5,000 wanasubiri visu na nyembe!!!!...hii mbaya kabisaa...!!!!!!!!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
409
Habari hii nimeisikia leo asubuhi BBC kuwa katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kuna wasichana na watoto wa kike 5,000 wakisubiri kufanyiwa tohara a.k.a kukeketwa katika mwezi huu wa Desemba. Kwa mujibu wa mtu mmoja aliyekuwa akihojiwa kuwa tukio hilo ni sherehe kubwa inayofurahiwa na wenyeji wa eneo hilo kiasi kwamba ilifikia hatua kulikuwa na msafara wa magari yakielekea huko kunako "site" na watumiaji wengine wa barabara likiwemo gari la polisi kusimama pembeni kupisha msafara huo???

Hivi hata kama ndio kudumisha mila kwa maoni yangu hiki kitendo si cha kiungwana hata kidogo ukizingatia madhara mbali mbali anayopata msichana wakati na baada ya kutahiriwa achilia mbali kukosa radha halisi anapofanya mapenzi....
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,599
1,677
Waandishi wa habari wanaweza andika chochote hata kama hawana uhakika ili mradi wapate pesa kwa kuuza habari zisizo sahihi
Nani alikwenda kuwahesabu?
Watachapwa mapanga na wakurya shauri yao!!
Watawekewa wanted mkoa wa mara!!
Hawajamaa ni noma kama ukiwachakachulia habari zao kwa uongo
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
Si madogo!

Katika suala zima serikali inatuhakikishia vipi usalama wa kiafya wa hao wanao tahiriwa?

Serikali imehakikisha vipi suala la kuzuwia maradhi ya kuambukiza?
 
seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
53
FGM is a crime against girl child; kwani hao hawaishi Tanzania? It is forbidden, it is wrong, it is depriving a child/girl her right, it is biologically destructive, emotionally harmful, and in wrong in every aspect of the word....wrong, wrong, those concerned must be taken legal action...Where are gender activist in this country and in that part of the country?
 
seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
53
And by the way, this topic does not deserve to be under mahusiano, mapenzi etc. It should be moved elsewhere and if there is no category, perhaps mods should open one under "gender" or "human rights" or anything of that sort. This is abuse of children has wasichana
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
Waandishi wa habari wanaweza andika chochote hata kama hawana uhakika ili mradi wapate pesa kwa kuuza habari zisizo sahihi
Nani alikwenda kuwahesabu?
Watachapwa mapanga na wakurya shauri yao!!
Watawekewa wanted mkoa wa mara!!
Hawajamaa ni noma kama ukiwachakachulia habari zao kwa uongo

Hata kama si 5,000 ni 5 tu basi bado hapa kuna walakin. Tunahitaji kusikia msimamo wa serikali kwenye hili.

Wizara husika inasemaje?
 
seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
53
Hata kama si 5,000 ni 5 tu basi bado hapa kuna walakin. Tunahitaji kusikia msimamo wa serikali kwenye hili.

Wizara husika inasemaje?
Ni kweli Gaijin, idadi si issue, issue ni girl child rights hata kama ni mmoja, na issue is to abolish kabisa this backward culture which is destructive
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
Haki ya mzazi kwa mtoto wake ni mpaka kitu gani?

Nini mipaka kwa mila na tamaduni?

Serikali ingechukuliaje kama kungekuwa na mila inayolazimisha jamii moja ya watu kutolewa jicho moja?
 
Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,033
2,296
Mkuu wa Polisi (OCD) alipoulizwa wao wanachukua hatua gani? Alisema ".. watoto wa kike wanajipeleka wenyewe kukeketwa... wanaona kama ni kitendo cha ushujaa fulani..."!!!
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
Mkuu wa Polisi (OCD) alipoulizwa wao wanachukua hatua gani? Alisema ".. watoto wa kike wanajipeleka wenyewe kukeketwa... wanaona kama ni kitendo cha ushujaa fulani..."!!!

Meaning.......?

Kama watoto underage watajipeleka wenyewe kwenye nyumba za ukahaba ndio utaacha tu waendelee?
 
Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
409
Waandishi wa habari wanaweza andika chochote hata kama hawana uhakika ili mradi wapate pesa kwa kuuza habari zisizo sahihi
Nani alikwenda kuwahesabu?
Watachapwa mapanga na wakurya shauri yao!!
Watawekewa wanted mkoa wa mara!!
Hawajamaa ni noma kama ukiwachakachulia habari zao kwa uongo
...Na wewe ni mura wa kughecha nini? maana nasikia hata wanaume wa kule hawataki kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana asiyekeketwa....mmezoea vya kunyonga jifunzeni na vya kuchinja basi radha ipo sana tu sio kuwaumiza hao mabinti.
 
seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
53
Mkuu wa Polisi (OCD) alipoulizwa wao wanachukua hatua gani? Alisema ".. watoto wa kike wanajipeleka wenyewe kukeketwa... wanaona kama ni kitendo cha ushujaa fulani..."!!!
Mtu yeyote anayetaka kutetea culture hawezi kukosa "an excuse" of some kind...Hili la kusema watoto wa kike wanajipeleka..." can be viewed on two levels: 1) Watoto wanafundishwa na kuwa blinded/hypnotized kiasi kwamba wanaona wasipofanya they will not fit in the society...this is some sort of underlying coercion. hoja ambayo inatolewa hata na watu/wanaume wanao-advocate polygamy, eti first wives will sometimes suggest to her husband to marry another woman....to share "burden"...
2) Lack of awareness concerning dangers of this crude rite among the society hasa kwa wasichana....lack of knowledge is detrimental
 
Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
409
Meaning.......?

Kama watoto underage watajipeleka wenyewe kwenye nyumba za ukahaba ndio utaacha tu waendelee?
..Hapo ndipo ninapotilia shaka utendaji wa hawa polisi eti na kuwa msichana asipokeketwa wengine huwa wanafikia hatua ya kujinyonga kwa kuwa huwa wanadharaulika mbele ya wanawake wenzao...bure kabisa!
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,599
1,677
...Na wewe ni mura wa kughecha nini? maana nasikia hata wanaume wa kule hawataki kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana asiyekeketwa....mmezoea vya kunyonga jifunzeni na vya kuchinja basi radha ipo sana tu sio kuwaumiza hao mabinti.

Sijui hata ulichoandika:redfaces:
 
Fab

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
762
14
nimepatwa hadi baridi.....
mwili wote umekufa ganzi......duh
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,941
Habari hii nimeisikia leo asubuhi BBC kuwa katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kuna wasichana na watoto wa kike 5,000 wakisubiri kufanyiwa tohara a.k.a kukeketwa katika mwezi huu wa Desemba. Kwa mujibu wa mtu mmoja aliyekuwa akihojiwa kuwa tukio hilo ni sherehe kubwa inayofurahiwa na wenyeji wa eneo hilo kiasi kwamba ilifikia hatua kulikuwa na msafara wa magari yakielekea huko kunako "site" na watumiaji wengine wa barabara likiwemo gari la polisi kusimama pembeni kupisha msafara huo???

Hivi hata kama ndio kudumisha mila kwa maoni yangu hiki kitendo si cha kiungwana hata kidogo ukizingatia madhara mbali mbali anayopata msichana wakati na baada ya kutahiriwa achilia mbali kukosa radha halisi anapofanya mapenzi....

Wakati mwingine ni vizuri kutafuta ukweli wa mambo kabla ya kukimbilia kusema kitu bila uhakika au kuwa na usahihi.
Wala tusitake kudanganyana hapa, suala la ukeketaji haliko tanzania tu, na katika tanzania haliko mara pekee, kuna mikoa kama singida, kilimanjaro, dodoma, arusha kwa mfano wanafanya ukeketaji.

Naomba aje mtu athibitishe kitakwimu na kisayansi kwamba wanawake wa mikoa niliyotaja ama tuseme moja kwa moja mkoa wa mara, kwamba wanawake wanaopata matatizo kutokana na huo ukeketaji, idadi yao ni kubwa kulinganisha na wasiokeketwa.

Lakini pia nataka niwaulize kitu kimoja, hivi mnafikiri hawa wasichana wote wanaokeketwa au wazazi/walezi wao hawana uelewa kabisa wa kinachoendelea duniani? Inawezekana wengi mmezaliwa na kukulia mijini, hamjui umuhimu na maana ya utamaduni, japo hata wa makabila yenu, pengine hata makabila yenu hamyajui. Haya mambo ya kujifunza utamaduni kwenye vitabu na magazeti YA Shigongo yanawasumbua wengi, ndio tunaishia kuwanyooshea kidole wengine. Utamaduni au mila ya mtu hata kama unaiona ni mbaya huwezi kuiondoa kwa siku moja, ama kwa amri ama sheria, unahitaji muda wa kutosha kuonyesha madhara ya hiyo mila. Na hayo madhara yanatakiwa yaonekane bayana, sio ya kufikirika, vinginevyo mtaendelea kuwashangaa watu wa mara kila baada ya miaka miwili libeneke linaendelea.
 
Fab

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
762
14
akina kyekue wa kilimanjaro hawatahiri...
afu sio kwa vile mikoa mingine inafanya tohara na nyie mfanye..
hili jambo linatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote...,
mie namjua mtu ameshindwa kuolewa sababu ya hii kitu...
its soo unfair...
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,941
Si madogo!

Katika suala zima serikali inatuhakikishia vipi usalama wa kiafya wa hao wanao tahiriwa?

Serikali imehakikisha vipi suala la kuzuwia maradhi ya kuambukiza?[/QUOTE]

wangapi wanapata magonjwa ya kuambukizwa kila siku na wala hata hiyo habari ya kukeketwa au hata kukeketwa kwenyewe hawakujui?
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,941
Meaning.......?

Kama watoto underage watajipeleka wenyewe kwenye nyumba za ukahaba ndio utaacha tu waendelee?Tafadhali sana mama, usifananishe mila yetu na ukahaba. Hizi tabia za ukahaba zipo huko mjini msikokeketwa.
 
Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Mar 18, 2010
593
63
nikiri kwanza kuwa mimi mwenyewe ni mwenyeji wa mkoa wa mara na nimewahi kuwa na uhusiano na mwanamke aliyekeketwa na asiyekeketwa kwa nyakai tofauti. anachosema mwita maranya ni sahihi na ningependa kizingatiwe. ukeketaji una faida zake hasa za kisosholojia na kisaikolojia.

kimaumbile, kutokana na uzoefu wangu, kuna tofauti kubwa sana ya mwanamke aliyekeketwa na asiyekeketwa katika kuhiriki mapenzi. japo naungana na watetezi wa aki za binadmu kuwa kumkekeketa mtu ni kumpunguzia kiungo muhimu mwilini mwake na kumnyima haki yake ya asili aliyopewa na Mungu. ikizingatiwa kuwa wengi wa wanaokekektwa wako under 18, basi ni dhahiri kuwa hukeketwa bila ridhaa yao. pamoja na kuwa jamii yangu ina utamaduni huu na mila hii. napinga ukeketaji kwa msingi wa kibinadamu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom