A tree house

Sky Eclat, kuna hawa ndugu zetu kutoka kabila la Korowai kule Papua New Guinea. Makazi yao ya kitamaduni kwenye vijiji vyao huwa ni ya juu kwa juu. Hebu tafuta documentary za BBC kwa jina Human Planet, ni nyingi, inayowahusu wakorowai inaitwa Forest People. Wakorowai huwa wanapanda hadi na mbwa wao na wanapika na kuwasha moto huko huko juu. Alafu vijitoto vyao huwa vinacheza cheza bila uoga kabisa huko juu ya miti kwenye nyumba.
 
Nitaitafuta mkuu, na wale ni watu wa asili hasa, si ajabu wanajua ni miti gani ukipanda karibu na nyumba nyoka hawasogei karibu.
 
Ndo wenye nyumba kama"MADUNGU "ya kule Rufiji kipindi Cha mafuriko
 
nzuri sana nyumba inavutia, na kwa kweli mtu unaenjoy ukikaa amakupumzika sehemu kama hiyo kwa kuwa ni ya asili. lakini pia inahamasisha utunzaji wa miti pamoja na misitu kwa kuepuka kuangusha mti ili ujenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…