" A Frame house" Nyumba zenye umbo A

" A Frame house" Nyumba zenye umbo A

PRO 90

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2012
Posts
301
Reaction score
817
images (2) (24).jpeg
images (2) (8).jpeg
Hello wajuzi.
Ktk tafiti zangu, nimekuwa ninawaza kujenga Get away houses, Airbnb, na ki sehemu kwa ajili ya watu wanaotaka kuishi ktk mazingira ya nature, around sehemu fulani hivi Pwani.

Mwanzo nilikuwa nataka kujenga kama zile za Safari bandaz, Morden Mud houses, ila katk mizunguko yangu nimekutana na hizi " A FRAME HOUSE".

Naona linawekwa zege, tofali zinainuliwa juu, kisha uzekaji wa A FRAME unafata. Humo ndani ,nimeona mbao zikituka sanaa,

Maswali yangu!
Je, jinsi gani ya kuzi tunza? Ishu za mchwa kuna namna ya kukabiliana nazo.??
Nimeona kwa nchi za wenzetu wakiweka insulation material, Je kwa huku tunawezaje kukabiliana na ishu ya hali ya hewa?

Msaada tutani nisije ingia cha kike.
 
inawezekana insulation materials ziko huku pia kwetu.
ningekushauri utumie zile frames flan hivi za chuma ( rectangular frames) alafu mbao zinakuwa kama decoration tu( hapa unatumia tng) kwa ndani au nje lakini structure inabebwa na hizo frame za chuma.
 
View attachment 2992778View attachment 2992779Hello wajuzi.
Ktk tafiti zangu, nimekuwa ninawaza kujenga Get away houses, Airbnb, na ki sehemu kwa ajili ya watu wanaotaka kuishi ktk mazingira ya nature, around sehemu fulani hivi Pwani.

Mwanzo nilikuwa nataka kujenga kama zile za Safari bandaz, Morden Mud houses, ila katk mizunguko yangu nimekutana na hizi " A FRAME HOUSE".

Naona linawekwa zege, tofali zinainuliwa juu, kisha uzekaji wa A FRAME unafata. Humo ndani ,nimeona mbao zikituka sanaa,

Maswali yangu!
Je, jinsi gani ya kuzi tunza? Ishu za mchwa kuna namna ya kukabiliana nazo.??
Nimeona kwa nchi za wenzetu wakiweka insulation material, Je kwa huku tunawezaje kukabiliana na ishu ya hali ya hewa?

Msaada tutani nisije ingia cha kike.
View attachment 2992775
A frames ni nzuri sana kwa space,na pia ni kivutio.Ila kuna mambo ya kuzingatia.
Hii ni kwa uzoefu zangu wa kuzichunguza maana na mimi nina interest nazo.
1.Hakikisha msingi wako unainuka juu-atleast kwenye goti.
2.Weka angalau line 2 za tofali(kwenye kuta za pembeni-kusaidia bati lisiguse chini kabisa--likigusa chini kuna nafasi utakuwa umeifungia ambayo hutaweza kuitumia na uchafu,panya,nyoka wanaweza kujificha humo,pia kurahisisha kuoza kwa bati)---Pia ukiweka line 2-hadi 5(inategemea na mapenzi yako) utapata sehemu za kuweka sockets kirahisi na paa lako litainuka juu zaidi.
3.Tumia mbao nzito-kwenye mbao itakayoshikilia chumba cha kulala(sunroom/attic)---au uijengee juu ya ukuta wa tofali.
4.insulation-kwa mazingira ya Tanzania inategemea na ulipo-ila jitahidi katikati ya bati na gypsum board/mbao unaweka kablanketi kembamba(kama una pesa weka plywood nene/marineboard chini ya bati) kupunguza joto/baridi la nje kufika ndani.
5.Tumia bati zilizokatwa tayari kiwandani-usiunge vipisi.
6.Tumia misumari yenye rubber.
7.Panga vizuri na Fanya wiring kabla hujaweka board/mbao.
8.Bafu/choo vikae chini upande wa nyuma (ukiweka juu au pembeni itakusumbua)
9.Floor ni mapenzi yako.Ila kwa mazingira ya Tanzania-sakafu/tiles ni bora na low risk(mbao itapendeza zaidi ila maintenance yake ni kubwa zaidi na risk ya kupinda,kuliwa na mchwa ni kubwa zaidi).
Narudia😛anga vizuri kabla hujaanza-Tumia fundi mzoefu,japo bati litakuwa na slope kali--fundi awe anajielewa--akitoboa bati mara mbili kugundua leakage na kuirekebisha ni kazi mno.
Ukiingia instagram kuna mtu wa Kenya anaitwa @dachasagana anazo nyingi--utapata wazo moja zaidi,pia tembelea pinterest kukusanya mawazo zaidi.
Kila la kheri.
 
Kuna nchi kujenga nyumba ya mbao ni more expensive kuliko nyumba ya tofali....- Fikiria hili kwa umakini

Another thing, nyumba zinatengenezwa kulingana na mazingira iliyopo. Huku kwetu kuna joto kali, mara nyingi naona nyumba za mbao mazingira ya baridi sana.

Pia ukanda huu una mchwa, unaweza kuta nyumba ikaliwa ghafla hata hujamaliza mwaka

Nyumba za mbao zinawaka unaweza jikuta unaishi kwenye kuni. Mzee aliweka nakshi za mbao mbao urembo kwenye nyumba yake, hizo zilikuwa zinachochea moto ziliwaka balaaa - think about it

Pili hicho kijumba hakina space kabisa, sijajua umependea nini, unaweza kuta unapanda huku unainama

Unataka ujenge nyumba uishi kama uko kichochoroni ? Why?
 
Kuna vipengele kadhaa nataka kuweka sawa...
1.Huku kuwa Mazingira ya Joto : Kwanza inabidi utambue kuwa Mbao ina uwezo mkubwa sana wa kukabiliana na Joto...
-Yaan mbao ni nzuri kwenye joto kuliko Zege au Matofali ya kawaida.

2.Uharibifu wa mchwa : Kemikali za kukabiliana na wadudu waharibifu zipo za kutosha na zinauzwa madukani.
-Mataluma ya reli hasa TAZARA,zipo za mbao na zimedumu miaka ya kutosha

3.Kwenye Moto : Mbao inayo andaliwa kwa ajili ya ujenzi wa nje,hutofautiana na mbao za urembo...
Huandaliwa kwa ajili ya kukabiliana na majanga kama hayo
 
Mbao inakuwa bora zaidi kwenye cold climate utake usitake. Haimanishi hazipo kwenye joto kali, ila ukiona pwani hakuna nyumba za mbao ujiulize why?

Tutabishana kila mtu atavutia upande wake. Ila hizo mbao unazotaka kuweka wewe zinawaka kama kuni

Second mbao ngumu zinauzwa expensive sana ubao mmoja mkongo au mninga unauzwq kuanzia 75000 mpaka 150,000

Sasa brother unataka kujenga nyumba kwa Cyprus au pines? Be serious

Hata hizo mbao ambazo zinachukua mda kuliwa ni aina ya mbao chungu plus mbali ba kuweka dawa, in regular intervals.

Kwa pwani siafiki hata kidogo hakufai kujenga aina hiyo ya nyumba anayotaka mwamba
 
Kuna mbao,,zenye:
1.Kuhimili maji chumvi
2.Kuhimili kemikali
3.Ugumu wa Chuma
4.Kudumu hadi karne
5.Kuhimili joto
6.Kuhimili wadudu...

Tafuta mda jifunze juu ya miti kama Cedar,Redwood,Ikoro,Teak,Oak,Douglas Fir and Clove tree....

Sababu kubwa ya mbao kutotumika kwa baadhi ya maeneo ni
-Kukosa ujuzi wa kuweza kuzuandaa,Kuziboresha na kuzijengea...
Hapa nchini hatuna mafundi mbao waliokwiva...
-Bei : Hii siyo sababu kubwa sana,kwani kuna matilio ni bei kwelikweli ujenzi na watabe wananunua na kuweka ndani.
 
Mbao inakuwa bora zaidi kwenye cold climate utake usitake. Haimanishi hazipo kwenye joto kali, ila ukiona pwani hakuna nyumba za mbao ujiulize why?

Tutabishana kila mtu atavutia upande wake. Ila hizo mbao unazotaka kuweka wewe zinawaka kama kuni

Second mbao ngumu zinauzwa expensive sana ubao mmoja mkongo au mninga unauzwq kuanzia 75000 mpaka 150,000

Sasa brother unataka kujenga nyumba kwa Cyprus au pines? Be serious

Hata hizo mbao ambazo zinachukua mda kuliwa ni aina ya mbao chungu plus mbali ba kuweka dawa, in regular intervals.

Kwa pwani siafiki hata kidogo hakufai kujenga aina hiyo ya nyumba anayotaka mwamba
Wakati wasema pwani mbao hazifai..unasahau kuwa
1. Ngalawa na Meli kubwa nyingi zilitengenezwa kwa mbao na zinapita kwenye maji tena ya Chumvi...

2. Magofu ya Bagamoyo ni yalitumia mbao badala ya nondo

3.Nenda Zanzibar ukaone ujenzi wa Resort ukifanywa kwa mbao

Kwenye Materials science tunasema : Materials zote zina nguvu sawa : Ni ujuzi ndiyo utakao kufanya utumie matilio gani....
 
Again aina gani ya mbao? Go back to my previous statement

Kweli nishaona nyumba nyingi za mbao ila sio mwambao huu wa pwani. Utoke nje ya mji huko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom