshindwa.
Siku hiyo, kama ilivyokuwa kawaida yake, Karume na viongozi wenzake wa Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) walikuwa wakicheza bao makao makuu ya chama hicho, eneo la Kisiwandui, alipopigwa risasi na kuuawa papo hapo, peke yake. Wenzake wote, akiwemo Katibu Mkuu wa ASP, Thabit Kombo walisalimika japo kwa kujeruhiwa hapa na pale.
Jumla ya risasi nane zilitolewa mwilini mwa Karume alipofikishwa katika Hospitali ya V.I. Lenin kwa ajili ya uchunguzi; ikiwa ni idadi sawa na miaka minane aliyoitawala Zanzibar hadi siku hiyo mauti yalipomfika!
Bila shaka Luteni wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Hamud Mohamed Hamud ambaye moja ya risasi za bunduki yake ndiyo iliyomaliza uhai wa Mzee Karume, alikuwa na sababu zake binafsi kuchukua hatua aliyochukua; ingawa hakuwa peke yake wakati wa mauaji hayo.
Washiriki wengine walikuwa ni askari mwingine wa JWTZ, Kapteni Ahmada Mohamed, koplo mmoja ambaye jina halikutajwa na raia mmoja aliyejulikana kwa jina la Ali Khatibu Chwaya, ambao kwa mujibu wa taarifa za kiulinzi na usalama, waliuawa na walinzi wa Rais kwenye eneo la tukio wakijaribu kutoroka baada ya mauaji.
Hapa ndipo ile dhana ya mauaji hayo kuhusishwa na sababu ya chuki binafsi ilipojikita na kutulia dhidi ya ile ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi; na kupewa nguvu na ukweli kwamba, katika mauaji hayo kulikuwa na mshiriki raia mmoja (Ali Chwaya). Kwa kawaida, operesheni za mapinduzi ya kijeshi hazihusishi raia.
Kuna taarifa nyingine zaidi ya tatu zinazokinzana juu ya jinsi wauaji hao walivyotekeleza mauaji na namna walivyouawa. Moja inadai kwamba, Hamud pekee ndiye aliyeuawa papo hapo na mlinzi wa Karume ambapo wenzake watatu, Kapteni Ahmada, Koplo wa Jeshi ambaye jina lake halikutajwa pamoja na Ali Chwaya, waliuawa katika mapambano ya silaha ya kujibizana na vyombo vya ulinzi nje ya eneo la tukio.
Dhana ya tatu, ambayo kwa mujibu wa William Edgett Smith katika Kitabu chake: “Mwalimu Julius K. Nyerere” (Uk. 156), anadai kwamba, Hamud aliuawa kwenye eneo la tukio ambapo wenzake wawili waliuawa baadaye na vyombo vya usalama na mmoja alijiua mwenyewe.
Lakini kwa mujibu wa jarida moja la kiharakati liitwalo “HABUSU” la Agosti 1976, lililokuwa likitolewa na “The Zanzibar Trial Trust Fund”, ni kwamba Hamud alikufa ama kwa kujipiga risasi kuepuka kukamatwa hai na kuteswa, baada ya kubaini kwamba asingeweza kutoroka; au alijeruhiwa vibaya na walinzi wa Karume na kisha Kapteni Ahmada akampiga risasi na kumuua kumwepusha asiteswe, na hata kutoa siri kama angekamatwa; kisha Ahmada mwenyewe akaweza kutoroka kwenye eneo la tukio.
Pamoja na taarifa zote hizi za kukanganya na zinazokinzana, iwe isiwe, kwamba mauaji hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa sababu ya chuki binafsi; inawezekana kabisa kwamba Mzee Karume, pengine bila ya yeye kuelewa, alijiandalia mwenyewe mazingira yaliyosababisha kifo chake.
Baada ya Mapinduzi ya umwagaji damu ya Januari 12, 1964, Serikali ya Karume na Karume mwenyewe, aliendesha utawala wa kimabavu kiasi cha kutotaka ushauri wala kukosolewa juu ya jinsi na namna ya kuyalinda mapinduzi yaliyopatikana Visiwani.
Akitawala kwa njia ya Amri za Rais (decrees), na kwa kuwa Zanzibar hapakuwa na Sheria, Karume alitangaza utawala wa Chama kimoja (ASP) na akaagiza watu wote wazima kujiunga kwa lazima na chama hicho.
Picha ya Karume ilikuwa lazima itundikwe kwenye kila nyumba. Kikosi chake cha usalama kilichofunzwa na Wajerumani Mashariki, kikiongozwa na Kanali Seif Bakari, kilipewa uwezo na mamlaka ya kukamata, kutesa, kufunga bila mashitaka, na hata kuua yeyote aliyeonekana kumpinga Karume au kuhoji utekelezaji wa Mapinduzi.
Yeyote aliyelalamika, hata kwa jambo dogo tu kama la upungufu wa chakula na bidhaa Visiwani, alichukuliwa kama “Adui wa Mapinduzi”, na adhabu ilikuwa kubwa ikiwamo kuuawa.
Karume pia alianzisha mfumo wa sheria wa ajabu kwa kufuta mahakama za kawaida na nafasi yake kuchukuliwa na Mahakama mpya, kwa jina la “Mahakama za Wananchi” zilizoongozwa na kusimamiwa na baadhi ya watu wasiojua kusoma wala kuandika (kwa mfumo wa elimu ya Kimagharibi), na wasio na elimu wala ujuzi wa sheria.
“Mahakamani”, wakati wa kesi, upande wa mashitaka uliweza kujigeuza kuwa upande wa utetezi pia na kuwatetea watuhumiwa inapofika zamu ya utetezi.
Kwa sababu hii, mawakili walipigwa marufuku Visiwani kwa madai kwamba ni “wabishi na wenye kuteteresha mkondo wa sheria”. Magereza yalipewa jina jipya la “Vyuo vya Mafunzo”, ingawa wafungwa wengi; hasa wale wa kisiasa, waliteswa na hata kuuawa kwa njia za kikatili.
Haki za binadamu hazikuheshimiwa. Na unyanyasaji, kwa misingi ya ubaguzi wa rangi na kijinsia, ulitia fora.
William Smith katika kitabu chake “Mwalimu Julius K. Nyerere” (UK. 152), anaelezea moja ya matukio kama hayo ambapo mwaka 1966, Karume alitangaza amri(decree) iliyowanyima wazazi na binti zao haki ya kuwakataa wanaume walioposa binti zao kama njia ya kuondoa ubaguzi wa rangi.
Chini ya amri hii, wasichana, hasa wale wa Kiarabu na Kiajemi, walilazimishwa kuolewa kwa nguvu. Karume mwenyewe, akiwa na umri wa miaka 65, aliamua kuoa wanne kati ya wasichana hao wengi, na alipokataliwa, aliamuru wazazi wao na jamaa 10 wa wazazi hao kutiwa kizuizini kwa kosa la “kuzuia utekelezaji wa ndoa mchanganyiko”, na kutishia kuwafukuza nchini Waajemi wote na wafuasi wa kikundi cha “Ithnasheri”.
Raia wa kigeni waliochumbia mabinti wa Kizanzibari, walilazimishwa kuilipa serikali ushuru wa ndoa wa Sh. 64,000 kwa kila binti; bila hivyo hawakuruhusiwa kuwaoa.
Kwa kuhofu mawazo mapya kuingia Visiwani, Karume alipiga marufuku vijana wa Kizanzibari kwenda nje kwa ajili ya elimu ya juu, ikiwa ni pamoja na kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; wala kujengwa Chuo Kikuu Zanzibar.
Karume, bila ya kutarajiwa, alifuta na kufunga ghafla mpango na Kituo cha Utafiti na Udhibiti wa Malaria, chini ya usimamizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Visiwani, kwa madai kwamba Waafrika ni “malaria proof” (hawaugui malaria), na kwamba mpango huo ulikuwa ni aina fulani ya “ukoloni-mamboleo”.
Kwa mujibu wa Gazeti la Serikali (The Standard) la Machi 9, 1968, Karume aliapa kuwa, chini ya utawala wake, pasingekuwa na uchaguzi Visiwani kwa miaka 50 tangu 1964.
Alidai kwamba “uchaguzi ni chombo cha mabeberu cha kuwakandamiza wananchi”. Ndiyo kusema kwamba, kama Karume angeendelea kutawala, uchaguzi wa kwanza Visiwani ungefanyika mwaka 2014!
Kwa upande wa Muungano, uhusiano kati yake na Mwasisi mwenzake, Mwalimu Julius K. Nyerere nao ulikuwa umeanza kuingia dosari. Kwa mfano, Karume alikataa kwa lugha ya kuchukiza kutumika kwa Siasa ya “Ujamaa na Kujitegema” Visiwani.
Wakati fulani alipiga marufuku nyimbo zenye kuikosoa na kuilaani Marekani kwa vita yake nchini Vietnam wakati Nyerere na Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kulaani vita hiyo!
Wakati Nyerere akihuzunika juu ya kupinduliwa kwa Serikali ya Rais Milton Obote nchini Uganda na dikteta Idi Amin, Karume hakuona ubaya kwa hilo, na kumwita Amin ‘rafiki na mwanamapinduzi wa kweli wa Afrika’.
William Smith katika “Mwalimu Julius K. Nyerere”, anaeleza kwamba, Karume hakutilia maanani tena suala la Muungano kiasi cha kutoshaurika, na mara nyingi akiudhika alimwambia Nyerere: “Kama ni hivyo, bora tuvunje Muungano”.
Ni kufikia hali hiyo Karume aliweza kutoa tamko lake maarufu hadi sasa kwamba: “Muungano ni kama koti, likikubana unalivua”.
Na katika hali iliyoonekana ni ya kukata tamaa, Nyerere amenukuliwa na William Smith (Uk. 154) akisema: “Kama watu wa Zanzibar wanaona hivyo …. mimi siwezi hata kidogo kuwaua wananchi wa Zanzibar. Kama waliingia katika Muungano kwa hiari yao, wanaweza pia kujitenga kwa hiari yao. Hatukuishinda Zanzibar vitani”.
Ingawa suala la fedha ni la Muungano, Karume hakuruhusu hata kidogo akiba yake, iliyoongezeka kutoka dola milioni 3 kabla ya Mapinduzi, kufikia dola milioni 80 mwaka 1972 kutokana na bei nzuri ya karafuu, iguswe na Serikali ya Muungano.
Aliitumia kwa manufaa ya Wazanzibari pekee ikiwa ni pamoja na kununua mtandao wa Televisheni ya rangi wa aina yake barani Afrika wakati huo; huku baa la njaa na ukosefu wa bidhaa muhimu kwa maisha, ukivitafuna Visiwa hivyo.
Pengine kudhoofika kwa mahusiano ya waasisi hawa wawili wa Muungano wa Tanzania, ndiyo iliyokuwa sababu kuu ya kutoteuliwa kwa Tume ya Kupendekeza Katiba ya Muungano na kuitishwa kwa Bunge la Katiba kupitisha mapendekezo hayo kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano.
Matokeo yake ni kwamba, kwa miaka 13 hadi 1977, Muungano uliendeshwa bila Katiba makini na ya kudumu, na kuzaa sehemu kubwa ya kero zinazoukabili Muungano hadi sasa.
Mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Karume alikuwa baba yake Luteni Hamud Mohamed Hamud, mzee Mohamed Hamud.
Mzee Mohamed Hamud alikamatwa miezi michache baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 kwa tuhuma za kutaka kuipindua Serikali mpya ya Karume.Alitiwa kizuizini na hatimaye kuuawa kikatili bila ya kushitakiwa.
Wengine waliomnyima Karume usingizi na kukamatwa na kuuawa kadri siku zilivyokwenda, ni pamoja na baadhi ya viongozi na wanachama wenzake (Karume) wa ASP wenye siasa za mrengo wa Kisoshalisti/Kikomunisti walioshirikiana na Vijana wa Chama cha Umma Party cha Abdulrahman Babu kufanikisha Mapinduzi ya 1964.
Kwa sababu hiyo, baadhi yao, kama tutakavyoona baadaye, walibambikizwa tuhuma za uongo na kuuawa kikatili.
Luteni Hamud Mohamed Hamud alifahamu juu ya kuuawa kwa baba yake miaka michache baadaye akiwa katika mafunzo ya kijeshi huko Tashkent, Urusi ya zamani. Inasemekana alitamka kwa kuapa kwamba, punde atakaporejea Zanzibar, angemuua Karume kulipiza kisasi kifo cha Baba yake.
Kwa kupitia majasusi miongoni mwa marafiki wa Hamud huko masomoni, Serikali ya Karume ilijulishwa juu ya kusudio la Hamud la kumuua Rais Karume, lakini haikuchukua hatua hata baada ya Hamud kurejea Zanzibar. Badala yake, Karume mwenyewe alimpandisha cheo kuwa luteni katika sherehe iliyohudhuriwa na wakuu wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama Zanzibar.
Je, taarifa juu ya “tamko” la Luteni Hamud Mohamed Hamud huko Tashkent juu ya dhamira yake ya kutaka kumuua Karume, zilikuwa za uongo?
- See more at: Raia Mwema - ABEID KARUME: Aliuawa kulipiza kisasi au kumpindua? kuna utata unaozunguka mazingira, sababu na namna alivyouawa kiongozi huyo, mwana mpendwa wa Tanzania na Afrika; ambaye, kwa kushirikiana na wanamapinduzi wengine Visiwani, aliwezesha kung’olewa kwa utawala wa Kisultani Visiwani katika mapinduzi ya umwagaji damu, Januari 12, 1964.

Haki za binadamu hazikuheshimiwa. Na unyanyasaji, kwa misingi ya ubaguzi wa rangi na kijinsia, ulitia fora. William Smith katika kitabu chake “Mwalimu Julius K. Nyerere” (UK. 152), anaelezea moja ya matukio kama hayo ambapo mwaka 1966, Karume alitangaza amri(decree) iliyowanyima wazazi na binti zao haki ya kuwakataa wanaume walioposa binti zao kama njia ya kuondoa ubaguzi wa rangi.

Pengine kudhoofika kwa mahusiano ya waasisi hawa wawili wa Muungano wa Tanzania, ndiyo iliyokuwa sababu kuu ya kutoteuliwa kwa Tume ya Kupendekeza Katiba ya Muungano na kuitishwa kwa Bunge la Katiba kupitisha mapendekezo hayo kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano. Matokeo yake ni kwamba, kwa miaka 13 hadi 1977, Muungano uliendeshwa bila Katiba makini na ya kudumu, na kuzaa sehemu kubwa ya kero zinazoukabili Muungano hadi sasa.