Hivi mmesikia hii ya wazimu flani na tajiri mwenye range? Tajiri mmoja alipenda sana kunywa chai kwenye mkahawa flani. Alikuwa akiegeza gari lake anaingia kwenye mkahawa. Wazimu flani akapita akaona gari lake kule nyuma limeandikwa 4x4, naye akaandika na kipande cha kaa =16.
Tajiri alipotoka akakasirika akapeleka gari carwash. Siku ya pili hivyo hivyo =16 -car wash, ya tatu tajiri hasira zikamzidi akaipeleka garage ikaandikwa kwa rangi 4x4=16, akasema basi nimewaweza.
Siku ya nne alipotoka kunywa chai kwenye mkahawa kazunguka gari akitabasamu ghafla akabadilisha sura kuona 4x4=16 -/(tick imeongezwa kama vile mwalimu amesema umepata!)