VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Teua/tengua aifanyayo Rais na Mwenyekiti wangu Dr. John Pombe Magufuli haina taswira nzuri. Huonesha na kutonesha 'udhaifu' katika teuzi. Kitendo cha Mteule 'kuchongewa' mbele za Mteuwa wake na Mteuwa kumtumbua siku inayofuata si chema. Nasisitiza, hiki si kitendo chema. Kitendo cha Mteule kukosea mbele ya Mteuwa wake na kutumbuliwa hima si kizuri.
Wakati nikiwa kwenye mifumo ya Serikali na chama, nilifahamu kuwa Wateule hupatikana kwa utaratibu maalum ingawa huteuliwa na Mteuwa. Huchujwa na kuchujika; kuchunguzwa wakachunguzika na kufuatiliwa na wakafutilika. Hujulikana uimara na udhaifu wao. Huteuliwa kwenye nafasi zinazoendana na uimara na udhaifu wao. Na husaidiwa kiserikali au kichama.
Kwasasa nimebaki chamani na sipo tena Serikalini kulipo na uteuzi. Nimebaki kama kada mwandamizi wa CCM lakini nisiye na maamuzi yoyote. Nabaki kustaajabishwa na aina ya viongozi wanaoteuliwa na kutumbuliwa. Wapo wanaolalamikiwa lakini wanachuniwa. Wapo wanaonyamaziwa lakini wanatangaziwa. Mambo yamebadilika. Mambo yamekuwa mambo!
Ndiyo maana najiuliza, Rais huwapata wapi anaowateuwa? Walikuwa timu moja wakati wa harakati zake za 2015 hata kama ni sirini? (maana nawajua waliokuwa naye kuanzia Ukumbini na kwenye kampeni zake wakimuunga mkono waziwazi). wanaletwa na utaratibu unaowachuja na kuwawasilisha kwake? Anawapataje hasa kwasasa? Naichukia tabia ya kumchongea kiongozi waziwazi mbele ya Mteuwa wake.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)