50 bil to train 25 personel for 30 days!

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Bei ya ngozi yaporomoka

Na Mwandishi wetu
21st May 2009

Bei ya ngozi imeporoka kutoka Sh 2,000 kwa kilo hadi Sh.500, imefahamika.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Nelson Kilongozi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya zao la ngozi yanayotolewa kwa wataalam 25 wa ugani nchini yanayofanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Mifugo Tengeru.

Kilongozi alisema alisema bei ya ngozi hiyo kavu imeporoka kwa kasi katika soko la ndani na nje ya nchi na kusababisha wafugaji kukosa mapato ya kutosha.

Alisema ngozi mbichi nayo bei yake imeporomoka kutoka Sh 1,200 kwa kilo hadi kufikia Sh 300.

Hata hivyo, Kilongozi alisema wameunda kikosi kazi kinachotarajiwa kushirikiana na wadau wengine nchini kuinusuru sekta ya ngozi na kwamba utaoji wa mafunzo kwa maafisa ugani hao ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo.

Alisema mafunzo hayo yamemepewa kipaumbele kikubwa kwa sababu yanatarajiwa kutolewa kwa wagani kutoka halmashauri 75 nchini.

Alisema awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yanayotolewa kwa wagani wa halmashauri 25 katika Chuo hicho yatagharimu zaidi ya Sh. Bilioni 50 .

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima alisema sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto ikiwamo ya kushuka kwa bei ya ngozi na kunakochangiwa na sababu mbalimbali ikiwamo ya mtikisiko wa uchumi duniani

Shirima alisema mtikisiko huo pia umeathiri soko la mazao ya mengine ya mifugo yakiwamo maziwa lililokuwa limeanza kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Arusha kwa kuuza bidhaa hiyo kwenye hoteli za kitalii .

Alisema serikali inaendelea kukabiliana na changamoto hizo na kuwataka wadau wa sekta hiyo kuendelea kuhamasisha soko la ndani la mazao ya mifugo.

CHANZO: NIPASHE
 
ZeMarcopolo,

Please hebu fika hapa tuangalie hii figure, je tuamini gazeti au tusiliamini?

Ninajipa moyo kidogo kuwa gazeti limekosea!!!
 
ZeMarcopolo,

Please hebu fika hapa tuangalie hii figure, je tuamini gazeti au tusiliamini?

Ninajipa moyo kidogo kuwa gazeti limekosea!!!

Aiseh Pundamilia nadhani kuna namna fulani hawa jamaa wamekosea kumnukuu huyo mheshimiwa. Ati!!! Billion 50???? Haingii akilini hata kidogo!! Kwani hii ni semina ya Ngurdoto???
 
Aiseh Pundamilia nadhani kuna namna fulani hawa jamaa wamekosea kumnukuu huyo mheshimiwa. Ati!!! Billion 50???? Haingii akilini hata kidogo!! Kwani hii ni semina ya Ngurdoto???

Wamekosea itakuwa, ila ni uzembe mkubwa, kukosea neno bilioni badala ya milioni kwa mfano , ingekuwa ni tarakimu sawa. Ila kama ni kweli bilioni 50, twafa!
 
Teh teh teh waacheni jamani wachume, watakosea magazetini tu au mpaka kwenye check?
 
Hiyo title nayo sidhani kama iko sawasawa.....ukisoma ndani wanasema, mafunzo hayo yanatolewa kwa wagani kutoka halmashauri 25 nchini...na si wagani 25 kama title inavyosema....!

Sasa swali ni je, kila halmashauri inawakiliswa na wagani wangapi?

Hata na hivyo.....na mimi bado ninawasiwasi na usahihi wa figure hiyo!
 
Back
Top Bottom