Habari Isanga.
Nipo Pretoria kwa masomo, natarajia kumaliza next year December.
Nimekua niki-save allowance/stipend nazopata kutoka kwa sponsor wangu, na natarajia mpaka namaliza nitakua nina savings around $7,000 (Rands 130, 000) hivi.
Sasa nikimaliza masomo savings zangu nitazibebaje, namaanisha ipi njia nzuri ya kuhamisha pesa zangu kutoka Standard Bank (S.A) kwenda Tanzania (kule natumia CRDB lakini naogopa rates zao wakuda wale).
- Unanishauri njia gani ni salama, haina complications (wasije wakazi block savings zangu), makato madogo na muhim zaidi exchange rates nzuri?
nimeona watu wanasema Sendwave, Wire Transfer, kufungua account mpya ya dollar bongo, kutumia VISA card yangu ya Standard Bank na kwenda kuwithdrawal mdogo mdogo kwa ATM za bongo?
lengo la kufanya hizi savings ni kukusanya pesa ya kununua gari ndogo nikimaliza masomo.
Naomba unishauri kaka. Najua wewe mzoefu.