50M per month one of my wish for 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

50M per month one of my wish for 2011

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Nxt Millionaire, Jan 27, 2011.

 1. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Habari wana Jamii,
  Tunapoanza mwaka ni vyema kuwa na malenge ama NDOTO au VISION kadhaa ambazo mtu angependa kufikia, nina malengo na ndoto nyingi kwa mwaka huu lakini moja ya ndoto hiyo ni kuingiza japo Milioni 50 kwa mwezi, sijui kama ni Tsh, $ au € sikumbuku ni alama ipi niliiona ndotoni, kwangu hiyo haijalishi mradi ifike 50m au zaidi.

  Najua kuna watu humu jamvini wanakwazika sana unapozungumzia kuhusu pesa au faranga, sijui ni sababu gani zinazowakwaza, lakini kama vile Yusufu pamoja na kukwazwa na kuchukiwa na nduguze hakuacha kuwaelezea ndoto zake, nami mniwie radhi iwapo nitamkwaza yoyoten kwa VISION zangu lakini sina budi kuiweka wazi kwa ni lazima itakuwa halisi siku moja.

  Waweza FUATILIA HAPA ikiwa ujakwazika au wapenda kujua zaidi.

  Kazi njema kwa wote.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Nimefuatilia ndugu yangu,nimeona ndani kuna forever living wakati Mungu kasema watu wote tutakufa,halafu mbona kuna nyuzi mbili za aina moja au una majina mawili mkuu? Na ile ya juzi imeishia wapi? Ni maoni mkuu,usinielewe vibaya.
   
 3. A

  Aalim Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakutakia kila la kheri. Inawezekana kabisa, hata hapa TZ kuna watu wanapata zaidi ya hizo tena si kwa ufisadi. Kaza buti KAKA.
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ni ndoto nzuri, malengo mazuri.
  Kila la heri.
   
 5. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu sijakupata wamaanisha nini, kwamba wote tufe sasa au?
   
 6. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana Aalim kwa kuntia moyo, nami nataka ata zaidi ya hizo za halali.
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Uzi wako umeanza vizuri sana,
  Niliposoma na kufika ktkt nikakutana na kitu kingine kinaitwa forever living,wakati ukweli ni kwamba hakuna biashara idumuyo milele chini ya jua. Lugha isikutishe,ila hiyo forever living ndio duh inatisha. Si kwamba siijui.
   
 8. babalao

  babalao Forum Spammer

  #8
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Next millionaire hata mimi nina ndoto za kuwa millionaire ila tu nadhani njia tunazotumia kufika huko zinatofautiana kuwa na ndoto malengo au--- chochote utakachokiita ni jambo la kwanza kwani maisha ni kama safari ukiwa na ndoto au malengo unajua unakokwenda, taabu inakuja ni jee unatumia njia gani kufika huko kihalali au fisadi,utatumia usafiri gani kufika huko, kwa miguu, bajaji, ndege meli nk. Angalizo unaweza kufika huko with honor or without honor mkuu nitafute tubadilishane mawazo birds of the same feather fly together simu yangu ni namba 0755394701
   
 9. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Utakuwa umeota 50m zim dollar! maneno ya kijiweni hayo, fanya kazi za uzalishaji: acha mambo ya "shotkati"-utapata zaidi ya hiyo kwa wiki!
   
 10. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thanks, Nitakutafuta Babalao
   
 11. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Amoeba hiyo currency sidhani kama ina-exist au ilisha exit, na hizo hata kwao hazikuwa za kuota bali kuokota.
  Thanks for the contribution.
   
 12. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu katika dunia hii ili uweze kupiga hatua kimaendeleo unabudi kupanga mikakati na malengo kama hakuna kufa yaani You will live forever, ingawa twapaswa kufanya ibada na kuomba Mungu sana kama twafa kesho, ila utakapoishi kama wafa kesho na kusali kama waishi milele utapata matokeo bila shaka lakini hayatakuwa sawa na huyo wa mwanzo.
  Good Lucky.
   
 13. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa faida yetu, Saidia Jukwaa kuonyesha ni vipi malengo yaweza timia.......
   
 14. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekusoama Smarter, bila shaka nitaonesha jinsi gani nimetimiza malengo hayo, nashukuru Mungu kwamba kwa mzwezi wa January nimefikia asilimia 10 ya lengo, najua kwa msaaada wa Mungu anayejibu maombi mwezi huu wa pili nitafikia kama si alilimia 100 ya lengo basi karibu yake kiduuuchu.
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  bado unazunguka tu....
   
 16. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu.ngoja tukutakie kila la heri ktk kutimiza ndoto zako.ili mradi tu utumie njia za amani ktk kutekeleza malengo yako, usitumie njia za shari, au za kifisadi.Kila kitu kinawezekana chini ya jua kwake anayeamini na kutenda.GOOD LUCK MAN.
   
 17. Nxt Millionaire

  Nxt Millionaire JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu na ubarikiwe, ni njia halali kabisa, no ufisadi, no shari, its by LEGAL MEANS.
  Thank and God bless you.
   
Loading...