A.E. MUSIBA - Ndani ya "UCHU"

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Ninapomkumbuka Mtunzi huyu ambaye ni marehemu huwa nahuzunika sana.
Ni kielelezo cha vile kalamu ya mwandishi wa Riwaya anavyotakiwa kuwa.
Hakuandika bora ameandika, alifanya utafiti na akajua nini cha kuandika, Hebu
tumtazame kidogo katika Riwaya yake ya UCHU.

"Nchi imegeuka, ubinafsi umetawala roho za viongozi wetu, wanajifikiria wao tu.
Si viongozi wa wananchi tena, ila wanatafuta uongozi kwa faida yao wenyewe.
Hata ukiangalia ni viongozi wachache sana kwa sasa ambao si matajiri. Wanaingia
katika uongozi wakiwa hawana kitu, lakini baada ya muda mfupi unawakuta wakiwa
wameshajilimbikizia mali. Afadhali wangefanya hivyo halafu wakaendelea kuwasaidia
wananchi ili na wao hali zao ziinuke, la hasha, sera zao ni kuwadidimiza wananci wawe
maskini pamoja na vizazi vyao ili wasiwe na sauti kabisa. Sauti wanataka ibaki yao na
vizazi vyao ili wabaki madarakani kama wafalme."
(UK. 18)

Maneno haya na mengineyo yananifanya nimuheshimu sana mzee huyu ambaye ni marehemu
kwa jinsi alivyokuwa na uwezo nzuri wa kutumia kalamu yake. Kwanini huwa namkumbuka sana

Juzi nimesafiri kutoka DAR kwenda Mtwara. Kilichonishangaza ni kukuta vizuizi baadhi ya maeneo
huku kukiwa na askari wenye SMG tayari kufyatua pale itakapolazimika. Baada ya kudadisi nikaambiwa
kuwa ni vizuizi vya kuwazui awakulima wasitafute masoko mazuri ya korosho zao badala yake wakopeshe
kwenye vyama vya Msingi vya ushirika. Yaani wenyewe wamelima bila kusimamiwa wala kusaidiwa
huku wengine wakikosa hata pembejeo kwa ajili ya mashamba yao loh! Inauma sana.

Baada ya uliza yangu ya hapa na pale naambiwa wanaohusika kuwakandamiza wakulima kiasi hicho
ni Hawa Ghasia, Mkuchika na Mbunge wa Tandahimba Juma Njwayo ambao kwa pamoja wanauhujumu
umoja wa wakulima ambao unataka kuuza mazao yao wenyewe. Hii ni Aibu kuwa na viongozi kama hawa.
Natafuta scaner niweze kuiweka barua ya Tamisemi ambayo inauzuia umoja huo kufanya kazi.

Ukikisoma kitabu cha UCHU utakubaliana nami kuwa fasihi imefanya kazi inayotakiwa.
 
waache waendelee kuonja joto la jiwe. Hiyo ndiyo zawadi watakayo endelea kuipata baada kuwachagua wanandoa magamba na CUF kama watetezi wao...!
 
Back
Top Bottom