1. ndio speed itaongezeka
2. kama simu yako haina 4g hutaona tofauti yoyote itakuwa ni kama tu line ya kawaida
Ooh okay, kwa hivyo kama mtu hatumii simu ya 4G hashauriki kwenda kwa ajili ya hiyo huduma mkuu ni bora akaendelea na hiyo 3G right ?.
Na vipi kuhusu gharama ukilinganisha 3G na 4G...?.
Thanks a lot mkuu.
Ooh okay, kwa hivyo kama mtu hatumii simu ya 4G hashauriki kwenda kwa ajili ya hiyo huduma mkuu ni bora akaendelea na hiyo 3G right ?.
Na vipi kuhusu gharama ukilinganisha 3G na 4G...?.
Thanks a lot mkuu.
Bora uwe na smile maana wao wako bora zaidi
Ubora wao ni Upi ukilinganisha Tigo 4G?
Au siku hizi wanatoa Voice na Data?
yap kama huna simu ya 4g huna haja na line ya 4g na gharama za 4g zipo juu sana, na vifurushi vya 4g ni ghali 1gb sh 10,000 kwa siku 7, gb 20 sh 180,000 kwa mwezi nk
Bado haujaweza Onesha Ubora wa Smile dhidi ya Tigo
Duh, aisee hii siihitaji kama ndio hivyo hainifai aseee acha tu nibaki na GB zangu 15 kwa 1500Tshs. nadhani zinatosha hizi kuliko hizo zipo expensive sana kwa kweli, khaaa !!.
mkuu GB 15 kwa 1500??? line gani hiyo na unajiunga vipi
Well, hizi 15GB zinakuwa ni siku 2 kwa 1500Tshs. Tigo. Inakuwa ni saa 5:00usk - 11:00asbh, sasa utakuta mtu kama mi nikiwahi kulala labda ni saa sita na nusu au saba kasoro kwa hiyo nikiwa nahitaji kushusha vitu siku najiunga nashusha vitu vya kutosha for two days.
Nilikuwa naongea na mtu jana akaniambia voda wanatoa 4GB kwa 1500Tshs usiku pia. Sasa hii ya Tigo kwangu inanifaa kabisa. Kwa mchana natumia 500Tshs napata GB1 au 500Tshs napata 180MB itategemea nataka kufanya nini kwenye net mkuu. Lisaa limoja kwa Tigo unapata 200MB kwa 100Tshs, hivyo nikitaka 1GB natumia 500Tshs napata 1GB mambo yanaenda tu kiongozi. Ni hivo tu mkuu.