Abbass Juma Muhunzi Aendelea kuidindishia CUF.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema licha ya Mwakilishi wake Abass Juma Muhunzi kukaidi amri ya uongozi wa chama hicho kutokwenda Dodoma kushiriki katika michezo na timu ya bunge chama hicho hakitomuadhibu kamwe.
Hayo yalisemwa na Mnadhimu wa baraza la wawakilishi kambi ya upinzani Haji Faki Shaali wakati alipoulizwa kuhusu hatua zipi za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya Mwakilishi huyo kwa kukaidi amri ya chama.
‘Hatuna mpango wa kumpa adhabu yoyote ile ingawa ni kweli alikaidi amri ya chama…sisi tuliamuwa kutokwenda Dodoma kushiriki katika michezo na timu ya Wabunge na Wawakilishi lakini yeye alipinga uamuzi huo hivyo ni uamuzi wake kushiriki hakutaka kutusikiliza sisi hatuna lolote la kumfanya katika uamuzi wake”alisema Shaali.
Shaali alisema huo ni uamuzi wake na alichofanya ni sawa sawa na chama hakitokaa kumjadili na kumpa adhabu kwa kuwa kila mmoja ana maamuzi yake licha ya kuwa anapaswa kusikiliza maamuzi ya chama lakini kama hataki kusikiliza hilo ni juu yake.
Wiki iliyopita timu ya baraza la wawakilishi ilifanya ziara kwenda Dodoma kushiriki michezo mbali mbali na timu ya wabunge katika ziara ya kudumisha uhusiano na mashirikiano mazuri ya kudumisha muungano kati ya tanzania bara na Zanzibar.
Uongozi wa chama cha CUF katika baraza la wawakilishi uliwataka wajumbe wake kutokwenda Dodoma na kushiriki katika michuano hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kuonesha hisia zao na kukerwa na zoezi linaloendelea sasa la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea huko kisiwani Pemba ambapo baadhi ya wananchi kadhaa wamekataliwa kuandikishwa katika daftari hilo
Shaali alisema chama cha CUF hakiridhishwi na zoezi la daftari la kudumu la wapiga kura na uboreshaji wake ikiwemo kuandikishwa wapiga kura wapya kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hata hivyo Mwakilishi wa Chambani Abass Juma Muhunzi alipinga uamuzi huo na yeye kuamuwa kujumuika na wajumbe wa chama cha mapinduzi na kwenda Dodoma kushiriki michuano hiyo
Muhunzi kwa muda mrefu sasa ametofautiana na wajumbe wenzake wa baraza la wawakilishi CUF, baada ya kiongozi wa kambi ya upinzani kumshutumu kwa ubadhirifu wa fedha za baadhi ya wajumbe ambao walimuamini kwa ajili ya kutaka kununuliwa gari.
Mwakilishi huyo amekuwa akija katika baraza la wawakilishi lakini hafiki katika ofisi ya baraza la wawakilishi ya kambi ya upinzani ziliomo ndani ya baraza hilo.
Mwakilishi wa Jimbo la Tumbe (CCM) Ali Mohamed Bakari alisema uamuzi wa kususia safari ya Dodoma umefanywa na chama na hivyo yeye hakuwa na sababu za kupinga.
“Ni uamuzi wa Chama cha wananchi CUF….sikuwa na sababu za kupinga…lakini mimi ningwekwenda Dodoma ningechukuwa medali nyingi zikiwemo za riadha kwa kuwa mimi ni mchezaji mzuri sana katika mchezo huo na ninaupenda sana” ‘alisema Bakari.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wa chama cha mapinduzi walisikitishwa na uamuzi huo na kusema umewakosesha wajumbe wa CUF ushiriki wa mashindano mbali mbali ambayo wamekuwa wakitaka mashindano hayo yawe yanaendelezwa
‘Tumesikitishwa sana kwa sababu katika timu yetu ya Baraza la wawakilishi wapo wanariadha wazuri kutoka CUF kwa hivyo mimi naamini wangetusaidia sana timu yatu kushinda vizuri zaidi” alisema Ramadhan Nyonje Pandu.




SOURCE: ZANZIBAR YETU BLOG.
 
Kesha nunuliwa huyu!

Kanunuliwa, na huenda CCM wakamsimamisha katika jimbo hilo hilo. Uchaguzi wa mwakani naona CCM wanataka tumia kila hila Pemba wapate japo majimbo machache. Nimesoma Mkuu wa Mkoa mmoja wa Pemba akizungumzia uandikishaji wa daftari la wapiga kura kuwa CUF Pemba walikuwa wanatumia hila kushinda. Yani CCM kutumia vikosi vya ulinzi kibao toka Bara, kuzuia baadhi ya watu kujiandikisha, na pia kuiba kura, leo wanasema CUF hushinda kwa hila Pemba. Uchaguzi wa mwakani utakuwa na hila kubwa tokea kwa CCM, na haya yameanza onekana mapema wakati wa kuandikisha wapiga kura.

Huyu Mhunzi kadhulumu fedha za wawakilishi, sasa anabebwa na CCM. Kazi tunayo.
 
Kanunuliwa, na huenda CCM wakamsimamisha katika jimbo hilo hilo. Uchaguzi wa mwakani naona CCM wanataka tumia kila hila Pemba wapate japo majimbo machache. Nimesoma Mkuu wa Mkoa mmoja wa Pemba akizungumzia uandikishaji wa daftari la wapiga kura kuwa CUF Pemba walikuwa wanatumia hila kushinda. Yani CCM kutumia vikosi vya ulinzi kibao toka Bara, kuzuia baadhi ya watu kujiandikisha, na pia kuiba kura, leo wanasema CUF hushinda kwa hila Pemba. Uchaguzi wa mwakani utakuwa na hila kubwa tokea kwa CCM, na haya yameanza onekana mapema wakati wa kuandikisha wapiga kura.

Huyu Mhunzi kadhulumu fedha za wawakilishi, sasa anabebwa na CCM. Kazi tunayo.
Tatizo kaanza kushirikiana na mafisadi naye kawa fisadi.Lakini CCM wakimchukua ni kheri kwa CUF maana jamaa mkaidi ile mbaya!! na wakimsimamisha Pemba ndiyo mwisho wake atarudi kuuza vyuma chakavu. Wakuu wa Mikoa Pemba ni wahuni wanapelekwa kule kundeleza na kuongeza madhila kwa watu. Hebu fikiria siku zile watu wanalalamika upungufu wa chakula Mkuu wa Mkoa anasema "waongo eti hakuna njaa wanajidai tu..." sasa Dadi naye kawa msemaji wa tume ya uchaguzi, maajabu hayeshi dunia hii....!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom