JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,249
- 5,743
SWALI: Ulipoanza kazi, ulifanya na nani na hali ilikuwaje?
(Katika maandishi kutokana na video hii)
Maisha ya kazi wakati nasoma pale katika hicho chuo cha Fordham University, nilikua nafanya kazi part time kwenye ubalozi wa Tanzania New York. Na wakati ule balozi, ambaye anaitwa permanent representative, ndio kwa nafasi za wale ambao wanawakilisha mataifa yao umoja wa mataifa, alikua ni Dr. Salim Ahmed Salim na nakumbuka wakati ule katibu mkuu wa foreign affairs alikua ni bwana mmoja, na bado yuko hai, anaitwa Anthony Nyaki.
Na baada ya zile kazi nilizozifanya waliona, manake nlikua nafanya kazi part time lakini ilikua ni kazi ya research, ndio ilikua ni kubwa zaidi pale. Kwa hiyo kuwafanyia kazi, kama kuna maswala Fulani kuyafanyia utafiti zaidi na nini. Ni kama vile supporting staff katika shughuli zao.
Nakumbuka katibu mkuu wakati ule, Nyaki, akasema tunaweza tukampa nafasi akaweza akatoa mchango wake. Na wakati huo nilikua nimemaliza degree yangu ya kwanza. Basi, nikajiunga na foreign service, nikaweza kuwafanyia kazi. Lakini sasa ikiwa siwafanyii kazi, nafanyia kazi taifa langu, nikawa najifanyia kazi mimi mwenyewe.
Na bahati nzuri, ikaonekana kwamba ninaweza, kwa kuwa nilikua already niko pale New York, naweza nikaanzia pale pale New York. Kwa hiyo nikaanza kazi yangu pale new york, lakini kazi kubwa sasa ambayo mimi ninasema ninashukuru, kwa mtizamo wa wakati ule, nikapewa kazi katika kamati; unajua zipo kamati sita za umoja wa mataifa.
Kuna kamati ya kwanza ambayo inashughulikia maswala ya disamarment. Na wakati ule ilikua cold war, mapambano makubwa sana kati ya Warusi, upande wao wakiwa na WARSAW PACT wakati Wamarekani wakiwa na NATO, NATO PACT. Kwa hiyo ni kamati ambayo ilikua inashughulikia maswala ya armament, disarmament, hasa disarmament na haya maswala ya nonproliferation of nuclear weapons katika dunia.
Kamati ya pili; maswala ya uchumi tu. Yote ya dunia haya unaona. Maswala ya uchumi, hali ya uchumi ilivyo, hali ya uchumi katika nchi, hali katika mataifa.
Kamati ya tatu ni maswala ya human rights ambazo tunazijua, tunaona mapigano kuweza kupata rights zao watu katika dunia.
Kamati ya nne ilikua decolonization, mambo ya ukombozi. Nchi nyingi za kiafrika wakati ule, ingwaje tulikua tunaona tumepata uhuru, lakini nyingi kwa mfano South Africa, wakina Namibia, wakina Mozambique, wakina Guinea Bissau, São Tomé and Príncipe na wengine walikua bado bado kabisa wakiwa chini ya utawala wa kikoloni pamoja na South Africa yenyewe ikiwa chini ya apartheid.
Lakini kamati ya tano ilikua inashughulikia maswala ya administration na maswala ya finance ya umoja wa mataifa. Na kamati ya sita maswala ya kisheria; legal issues, legal questions zote ambazo unaziona kama za kuestablish treaties.
Sasa kulikua kuna na special committies ambazo zipo lakini kubwa ni hizi, na mimi nikaja kuwekwa kamati ya tano na kamati ya tano ilikua inashughulikia maswala yote ya administration ya umoja wa mataifa na maswala yote ya finance ya umoja wa mataifa, ilikua hakipiti kitu kinachohusu mambo ya fedha kama hakijapita katika kamati ya tano, kwa hiyo nikaingia pale.
Na mimi nashukuru uamuzi wa viongozi wakati ule kuniweka katika kamati hiyo kwa sababu ilinipa mimi nafasi. Hakuna kitu cha umoja wa mataifa mpaka leo tunavyozungumza kinachoweza kikapita ambacho kina financial implications kisipite katika kamati ile.
Kwa hiyo inakupa nafasi ya kuujua umoja wa mataifa vizuri, kujua function ya umoja wa mataifa vizuri, kujua mwenendo na matumizi ya umoja wa mataifa vizuri. Kwa hiyo nilikua katika kamati hiyo ambayo nilifanya, mimi naweza kusema kwamba nilifanya kila jitihada ya kuhakikisha kwamba taifa letu linawakilishwa vizuri, lakini pia chini ya uongozi wa Dr. Salim, ambaye mimi naweza nikasema kwa kua mimi nilifanya kazi chini yake for quite some time na nilikua bado ni kijana na yeye alikua bado umri wake haujawa, hajawa mtu mzima kiasi hicho of course na mwalimu alikua in power wakati ule.
Kwa hiyo nasema kwamba kwa kweli nilikua katika timu ambayo naweza kusema kwamba ni timu ilikua nzuri sana na ukiwa na watu kama akina Anthony Nyaki yule mzee, ambaye alikua ndio katibu mkuu. Yeye bado yupo huyo nyaki lakini akaja kuja katibu mkuu mwingine baada ya Nyaki, Nyaki alikwenda katika wizara ya defence wakati ule yalivyokuja mambo ya iddi Amini ugomvi na nini, mapambano yale, walimhamisha foreign wakampeleka defence na pale akawekwa mtu mmoja anaitwa Daniel Mtonga Mloka, ndIo akaja kuwa katibu mkuu pale.
Of course unfortunately ameshafariki wakati huu na nini lakini ni watu ambao walikua wenye uwezo mkubwa na ambao tulifanya nao kazi vizuri katika kuliwakilisha taifa letu huko nje.
SWALI: Tueleze maisha yako ya kazi...

Nilifanya kazi mimi New york, niliingia pale katika ngazi ya chini kabisa kama third secretary maana yake ziko zile rank zile, unaaza third secretary, unakuwa second secretary, unakuwa first secretary, unakuwa councilor, unakuwa minister councilor, unakuwa minister plain potentially then of course unakuwa balozi.
Kwa hio zipo hatua ambazo unazipitia kabla hujafika ngazi ya juu. Kwa hio mimi nilianza hizo third secretaries pale na kwakweli kwa kuwa nilikuwa nafanya research pale, kwa hio nilikuwa na background ya mambo mengi pale, kwa sababu nilikuwa nafanya kazi pale part time lakini baadae nilipopata ile nafasi na nikawa officer sasa, nikafanya kazi pale kama third secretary lakini nikapata nafasi sasa ya kuiwakilisha Tanzania katika mikutano mbalimbali.
Kwa mfano nilikuwa naweza kutoka New York na kwenda Geneva katika vikao vya ECOSOC. Economic and social council ambayo inashughulika na maswala ya kijamii lakini na maswala ya kiuchumi ya dunia nzima na ya nchi mbalimbali. Of course kuna maswala ya human rights na human rights center ikiwa pale New York na inakupa nafasi ya kukutana na wawakilishi wa nchi mbalimbali, wenye mawazo mbalimbali, wenye misimamo mbalimbali na kadhalika.
Kwa hio nikafanya kazi mimi pale kama third secretary, nikapanda nikawa second secretary alafu nikarudi nikaja nyumbani, nikawa foreign affairs hapa. Nakumbuka mimi nilirudi kutoka New York 1982, nakumbuka vizuri sana wakati nimerudi Dr. Salim nilikuwa naye New York akiwa balozi wangu lakini wakati ule alikuwa foreign minister.
Kwa hio kwa kuwa alikuwa ananifahamu na ule uwezo wangu ama limitation zangu alikuwa anzifahamu za kazi. Niliingia katika economic department ya wizara ya foreign affairs ambayo ilikuwa chini ya legal and international organization department ambayo ndio ilikuwa department mama lakini mle kulikuwa na sections mbalimbali ikiwemo section ya mambo ya uchumi, kwa hio nikafanya pale, nikapanda nikawa first secretary nikiwa hapo lakini baadae sasa Dr Salim alipofariki mheshimiwa Sokoine akiwa waziri mkuu, Dr. Salim akatoka Foreign akaenda kuwa waziri mkuu.
Kwa hio mheshimiwa Mkapa akarudi sasa pale foreign akawa waziri wangu na mheshimiwa Mkapa of course nilisafiri nae sana katika safari zake wakati akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje na mimi of course nilikuwa desk officer na nikishughulika maswala ya uchumi na kadhalika kwa hio nikapata nafasi ya kuwa na hawa viongozi ambao walikuja baadae kuwa viongozi wa kitaifa kwa maana ya kusema kuwa Rais na kadhalika.
Kwa hiyo wakati niko pale as first secretary nikapanda nikawa councilor nikiwa hapa, nakumbuka mheshimiwa Mkapa akawa anasema kuna baadhi ya balozi iko haja ya kuzipa nguvu na moja ya balozi alisema lazima ipewe nguvu zaidi ilikuwa ni ubalozi wa Geneva na kwa hio mimi mpaka leo nakumbuka kabisa, kwenda kwangu mimi pale Geneva wakati ule nikiwa councilor ilikuwa ni uamuzi wa waziri mwenyewe wala haukuwa uamuzi wa katibu mkuu. Ulikuwa ni uamuzi wa waziri mwenyewe ambae alikuwa ni mheshimiwa Mkapa wakati ule. Sasa nimekwenda wakati nakwenda Geneva aliokuwa balozi sasa wakati ule pale Geneva alikuwa ni mzee Amir Jamal.
Amir Jamal of course mtamfahamu, I think the longest serving finance minister wa Tanzania kwa sababu kwa ujumla wake katika miaka yote, alikuwa finance minister wa Tanzania kwa miaka kumi na sita. Nikamkuta pale Geneva lakini nakumbuka kabisa mzee Mkapa alinipa mafunzo mazuri sana, akasema unapoenda utamkuta mzee Jamal, ni mtu mzima sana kwa hio nenda nae vizuri, uwe mnyenyekevu, uwe msikivu.
Akasema unajua watu wakishafika umri Fulani na kwa kuwa yeye ni mzee, amefanya kazi katika taifa hili kazi kubwa, kwa hio ilikuwa kama kuniasa kwamba niende vizuri, nafanye nae kazi vizuri mzee Jamal. Kwa hio nikienda Geneva, nilivyoenda Geneva hio ilikuwa 87, nilikwenda pale nikakabidhiwa mambo mengi ya kufanya pale lakini pia kwa bahati nikawa mwakilishi maana Geneva pale ndipo yalipo mashirika mengi ya umoja wa mataifa pale ya kina ILO, wakina WHO, wakina ITU of course WTO na kadhalika lakini yapo mashirika ya umoja wa mataifa ambayo yako Vienna.
Sasa tunawakilishwa pale Geneva lakini pia kuna uwakilishi wa Vienna na pale Vienna kuna UNIDO ambayo inashughulikia sana maswala ya industrialization lakini kuna maswala ya International atomic energy agency na hio agency iko based pale in Vienna.
Bahati nzuri of course nikapata nafasi ya kuwa altenate representative maana yake representative alikuwa mzee Jamal lakini mimi nikapata nafasi ya kuwa namba mbili ya uwakilishi, kwa hio mara kwa mara nilkuwa nakwenda Vienna katika maswala ya Industrialization, mikutano yao ya industrialization lakini pia na maswala ya international atomic energy agency na nakumbuka wakati nakwenda katika vikao vile, mheshimiwa Gharib Bilal, vice president alikuwa university of Dar es Salaam lakini pia alikuwa ndiye mkubwa wa Tanzania radiation commission ambayo iko based in Arusha kwa hio alikuwa anakuja in that capacity kama mkubwa wa Tanzania radiation commission, kwa hio mheshimiwa Gharib Bilal tulikuwa tukiwakilisha Tanzania pamoja lakini of course yeye akitokea hapa, mimi nilikuwa nikitokea pale, kwa hio kazi zikawa zinaenda vizuri.
Ukaja ubalozi, ubalozi wenyewe ulivyokuja, ubalozi wangu huwezi ukauchukulia kama kwa sababu tayari nilikuwa wakati niko Geneva na wakati nafanya kazi za uwakilishi, kuna shirika moja linaitwa world intellectual property organization ambalo ni one of the agencies za UN, ziko agencies 16 na hii ni one of the sixteen katika zile kumi na sita.
Wao wakani-offer kazi, wakani-offer kazi kuwa incharge wa program ya Africa pale, sasa ikabidi lazima niombe ruhusa nyumbani, nisingeweza kwenda namna hii, na nilivyoomba ruhusa nyumbani, nakumbuka wakati ule chief secretary ikulu alikuwa ni mzee Paul Rupia, nikawasiliana nae, of course akasema leta hayo makaratasi, nikampelekea akayasoma, akasema jambo jema kwa nchi yetu kwa hio tutakupa ruhusa. Kwa hio ilikuwa January 1990 nika-join United Nations kwa maana ya kusema kwamba nika-join hili shirika. Wakati nimeli-join sasa nafanya kazi, kwa kweli siwezi nikajipigia filimbi lakini kuna vitu vingi baada ya kuingia pale nilivifanya kwa nchi yetu.
Kwa mfano, Tanzania kama member wa shirika hili, kila mwaka membership fee yake ambayo walikuwa wanalipia katika shirika hili, ilikuwa 24,000 dollars kila mwaka, of course mimi baada ya kuwa pale nikatengeneza utaratibu Fulani wa kushirikisha nchi Fulani kama India na nchi nyingine zinazoendelea, tukatoka hapo na hii records wananzo na hili swala nililifatilia na wakati ule haijawa BRELA, ilikuwa transformed kuwa BRELA na mimi nilisaidia wakati niko outside, kwa sababu of course course wanaoshughulikia maswala ya trademarks, maswala ya patents hayo lakini pia na maswala ya registration of companies etc.
Tukatoka, tukaweza kunegotiate wakati nikiwa ndani na tukatumia argument ya kutosha na tukatumia member states wengine, Tanzania ikatoka katika kulipa dola 24,000 kila mwaka, tukarudi ambapo Tanzania ikawa inalipa dola 800 kila mwaka, you can imagine the saving ambayo niliweza kuitoa in term of foreign exchange kwa wakati ule. Lakini hii haiku-apply for Tanzania peke yake, tuli-argue hizi least developed countries, hizi nchi masikini lazima zipewe a relief, tukatizama ni kitu gani ambacho wanakipata Internationally katika hizi patents, katika trademarks etc. Sasa ninasema tu ni mfano lakini pia ofisi yao pale kitengo cha trademarks.
Computers ambazo ziliwekwa pale at the time ambazo tuliweza kuwaletea abount ten computers za kuweza kufanya processing, mambo ya registration na nini ili waweze ku-offer trademarks kwa sababu trademarks zinakuwa registered kwa upesi zaidi kuliko hata patents, patents ni suala la uvumbuzi etc, It's a long process. Kwa hiyo tuliziweka pale, kutokana na yote haya lakini pia Tanzania tukaingia katika chombo kinaitwa The Madrid club ambayo iko chini ya organization hiyo, by being there unakuta kila mwaka baada ya registration zinazofanywa Internationally mnarejeshewa pesa kiasi flani.
Basi wakati ule serikali wakaona ili kunipa nguvu zaidi kwa kazi ambayo nilikuwa naifanya na kwa kuwa nilikuwa bado on secondment, nilikuwa foreign affairs, wakani-promote to the rank ya kuwa balozi, kunipa nguvu, kuweza kufanya kazi na kweli nikafanya kazi za uwakilishi waTanzania nikiwa katika shirika hili la umoja wa mataifa ambayo niliweza ku-rise maana yake niliingia mimi kama director pale, lakini nikaweza ku-rise mpaka wakati natoka nilikuwa ni assistant director general ambayo unaweza kusema ni level ya assistant secretary general katika umoja wa mataifa which was actually senior enough katika kazi zangu na katika kazi za uwakilishi.
*Zingatia hii ni swali la pili & tatu katika orodha ya maswali yaliyojibiwa. Kwa taarifa zaidi tembelea - [video]https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-jamiiforums-na-khamis-kagasheki.html[/video]

Last edited by a moderator: