Abarikiwe aliyemleta Rais Samia Duniani

Abarikiwe aliyemleta Rais Samia Duniani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
36,387
Reaction score
23,774
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika libarikiwe sana tumbo lililombeba mama Samia, lilibeba mtoto aliyekuja kuwa kiongozi wa Tanzania, kiongozi mwenye upendo, hekima, busara, ukarimu, huruma, unyenyekevu na usikivu.

Kiongozi asiye na makuu wala makidai, kiongozi mwenye kujishusha na kujua kuwa pamoja na madaraka yake makubwa kiuongozi lakini bado anabaki kuwa mwanadamu aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu.

Kiongozi ambaye pamoja na uwezo wake mkubwa kimamlaka lakini anatambua kuwa yupo Mungu ambaye ndiye anayepaswa kuabudiwa na kupewa sifa na utukufu, kiongozi ambaye wakati wote madaraka yamemfuata yeye kutokana na kupewa kibali na Mwenyezi Mungu.

Kiongozi ambaye mikono yake ameinyoosha katika kuwafuta machozi na kuwapatia haki wenye kuonewa, kiongozi ambaye ulimi wake umewaponya na kuwafariji wenye majeraha na makovu.

Ni kiongozi ambaye hajawahi kufurahi wala kuwa tayari kuongoza taifa la watu wanaolia na kububujikwa machozi kwa kuonewa, hajawahi kuwa tayari kimaneno na hata kimatendo kuhubiri uonevu, ukatili, ubaguzi na hata chuki kwa watu.

Ni kiongozi ambaye ulimi wake muda wote ni wenye kutoa maneno ya upendo mshikamano na kujenga umoja wa taifa.

Ndio sababu ya kuungwa mkono na Watanzania wote, ndio sababu ya kupendwa na kuombewa afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia Watanzania, ndio sababu ya kusikilizwa na kufuatiliwa sana kwa hotuba zake, ndio sababu ya kuteka hisia na mioyo ya Watanzania, ndio sababu ya kukubalika kwake na makundi yote, ndio sababu ya umaarufu na ushawishi wake kuwa mkubwa sana Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.

Rais samia ni nuru katikati ya giza, ni tumaini katikati ya waliokata tamaa, ni faraja kwa waliao, ni mpatanishi wa kweli, mpenda haki na mtenda haki, ni Nyota ya alfajiri iletayo matumaini ya pambazuko lililojema.

Ndio sababu ya kila Mtanzania kuwa na matumiani ya pambazuko katika maisha yao na ndoto zao, kila mmoja anao uhakika wa kutimiza ndoto zake na kufikia mafanikio anayoyataka.

Serikali yake imekuwa kwa ajili ya kuwasaidia watu, kuwawezesha na kuwashika mkono katika kufikia malengo yake. Serikali yake haipo kwa ajili ya kumuonea mtu, kumdhuru mtu, kumtesa mtu, kumliza mtu.

Ni serikali safi ya haki yenye matendo mema na hatua njema, ni serikali yenye dhamira ya kuwatumikia watu kwa upendo na uzalendo mkubwa.

Ndio sababu ya kuona mioyo ya Watanzania ikiwa haina hofu wala wasiwasi, kila mmoja anayo amani moyoni mwake, kila mmoja anayo imani na serikali hii, kila mmoja anaridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya Rais Samia.

Viongozi aina ya Rais Samia hawazaliwi kila siku wala hawapatikani kila mahali, maana wenye moyo kama wake wa kuweza kumsikiliza kila mtu, kumvumilia kila mtu mwenye kutofautiana nao, wenye kifua kama chake, wenye kusikiliza sauti zote hata zikwaluzazo kwa lugha za ukakasi, kukaa mezani na yeyote, kujumuika na yeyote ni wachache sana.

Viongozi aina yake huja kama mitume kwa ajili ya kuwatumikia watu kwa haki na upendo. Huja wakiwa wameandaliwa na Mwenyezi Mungu, hawaandaliwi na wanadamu wala kwa mipango ya wanadamu, huja wakiwa wamepewa maaarifa na njia za kuongaza.

Mwenyezi Mungu huwapa kila kitu kama ilivyokuwa kwa Musa, huja wakiwa na kibali mkononi cha Mwenyezi Mungu katika ulimwengu wa kiroho. Huja kwa makusudi maalumu, huja kama nyota katikati ya giza, hung'aa na mwanga wao huwa tumaini la watu waitazamayo nyota hiyo, huja wakiwa na majibu ya maswali.

Ndio sababu ya kuona Rais Samia akiwa kipenzi cha Watanzania, ndio sababu ukiona Rais Samia hakauki midomoni mwa Watanzania kwa mema. Amejiandikia ukurasa wake na anaendelea kuandika kitabu chake kitakachosimuliwa vizazi na vizazi kwa mema mengi na makubwa aliyolifanyia Taifa letu yanayobaki kama alama katika mioyo ya watu.

Rais Samia kwake haki ndio kipaombele kwa kuwa anatambua ya kuwa haki huinua taifa. Ni heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi na ufahari wa kidunia.

Rais samia amechagua jina jema kwa kutenda mema kwa Watanzania, yanayomfanya kuwa chaguo la Watanzania kwa muhula wa pili, yanayomfanya apendwe na kuzungumzwa vyema na watu wa makundi yote, rika zote, jinsia zote na vyama vyote.

Rais Samia pamoja na madaraka yake makubwa, ukubwa wa kimamlaka alionao mikononi mwake na katika ulimi wake kikatiba na kisheria, lakini bado anatambua ya kuwa yeye ni mwanadamu na kwamba anayestahili kuabudiwa na kupewa sifa na utukufu ni Mwenyezi Mungu pekee na siyo mwanadamu.

Ndio sababu ya kuwa mnyenyekevu muda wote, mwenye kujishusha na kuwasikiliza watu wote pasipo ubaguzi wala kuwagawa kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda, ndio sababu ya kuongoza taifa kwa haki na upendo.

Libarikiwe tumbo lililombeba Rais Samia, maana matumbo mengine yanaleta watu Duniani wanaokuja kuleta mateso kwa watu, uchungu katika maisha ya watu, simanzi kwa watu, machozi kwa watu, maumivu kwa watu, giza katika mioyo ya watu, majeraha na uvuli katika mioyo ya watu, kumwaga damu za watu, kunyonga watu, kuua watu, kukatisha na kuzima ndoto za watu, kushindana na Mwenyezi Mungu anayewapa watu pumzi ya kuishi.

Tujitahidi kutenda mema tukiwa hai kwa kadri tuwezavyo ili matendo yetu yasimame kututetea tukiwa hatuna uwezo wa kujitetea wala kufungua vinywa vyetu. Ya Duniani ni ya kupita tu, yanini kuumizana, kutesana, kukatishana ndoto, kujengeana chuki, kuuwana kwa sababu ya mali au madaraka au vyeo?, nani anazikwa navyo?

Kazi iendelee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Mkuu umeandika vizuri sana na kweli mama yetu ni Rais bora na anauwezo mkubwa sana na anatumia sayansi kubwa sana katika uongizi wake hiki ni kipaji cha kipekee. Tatizi lako ni kuweka number yako ya simu mwisho wa uzi wako na kujiita mzalendo mpenda nchi hapo sijui umekusudia nini.

Sisi tutaaminije kuwa wewe ni mzalendo na mpenda nchi maana hatuna kifaa cha kupima hayo mambo na mpaka sasa umeifanyia nini hii nchi hadi sisi tujue kuwa unaipenda? Ungetueleza kidogo mkuu maana wazalendo wa kweli tunawafahamu kwa matendo na kazi zao za kulilinda na kulijenga hili taifa kwa jasho na damu usiku na mchana, wengine wapo mashambani wakizalisha chakula kuhakikisha taifa haliingii kwenye baa la njaa na sio kuwa mzalendo kwa maneno au kwa kuvaa nguo zenye rangi ya bendera.
 
Mkuu umeandika vizuri sana na kweli mama yetu ni Rais bora na anauwezo mkubwa sana na anatumia sayansi kubwa sana katika uongizi wake hiki ni kipaji cha kipekee. Tatizi lako ni kuweka number yako ya simu mwisho wa uzi wako na kujiita mzalendo mpenda nchi hapo sijui umekusudia nini.

Sisi tutaaminije kuwa wewe ni mzalendo na mpenda nchi maana hatuna kifaa cha kupima hayo mambo na mpaka sasa umeifanyia nini hii nchi hadi sisi tujue kuwa unaipenda? Ungetueleza kidogo mkuu maana wazalendo wa kweli tunawafahamu kwa matendo na kazi zao za kulilinda na kulijenga hili taifa kwa jasho na damu usiku na mchana, wengine wapo mashambani wakizalisha chakula kuhakikisha taifa haliingii kwenye baa la njaa na sio kuwa mzalendo kwa maneno au kwa kuvaa nguo zenye rangi ya bendera.
Nipo shambani naendelea kuzalisha chakula ili kulilisha Taifa letu lisiingie katika baa la njaa maana huwezi ukamuongoza mwenye njaa Wala kusikilizwa na mtu mwenye njaa ya chakula
 
 
Aliyemleta Samia duniani Ni Mungu! Acha kufuru in the first place Nani wa kumbariki Mungu?
Ndugu yangu na rafiki yangu Dolphin T napenda kukuhakikishia kuwa siwezi kukufuru Wala kufanya dhihaka kwa Mwenyezi MUNGU maana huyu hafananishwi na yeyote Wala na chochote ,huyo Ni alfa na Omega, ndio maana hata katika andiko langu nimeandika Hilo juu ya uweza wa MWENYEZI MUNGU
 
Bwashee umemsahau aliyemteua kuwa makamu wake, bila huyo hayo yote uliyoyasema asingeyafanya.
Sifa na Utukufu Tunamrudishia Mwenyezi MUNGU maana uongozi hutoka kwa Mwenyezi MUNGU,yeye ndiye mtengeneza njia ya mtu na mtoa maarifa kwa mtu na watu, akihitaji kukuinua na kukupa kibali Cha uongozi hazuoliwi na watu Wala kusubiri maamuzi ya mwanadamu,maana yeye anatufahamu sisi Tungali katika matumbo ya mama zetu katika uumbaji wetu
 
Chagua upande mmoja kaka wenzio wanamnanga mama samia na kumtukuza marehemu wewe upo upande gani😁
 
Chagua upande mmoja kaka wenzio wanamnanga mama samia na kumtukuza marehemu wewe upo upande gani😁
Rais Samia Ni Kama maji Usipoyanywa utayaoga tu,pia sipo hapa kumnanga mtu Bali kuwasilisha mawazo yangu juu ya Rais Samia na uchapa kazi wake uliotukuka na ulioteka mioyo ya watanzania ambayo imeridhishwa na utendaji kazi wake
 
Back
Top Bottom