Habari hii nimeisikia leo asubuhi BBC kuwa katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kuna wasichana na watoto wa kike 5,000 wakisubiri kufanyiwa tohara a.k.a kukeketwa katika mwezi huu wa Desemba. Kwa mujibu wa mtu mmoja aliyekuwa akihojiwa kuwa tukio hilo ni sherehe kubwa inayofurahiwa na wenyeji wa eneo hilo kiasi kwamba ilifikia hatua kulikuwa na msafara wa magari yakielekea huko kunako "site" na watumiaji wengine wa barabara likiwemo gari la polisi kusimama pembeni kupisha msafara huo???
Hivi hata kama ndio kudumisha mila kwa maoni yangu hiki kitendo si cha kiungwana hata kidogo ukizingatia madhara mbali mbali anayopata msichana wakati na baada ya kutahiriwa achilia mbali kukosa radha halisi anapofanya mapenzi....
Wakati mwingine ni vizuri kutafuta ukweli wa mambo kabla ya kukimbilia kusema kitu bila uhakika au kuwa na usahihi.
Wala tusitake kudanganyana hapa, suala la ukeketaji haliko tanzania tu, na katika tanzania haliko mara pekee, kuna mikoa kama singida, kilimanjaro, dodoma, arusha kwa mfano wanafanya ukeketaji.
Naomba aje mtu athibitishe kitakwimu na kisayansi kwamba wanawake wa mikoa niliyotaja ama tuseme moja kwa moja mkoa wa mara, kwamba wanawake wanaopata matatizo kutokana na huo ukeketaji, idadi yao ni kubwa kulinganisha na wasiokeketwa.
Lakini pia nataka niwaulize kitu kimoja, hivi mnafikiri hawa wasichana wote wanaokeketwa au wazazi/walezi wao hawana uelewa kabisa wa kinachoendelea duniani? Inawezekana wengi mmezaliwa na kukulia mijini, hamjui umuhimu na maana ya utamaduni, japo hata wa makabila yenu, pengine hata makabila yenu hamyajui. Haya mambo ya kujifunza utamaduni kwenye vitabu na magazeti YA Shigongo yanawasumbua wengi, ndio tunaishia kuwanyooshea kidole wengine. Utamaduni au mila ya mtu hata kama unaiona ni mbaya huwezi kuiondoa kwa siku moja, ama kwa amri ama sheria, unahitaji muda wa kutosha kuonyesha madhara ya hiyo mila. Na hayo madhara yanatakiwa yaonekane bayana, sio ya kufikirika, vinginevyo mtaendelea kuwashangaa watu wa mara kila baada ya miaka miwili libeneke linaendelea.