Abdi Banda wa Simba amesimamishwa

Apr 8, 2017
18
12
Abdi Banda wa Simba amesimamishwa - WILLYD HABARI
Screen-Shot-2017-04-09-at-6.46.44-PM.png

Beki wa kati wa wekundu Msimbazi Simba leo Jumapili ya April 9 2017 taarifa zilizotolewa kutoka katika kamati ya saa 72 ni kuwa amesimamishwa kuendelea kucheza mechi za VPL na kamti hiyo hadi tuhuma zake za kumpiga ngumi George Kavilla zitakapotolewa maamuzi na kamati ya nidhamu ya TFF.

Abdi Banda anatuhumiwa kumpiga ngumi George Kavilla wa Kagera Sugar wakati wa mchezo dhidi yao akiwa hana mpira mchezaji huyo, hivyo kamati imeamua imsimamishe hadi itakapotoa maamuzi rasmi, tukio la Banda ambalo halikuonwa na refa inadaiwa aliwahi lifanya pia katika game dhidi ya Yanga.

Katika mchezo huo ambao ulichezwa April 2 2017 katika uwanja wa Kaitaba Bukoba, Simba ambayo ilikuwa inaongoza Ligi kwa tofauti ya point moja dhidi ya watani zao Yanga, ilichezea kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar.

VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera April 2 2017
 
Banda anatakiwa kujifunza the hard way ili aache tabia za kihuni kihuni. Jamaa anajua sana mpira, ni hazina ya Taifa ila tabia zake sio ni kama kiana Yondani

Lkn hii kamati nayo inaleta uswahili, haipaswi kumsimamisha, anapaswa kupewa adhabu ama kuachiwa kama hana makosa. Kumsimamisha kabla ya kumtia hatiani ni kumwadhibu tayari.
 
Banda anatakiwa kujifunza the hard way ili aache tabia za kihuni kihuni. Jamaa ananua sana mpira, ni hazina ya Taifa ila tabia zake sio ni kama kiana Yondani

Lkn hii kamati nayo inaleta uswahili, haipaswi kumsimamisha, anapaswa kupewa adhabu ama kuachiwa kama hana makosa. Kumsimamisha kabla ya kumtia hatiani ni kumwadhibu tayari.
Ndio mara ya kwanza naona hii kitu. Unamsimamisha kupisha uchunguzi? MADE IN TANZANIA.
 
Banda anatakiwa kujifunza the hard way ili aache tabia za kihuni kihuni. Jamaa anajua sana mpira, ni hazina ya Taifa ila tabia zake sio ni kama kiana Yondani

Lkn hii kamati nayo inaleta uswahili, haipaswi kumsimamisha, anapaswa kupewa adhabu ama kuachiwa kama hana makosa. Kumsimamisha kabla ya kumtia hatiani ni kumwadhibu tayari.
Kabisa Mkuu maana je akija kuonekana Hana hatia itakuaje?
 
Kamati za kipumbavu sana, ningekuwa Karibu yao ningepiga mtu ngumi pia, kumsimamisha ni kumuadhibu tayari, halafu hv adhabu ni lazima mchezaji asicheze? ?????? Badilikeni nyie watu na mawazo mgando miaka nenda rudi hamtumii akili zenu ndogo hata kidogo, Ingekuwa mimi Banda angeendelea kucheza hadi hapo TFF watakapo toa msimamo, na TFF kama Banda anahatia alipe fine tu ya Mil moja, na kuendelea na kazi.
 
Ni kweli hata ile mechi ya Kagera sugar Simba imechapwa uwanjani, kama kuna dosari timu ipigwe faini ya pesa na matokeo yabaki kama yalivyo.

Ulaya hakuna point za mezani.
 
Ni kweli hata ile mechi ya Kagera sugar Simba imechapwa uwanjani, kama kuna dosari timu ipigwe faini ya pesa na matokeo yabaki kama yalivyo.

Ulaya hakuna point za mezani.
Watu hawataki kujifunza, wanabakiza mambo tata maksudi ili mradi tu matumbo yao yajae vyakula, hovyo sana
 
Tunapomzungumzia Banda hatuzungumzi kwa faida ya simba.Banda ni beki bora kwa sasa Nchini,tunaona mchango wake stars.Hii kumweka bechi bila hukumu ni kuua kipaji chake.Banda anapaswa kulipa faini na mpira ukaendelea.Huu uyanga na usimba ni uchawi wa soka letu.Kila mtu anavuta kwake,tunatakiwa tutazame mbele zaidi ya faida kwa simba.
 
Hapana kiongozi sikubaliani na utaratibu wa kubadilisha kanuni kwa sababu ya mtu.

Kama kuna kosa limethibitishwa kufanywa na Banda apewe adhabu kulingana na sheria na kanuni inavyosema. Kama ni kufungiwa afungiwe, kama ni faini apigwe faini, kama ni onyo kali apewe. Kifupi kanuni ifuatwe kama ambavyo kuchezesha mchezaji mwenye kadi tatu kutakavyoiponza Kagera Sugar.

Ubovu wa TFF an kamati zake ni kujichulia maamuzi ya kumsimamisha ambayo ni adhabu tayari. Kinachowafanya wachukue muda mrefu kufanya uamuzi ni nini hasa? Kwa uamuzi huu wameiathiri Simba na Banda mwenyewe kinyume cha kanuni. Ni rahisi kuona hili jambo limeamuliwa kwa hisia na shinikizo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom