A wise man, changes his mind sometimes

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
Suala la muswada wa marekebisho ya sheria ya katiba ya mwaka 2011, kidogo liingize nchi katika machafuko. Watu walirushiana maneno, vitisho, na ubabe mwingi ulishuhudiwa bungeni na nje ya bunge.

Hatimae Mheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kwa busara ambazo hasa ndio zinazo mpa wadhifa alionao, bila kujali maslahi ya chama au kile wazungu wanacho kiita "Rhetoric" za wabunge wa chama tawala, raisi amesikiliza mawazo ya vyama vya upinzani na Taasisi nyingine, hata kufikia bubadilisha maamuzi yake mwenyewe maana alisha tia saini, na kulazimisha muswada usomwe kwa mara ya pili, kama taifa lilivyokua linataka.

Mpaka wabunge wengine wakafika mbali sana kutaka kumpigia Mtukufu Raisi, kura ya kutokua na imani nae, sijui kwa maslahi ya nani kwa maamuzi aliochukua Raisi.
Any way hilo lina onyesha ugumu wa maamuzi alio chukua Raisi. Wadhungu wanasema, "
A WISE MAN , CHANGES HIS MIND SOME TIMES".

SASA MPENI RAISI HESHIMA YAKE NA HADHI YAKE KWA HILI.

 
Yaani Jambo hili, lisipite kimya kimya. Maana uungwana sio kua kulalamika tu, na hata kusifia juhudi za zinazo uonekana pia ni uungwana.
 
definitely rais ameonyesha uongozi, hekima na busara kwa namna ambavyo ameshughulikia hili suala - anastahili kupongezwa
 
Nampongeza Kikwete kwa hili. Na kimsingi maneno machafu yaliyotolewa na wabunge wa chama tawala yananifanya niamini kwamba, kuna wakati Kikwete anashindwa kufanya maamuzi kwa sababu ya magamba yaliyojaza chama. Kwa mfumo huu, naamini Kikwete anaweza kutuachia kitu ambacho tutakuwa na historia ya kumuenzi.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Tanganyika.
 
Maranyingi sana nahisi, kua Tanzania imepata rahisi sahihi kwa wakati tulio nao. Zamani nilidhani Raisi anatakiwa awe mbabe sana, lakini huyu bwana ana ongoza fair play sana. Full respect to you Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Back
Top Bottom