50 wakimbia CCM kujiunga- Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

50 wakimbia CCM kujiunga- Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Jul 2, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  NA MWANDISHI WETU
  WAKAZI wa Kibwegere, Kata ya Kibamba Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wameaswa kukiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ili kiwaletee maendeleo ya kweli.
  Nasaha hizo zimetolewa jijini jana, katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya kitongoji cha Manzese,na Diwani wa Kata ya Saranga Efraim Kinyafu (Chadema), ambaye ameteuliwa na chama chake kuwa mlezi wa kata hiyo,
  Katika mkutano huo, Kinyafu alisema iwapo wakazi hao watakubali mabadiliko ya uongozi kwa kukiunga mkono Chadema kwa asilimia mia moja uhakika wa kuyapatia ufumbuzi matatizo yao utapatikana.

  Alibainisha kuwa matatizo yote yanayowakabili wakazi hao yakiwemo ya elimu duni, huduma mbovu ya upatikanaji wa maji na miundombinu mibovu ya barabara havikuja vyenyewe bali vimesababishwa na utawala mbaya wa Chama cha Mapinduzi (CCM), usiojali maslahi ya wananchi.
  “Jipangeni kukiunga mkono Chadema haswa kwa kuwachagua viongozi wake kuanzia ngazi za shini hadi Ikulu, ambapo tuanziye na serikali za mitaa mwaka 2014 kisha udiwani, ubunge na urais mwaka 2015, hapo Kichaguweni kiwaondolee kero zenu zote”alisema Kinyafu.
  Alisema hadi sasa nchi hii inakabiliwa na tatizo la uongozi bora kutokana na viongozi wengi walioko madarakani kufikiria matumbo yao kwanza.
  Naye katibu wa chama hicho Vitalis Muro, wakati akikabidhi kadi kwa wanachama wapya 50 waliyokihama Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema inasikitisha kusikia kuwa kuna baadhi ya wakazi wa eneo hilo hawamjui diwani wa Kata kutokana na kushindwa kwake kuitisha mkutano tangu achaguliwe.
  Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho.
  Vile vile aliwataka wakazi baadhi ya wakazi wengine kujitokeza katika kujiunga na chama hicho ambacho kimenuia kuwakomboa kutoka kwenye utawala wa kifisadi.

  Kiganyi, JF.
  Mwanzo - wotepamoja.com


   
 2. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,584
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  dawa yao hawa magamba ni kwenye kura tu, haiwezekani hoja nzito zikapewa majibu mepesi, madaktari walikuwa na hoja zaidi ya tatu yeye ****** anajibu moja tu ya nyongeza ya mishahara.
   
Loading...