A220-300 / CS 300

Bahati furaha

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
3,030
1,384
Ni hivi karibuni tumepokea ndege nzuri(hata kwa muonekano tu) na iliyoweka rekodi kuwa ndege ya kwanza ya aina hiyo kwa Afrika.
Tunapaswa kujivunia.

Je sisi ndio wa kwanza kutumia ndege hii tuliyoipokea? Ni kwa ajili ya kutaka kufahamu wala si zaidi ya hapo.
Airbus-delivers-First-A220-Air-Tanzania.jpg



Sekunde ya 40 inaonesha vizuri C FOWU


Namba hii ya usajili imehusika na airBaltic
A220.png


Bombardier CSeries/Airbus A220 Full Production List
Angalia namba 55005 na 55047 kisha namba 55034 na 55048

yl-csc-air-baltic-bombardier-cseries-cs300-bd-500-1a11_PlanespottersNet_753017_b0b38f6e4d.jpg


Baadhi ya maeneo YL CSC imefika.
https://www.planespotters.net/photos/reg/YL-CSC


Je, hapa ilikuwa inakarabatiwa?
mwenye ufahamu asaidie tafadhali.

Kwa pamoja tutaijenga nchi yetu.
 
Yote kwa yote, ndege hiyo imetengenezwa na hao mnaowaita mashoga mara mabeberu. Waheshimuni hao watu.
 
Yote kwa yote, ndege hiyo imetengenezwa na hao mnaowaita mashoga mara mabeberu. Waheshimuni hao watu.
Sijazungumzia mashoga wala mabeberu mkuu kwa sababu mimi sio shoga wa jike(la mbuzi).

Concern ni kama hiyo ndege ilishawahi kumilikiwa na airBaltic ama walicancel order tukaichukua?
 
Anayeheshimiwa ni mwenye hela! Wao ndo inabidi watuheshimu sisi. Siku zote mnunuaji ndo mteja na ndo bossy
Sasa nyingi fukara mna hela kuwashinda hao mabeberu? Muulize Iran pamoja na fedha zake alipigwa ban ya kutonunua ndege tangu miaka ya sabini akaishia kuendesha ndege chakavu.
 
Sasa nyingi fukara mna hela kuwashinda hao mabeberu? Muulize Iran pamoja na fedha zake alipigwa ban ya kutonunua ndege tangu miaka ya sabini akaishia kuendesha ndege chakavu.
Kusema ni jambo 1 na kuelewa hasa unachokisema ni jambo jingine mkuu.
Acha tu tutakuwa dona kantri soon.
 
Hizo nadhani ni Letter Codes za usajili kiwandani zinazotolewa mara ndege inapofikia hatua za kuunganganishwa na baadaye kuruka kwa mara ya kwanza. Inawezekana zikawa zinajirudia kulingana na matoleo ya ndege kwa mwezi, kwa sababu C-FOWU iliishawahi kuandikwa kwenye ndege ya Korea CS300 yenye msn 55022 iliyotolewa tarehe 25-01-2018 pamoja na ile ya Air Baltic msn 55005 C-FOWU iliyotolewa tarehe 31-3-2017.....

Inayofuata kwenye mtiririko huo ni Air Tanzania. Ile ya pili msn 55048 imepewa herufi za usajili C-FOUY ambayo tayari iliishatumiwa na msn 55034 CS300 ya Air Baltic iliyotolewa 16-06-2018.

Huko nyuma zaidi hizi codes mbili za C-FOWU na C-FOUY ziliishawahi kutumika kwa ndege za kampuni-mama: Bombardier Aerospace katika matoleo ya CS300 za mwanzo. Naamini huu ni utaratibu wa kiwandani ambao unakuja kurithiwa na namba halisi za usajili kama ilivyo 5H-TCH. Mimi sio msemaji wa kampuni husika, nimejaribu tu kushirikisha wengine kwa kile ninachokijua.
 
Back
Top Bottom