Ilikuwa mwaka jana mwezi wa January nilipotua katika kijiji kimoja kilichopo mkoani Singida, jina la kijiji ni mdida. Nilikuwa katika harakati za kutafuta data kwa ajili ya kukamilisha utafiti fulani. Katika mazungumzo mbalimbali yasiyokuwa rasmi kati ya mimi na mwanakijiji mmoja tulijikuta tukiongelea mambo yanayohusu mahusiano ya kimapenzi baina ya wakazi wa kijiji hicho.
Mwanakijiji huyo aliniambia ni vigumu kukuta katika kijiji hicho wazee hasa wa miaka ya 50 na 60; na baadhi ya vijana wa makamo ambao wameoa mke mmoja tu. Alinionya ya kwamba nisishangae kuona au kusikia kuna wanaume wameoa wake 2-3.
Alienda mbali zaidi aliponiambia ya kwamba kuna mzee mmoja, jina lake ni "Ahmedi Mimbi" maarufu kama Mzee Mrii, kuwa ana wake 12, na mke wake wa mwisho amezaliwa mwaka wa 1978! Nilishtuka lakini alifanya kila jitihada ili kunishusha Munkari.
Nilipata hamu sana ya kujua, kulikoni! "How this guy succeeded to manipulate this bunch of wives".
Nilimwuuliza kama kulikuwa na nguvu au uwezo wowote wa ziada ambao ulimwezesha huyo mzee kumiliki idadi hiyo ya wanawake; jamaa aliendelea kusimulia:
"Mzee Mrii ni tajiri mkubwa wa ng'ombe, ana wake 12, wake 8 wapo katika kijiji hiki cha mdida, na wengine 4 wanaishi katika kijiji fulani kinaitwa Kijota. Kila mke ana watoto kadhaa - wapo wenye watoto hadi kumi na zaidi. Pia Kila mke amejengewa kaya/mji wake. Sifa kubwa ya huyu mzee ni uwezo wake wa kuweza kutoa mahari na kuoa kwa sababu ana ng'ombe wa kutosha, vilevile anajitahidi kuhudumia wake zake kwa mahitaji kadri anavyoweza".
Alidai kuwa, kwa sasa hao ng'ombe wamepungua lakini miaka ya nyuma inakadriwa alikuwa akimiliki ng'ombe elfu kadhaa".
Nilitaka kujua ni kwa namna gani anaweza kuwaridhisha wake hao 12 hasa ikija swala la mapenzi?
Mwanakijiji huyo alidai kuwa kwa kawaida huyo mzee huwa hafanyi kazi nyingine zaidi ya kufanya ziara za kutoka kaya moja hadi nyingine kwa ajili ya kuwahudumia wake zake kimapenzi. Alidai hata hivyo, watoto wake wengi wanafanana naye - ishara nzuri ya matunda ya kazi yake, lakini pia kuna wengine ambao huwezi kuthibitisha moja kwa moja kama ni wa kwake au lah!
Nilimwuuliza je kuhusu swala la kuwasomesha?
Jibu lilikuwa ni kwamba mzee huyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasomesha watoto wake hadi kiwango cha shule ya msingi! Ilidaiwa kuwa, watoto kadhaa wa mke wa pili (seniority) katika orodha hiyo wamefanikiwa kuonja elimu ya sekondari na wengine chuo.
Simulizi zaidi zilidai kuwa huyo mzee ana watoto wanaokadriwa kufika 100 (achilia mbali nyumba ndogo). Umri wake kwa sasa ni mkubwa, kwani msimuliaji alinieleza kuwa huyo mzee ana umri mkubwa kuliko wa baba yake ambaye alizaliwa mwaka wa 1945.
Nilitaka kujua kama anawatambua vizuri watoto wake!
Mwanakijiji aliendelea kufunguka na kudai kwamba, mara nyingi huyo mzee huingia mkenge pale mtoto anapomdai hela kwa ajili ya malipo fulani - hasa michango ya shuleni. Kwani kinachotokea ni kwamba, mtoto yeyote hata wa jirani anaweza kumwibukia na kumwambia naomba hela nikanunue daftari au hela ya mchango, nadaiwa shuleni, kwa sababu ya wingi wa watoto imekuwa ni vigumu yeye kuwafahamu wote - kwa hiyo mara nyingi amelazimika kutoa hela kwa mtindo huo.
Imedaiwa kuwa, hivi karibuni ameunda kamati maalumu inayojumuisha watoto wake kadhaa ambao anawaamini - hiyo kamati kazi yake ni kumhakikishia kama kweli mtoto yeyote anayedai malipo yanayohusiana na malezi ni wa kwake kweli! Pia ili kuepuka "fraud" ya aina yoyote na utapeli wa mara kwa mara. Malipo mengine kama michango ya shule, hulazimika kwenda kuuza ng'ombe na hatimaye kuondoka na fuko la hela kuelekea shuleni kwa ajili ya kulipa michango mbalimbali wanayodaiwa watoto wake. Pia kila mwanamke amegawiwa ng'ombe kadhaa kwa ajili ya kuendesha maisha yake na ya watoto wake.
Imedaiwa kwamba, hivi karibuni amefanya majaribio kadhaa ya kuoa wake wengine, lakini watoto wake hasa wakubwa wamekuwa wakiwawekea ngumu wanawake wanaotaka kuolewa na mzee huyo. Mara nyingi watoto wake huwachimba mkwara au kutishia kuwadhuru wanawake iwapo wataolewa na baba yao - cha ajabu imedaiwa kuwa watoto hawana ubavu wa kukabiliana moja kwa moja na baba yao.
Msimuliaji aliongeza kuwa, watoto wake karibu wote waliofikia umri wa kuoa wana wake zaidi ya mmoja na huenda wana mpango wa kuongeza wengine hapo baadaye. Alibaini kwamba ni mtoto mmoja tu wa rika la juu ambaye ameamua kuwa mkristo na ameoa mke mmoja tu.
Msimuliaji aliniambia ya kwamba hajawahi kuona, kuhisi au kusikia hali yoyote inayoashiria usaliti wa wake hao dhidi ya huyo mzee.
Taarifa zaidi zilieleza kwamba, wanawake/kaya karibu zote zinahasimiana, lakini cha ajabu yeye ameweza kuwadhibiti wake wote 12 na wote wanakiri na kumtambua asilimia 100 kama mume wao!
Overview/comments/questions/
1. Je huyu mzee anatoa wapi nguvu ya kuwaridhisha wake zake wote 12 na mahawara wengine, wakati tunaona na kusikia kila leo hasa hapa mujini Darisalama watu wenye mwanamke mmoja tu wanakimbiwa na wake zao kwa tatizo la kushindwa kuwaridhisha?
2. Ni kwa nini wanawake waendelee kumkubali na kuolewa na mzee Mrii wakati tayari wakijua kuna msururu wa wanawake wengine ambao tayari alikuwa amewaoa?
3. Kwa nini hapakuwa na ugomvi dhahiri kati ya Mzee Mrii na wake zake badala yake wake zake tu ndio wanaogombana? Ndio tuseme alitumia mbinu ya "divide and rule"?
4. Je, hii dhana na uhalisia wa nyumba ndogo au kuoa wake wengi iliyoasisiwa vijijini; na kurithishwa, hasa mijini, ni mwendelezo uleule wa kuwa na wake wengi lakini kwa kificho? Au hii ni "trend" tofauti?
5. Je, tunaweza kusema ya kwamba huyu mzee ameamua kuondoa kabisa unafiki na kuweka mambo wazi, akiashiria na kuitangazia dunia ya kuwa mwanaume kutokana na nature yake hatosheki na mke mmoja? Je, kwa mustakabali huu "is he a hero"?
Kwa kweli nina maswali mengi ambayo nimejiuliza lakini niishie hapa. Wadau bila shaka na nyie mtajiuliza maswali mengi na sote kwa pamoja tunaweza kujadili.

Last edited by a moderator: