mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,229
- 4,554
Mabinti hawa wanne wa Kifilipino wanatufungia mwaka 2015 kwa kuwaonyesha Waingereza kwamba hakuna lisilowezekana chini ya jua.
Wakiwa wanatokea katika familia masikini ya Kifilipino baba yao akiwa mzoa taka walisimama na kusema lazima wabadili hali ya familia yao kupitia vipaji vyao vya kuimba.
Wakihojiwa na waandishi wa habari walisema walianza kuimba katika mashindano ya kupiganisha majogoo mchezo ambao ni maarufu nchini humo, kidogo kidogo wakaanza kuwa maarufu.
Lakini ndoto zao hazikuwa kuishia katika jiji la Manila, bali kwenda mbali zaidi, walipania kwenda kwenye mashindano ya kutafuta vipaji wakianzia nchini mwao na kuvuka mipaka katika nchi ya Korea na kwingineko ambapo kote walitwaa mataji na kuwaacha wenyeji vinywa wazi.
Lakini kote huko ndoto zao zilikuwa hazijatimia walipania kwenda nchini Uingereza kushiriki mashindano ya X Factors.
Baada ya kupanda jukwaani na kuonyesha umahiri mkubwa, Simon mmiliki wa mashindano hayo pamoja majaji wenzie na washabiki waliofurika kwenye ukumbi huo alibaki vinywa wazi wasiamini wanachokiona.
Mabinti hao waliimba wimbo mgumu wa Jessie J wa Bang Bang kwa umahiri mkubwa.
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kupanda chat hadi fainali ambapo Waingereza kwa roho mbaya zao au labda na wivu wakawanyima kura, lakini waliwashikisha adabu Waingereza na kuwa gumzo nchini humo.
Huo ukawa ndiyo mwanzo wa kujulikana kwao kimataifa.