Kwa jina maarufu hujulikana kama beltway (barabara) ya kufunga mkanda. Usipofunga mkanda hapo ni hasara yako. Magari yote husafiri kwa spidi ya kati ya 100km/h na 130km/h. Ingawaje spidi ya mwisho kipolisi ni 80km/h.
Ni jibarabara kubwa lenye lane nyingi linalozunguka eneo lote la Washington DC na vitongoji vyake.
Chukulia barabara izunguke jiji la Dar. Ukitaka kutoka Tandika kwenda Tandale huhitaji kupambana na msongamano wa magari wa Temeke, Kariakoo. Magomeni ndio ufike Tandale. Unaingia kwenye hili jibarabara kwenye exit iliyo karibu na Tandika na unatoka katika exit iliyo karibu na Tandale.
- Of course ni barabara isiyo na mashimo.
- Haina taa za kuongoza magari yapishanayo. traffic lights)
- Haina baiskeli wala wavuka kwa miguu.
- Ina over pass nyingi nyingine juu nyingine chini kuepuka msongamano wa magari kutoka barabara nyingine.
- Imezungushiwa kuta ndefu kuzuia makelele ya magari yasiwafikie wakazi wanaoishi karibu na barabara hiyo.
- Ina vibao vinavyoonyesha spidi inayokubalika, exits, umbali nk.
- Ina vibao vya matangazo kama kuna ajali, msongamano. gari linatafutwa, hali ya hewa nk
- Ina express lanes na (HOV). Express lane huwa ni za kulipia. Ukijiona una haraka sana unapita kwenye lanes hizo. HOV ni lane ambayo haruhusiwi kuendesha gari peke yako katika masaa ya msongamano wa magari mengi (rush hour)
- Ina madaraja marefu, mapana na ya kisasa.
- Ina polisi wengi wanaotumia magari ya polisi na yasiyo na alama za polisi.
- Ni barabara ya kiungo. Wanaotoka majimbo ya kusini mwa DC hawahitaji kukatiza katikati ya DC kuendelea na safari kaskazini mwa DC.
Ni barabara muhimu kwa kifupi babu kubwa.
Kazi kwenu wakandarasi wa Bongo. Changamoto hiyo.