Aaaaahhhh! Kumbe mapenzi yana rangi nyingi.

Aaaaahhhh! Kumbe mapenzi yana rangi nyingi.

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,322
Mwaka 2014 haukuwa mwaka mzuri kwangu katika mambo ya mahaba. Baada ya kuwa katika mahusiano kwa karibu mwaka 1 La-azizi wangu alinipa makavu "live" tena bila kupepesa macho kuwa hanitaki. Nikajitahidi kadri ya uwezo wangu kumbembeleza na kumsihi ili atengue kauli Lakini ilikuwa ni kazi bure. Kabla yangu jimbo lilikuwa na mwenyewe alieamua kulitelekeza. Kwa kutumia ving'amuzi na vyanzo sahihi nilijiridhisha La-azizi wangu baada ya kunitema alibaki kuwa 'single'. Hilo lilinitia matumaini na kujaribu kumsihi anisamehe mtoto wa mwanamke mwenzie na turudi kuwa kama zamani. Duuhh huwezi amini nilipewa lugha za kibabe, kebehi, jeuri na maudhi. Mimi ni miongoni mwa wachache ambao tuko karne ya 21 kwa bahati mbaya. Katika kupenda kwangu sijawahi kupenda mtu kwa kuvutiwa na macho, kiuno cha nyigu, miguu ya bia au 'figure' kwa ujumla wake. Mimi kigezo changu ni IQ na weledi wa mtu ktk kupambanua mambo. Kwa kweli huwa nakerwa na watu wenye akili za kushikiwa. Kwa kuwa La-azizi wangu alikamilika ktk mambo ambayo kwangu ndio 'password word' niliumia sana. Hata shughuli zangu za utafutaji nikazihamishia mkoa mwingine. Pamoja na yote hayo sikuwahi kukata tamaa, japo nilipokuwa natuma sms kwenye what'sap ananiblock hata kwa wiki baadae ananifungulia. Nikiwa sina hili wala lile mwezi wa pili alinipigia simu. Mwanzoni alianza kwa kunisalimu Lakini kadri siku zinavyokwenda ameamua kurudi tena kwa kasi ya ajabu. Ooooohhh my baby sahau yaliyo pita, ni wewe tu hakuna mwingine zaidi yako. Kwa upande wangu baada ya kukaa na kutafakari nimeona Sina jinsi zaidi ya kumpokea. Naweza kuwa sipo sahihi Lakini kwangu mapenzi yana Rangi nyingi. Siwezi kushuka kwenye Farasi kwa matarajio ya kupanda Punda.
 
Kweli lakini.........utashukaje farasi......upande punda..........?.....
Horses are there to stay bana.......
 
Yamemkuta huyoo....what goes around comes around!!Uwe makini nae sana atakuja kukuliza tena!Chunguza ujue kilichomkimbiza ni nn na kilichomrudisha ni nini?
 
Alikufanya plan B huyo, ila make sure kule kwa mwenye jimbo mambo yamekoma kabisaaa, maaana wahenga walisema ukiona mapenzi ya ghafla yamezidi ujue kuna ---- kaachwa
 
Mrudishe Leo na kesho umtimue mazima ili apate machungu
 
Mhhh?kipi kilimfanya akukatae na kipi kimemfanya akurudie?
 
Aisee hicho kimeo achana nacho kitakufanya vibaya next time..kimezinguliwa huko eti kinarudi na kujifanya bado kinaupendo na wewe..na hivi mtu mwenyewe unaonekana ni wakulialia ngoja akuonyeshe rangi nyingine..,
 
Ukiona hivo alikokwenda katendwa akakumbuka kiporo chake ikabidi akirudie ila ataondoka tu uyo anapumzika kwa muda
 
huyo lazma aliliwa pembeni afu jamaa akasimamia kucha ukawekwa kando...concluded!!
walivozinguana(kugundua jamaa ana wake ampendae ye au ye hana chance hapo)akakumbuka kuna boya wake kamuweka bench acha arudi TAKE CARE akichepuka tena akakutana na msimamia kucha kwa mara nyingine huna chako!!!!
 
Kwa kifupi jamaa alitemwa baada ya kushindwa kukidhi signature yako ! It takes a real man to make a woman satisfied
 
Mrudishe Leo na kesho umtimue mazima ili apate machungu

Alikufanya plan B huyo, ila make sure kule kwa mwenye jimbo mambo yamekoma kabisaaa, maaana wahenga walisema ukiona mapenzi ya ghafla yamezidi ujue kuna ---- kaachwa

Ukiona hivo alikokwenda katendwa akakumbuka kiporo chake ikabidi akirudie ila ataondoka tu uyo anapumzika kwa muda

Zingatia walichoandika hawa
 
Mrejesho ni muhimu jamanu.....kweli mapenzi yana rangi!
 
Mkuu uwe makini Sana maana Mara nyingi kumrudia ex ni kupoteza muda hasa Kama aliona unang'ang'ania japo wapo wenye bahati ambao walirudi waka Kama zamani.Ila MUNGU alituonya kuhusu wanawake(soma mithali 31:3,version ya kiingereza iko poa zaidi)
 
Ukiona hivo alikokwenda katendwa akakumbuka kiporo chake ikabidi akirudie ila ataondoka tu uyo anapumzika kwa muda
Wahenga walisema "ushikwapo shikamana". Akiondoka tena wenye tatizo nitakuwa mimi. Ukiona Labour turnover kubwa kwenye kampuni basi tatizo sio la wafanyakazi bali ni la kampuni.
 
Aisee hicho kimeo achana nacho kitakufanya vibaya next time..kimezinguliwa huko eti kinarudi na kujifanya bado kinaupendo na wewe..na hivi mtu mwenyewe unaonekana ni wakulialia ngoja akuonyeshe rangi nyingine..,
Hakuna mwanaume shujaa kwenye mapenzi. Kwenye vitabu vya mapokeo hata watu mashujaa na wanaamini walianguka, kumbuka yaliyomkuta Daudi, Samson.
 
Back
Top Bottom