4G ya Airtel

Mi nina wiki kama tatu hv natumia 4g ya airtel nilishangaa tu ikapanda na kuwa lte(4g)

Toka siku hiyo voda nimeiweka mahabusu
Uko maeneo gani mkuu. Mie Niko Arusha Airtel 4G siipati
 
Ila mkuu speed yao unaionaje?wanaweza kuwaweka Vodacom bench kweli kwa upande wa speed?

Line yangu imeshasoma 4G ila sijaitest nina bundle la voda nalimalizia kwanza.
Mkuu ulienda kubadilisha line au imesoma yenyewe?
 
Watumiaji wa hii 4G ya airtel ningependa maelezo ya ziada. Je, airtel wanatumia band gani kwa 4G yao, pamoja na Speedtest japo chache tujue kama ipo vizuri au ni yale yale (4g jina)
Angalia #43 nimeweka speedtest
 
Mkuu Hapa umechanganya megabyte per second na megabit per second, megabyte kwenye kifupi chake inakuwa na B kubwa mfano MBps na megabit inakuwa na b ndogo Kama Mbps.

Megabyte 1 Ni sawa na megabit 8

Hivyo unapodownload kitu kwa 6MBps kwenye idm Ni sawa na kupima speed ikaonesha 48mbps.
 
Anhaa Ahsanteh Mkuu kwa Elimu basi hili lilikuwa ni tatizo langu boss kufananisha hayaa maneno,Nimejifunza

Basi kwa Airtel naona kuna mda nikidownload kitu inakamata hadi 2.7MB/s na Tigo wanacheza 4 MB/s kwa 4G mi naona si mbaya sana kwa hizi speed.

Kwa Hilo basi VODA wako juu zaidi sema tu Tatizo bei za Packages zao.
 
Kwa vifurushi vya Airtel Sasa Hivi Ni moja ya mtandao Bora kusema kweli, mwanzo walikuwa hawana mvuto sababu ya speed Yao japo vifurushi Ni vizuri.

Zamani nilikuwa naunga 500MB kwa 500 Voda, pamoja na dakika za mitandao yote na sms, ila Voda wamepunguza mpaka 250MB, Airtel Wana vifurushi same ila still unapata 500MB.
 
4G+ kwa nchi nyingine inachezaga 70 Mbps kwenda 150 Mbps na zaidi kwa Tanzania hii mitandao inayotangaza 4G+ hata spidi zao hazifiki za Vodacom.

naona TTCL mwaka Jana sijui juzi walisema wana 4G+ lakini hadi leo hii kwa matumizi yangu sijawahi ona ikivuka 30 Mbps, Tigo nao wanasema wana 4G+ lakini spidi yao ya kusikitisha.. Labda kama kuna fundi wao hapa anielekeze maeneo hapa Dar walipo funga hiyo 4G+ niende nikajionee
 
Kwa hiyo simu ikiwa na 4g automatically ni 4g+? Na kwenye signal inatakiwa ionyeshe +?
 
Kwa hiyo simu ikiwa na 4g automatically ni 4g+? Na kwenye signal inatakiwa ionyeshe +?
Sio necessary kwamba simu ikiweza kusoma 4G itaweza kuwa 4g+, unabidi uangalie kwenye box kama inasupport LTE-A au 4G+. Simu za zamani kidogo 2013 kurudi nyuma zilikuwa zina 4G lakini ni Cat 3 100/50 Mbps, kwahiyo zilikuwa hazi support LTE-A au 4G+ lakini simu za siku hivi nyingi zinakuwa na LTE-A Cat 4,6,9, 16,18,20 so zinasupport 4g+

Cat 4 ina support spidi hadi download/upload 150/50 Mbps
Cat 6 300/50 Mbps
Cat 9 450/50 Mbps
Cat 16 1024/150 Mbps
Cat 18 1200/200 Mbps
Cat 20 2048/150 Mbps


Unaweza kuangalia Gsmarena simu yako inasupport Cat kwenye eneo la "Speed" ili ujue kama inaweza support LTE-A au 4G+. Lakini sidhani kama kuna simu ya siku hizi ambayo haisupport LTE-A
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…