4 baraza la katiba mpya tanzania 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

4 baraza la katiba mpya tanzania 2011

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Iga, May 28, 2011.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  BAADHI ya Watanzania wanaamini kuwa serikali na uongozi uliopo nchini hivi sasa utaitendea haki katiba mpya na kuwatendea haki wananchi wa nchi hii kwa kukubali kuwepo kwa Baraza la Katiba Mpya Tanzania 2011 au Mkutano Mkuu wa Katiba Mpya Tanzania 2011. Je, wewe mkulima unayehamasishwa hapa chini unasemaje ?


  MKULIMA.
  TULIPOPATA uhuru ilisemekana eti Uti wa mgongo wa taifa letu ni kilimo. Mkulima na vijiji vimebadilika kidogo sana toka tupate uhuru. Ingawa tumejenga kiasi mijini lakini vijiji vimesahaulika.

  Serikali na chama tawala vilipoua ushirika halisi na kuleta ushirika wa kisiasa mkulima aliathirika vibaya sana.

  Vijiji vya Ujamaa lilikuwa ni wazo zuri lakini watendaji wa serikali wakatumia fursa hiyo kuchukua ardhi nzuri ya vijiji na kuwahamisha wakulima karibu na barabara au kwenye maeneo yasikokuwa na rutuba hata kidogo.

  Mamlaka nyingi z amazao zilizoanzishwa zilimnyonya na kumuibia zaidi mkulima kuliko kumsaidia na wanasiasa taratibu wakavila na kuviua vyama vya ushirika.

  Soko huria na siasa za kiliberali zilipoingia mkulima tu ndiye ambaye hakuruhusiwa kuuza mazao au bidhaa alizozalisha nchi za nje. Na hadi wa leo soko la mkulima limekuwa likivurugwa na serikali na wanasiasa. Tujiulize:

  i. Kama tumekubali soko huru jambo hilo halimhusu pia mkulima;
  ii. Kwanini tusimruhusu moja kwa moja mkulima kuuza mazao yake nchi za nje kwa taratibu atakazopanga yeye na wenzake;
  iii. Je, tukimhakikishia mkulima soko linalomlipa bei za kishindani kilimo hakitafanikiwa;
  iv. Je, VICOBA vya kilimo haviwezi kuendeshwa kwa namna ambayo sio tu ni benki za kijamii, bali pia ni chombo cha bima na hifadhi ya mkulima (Social security fund);
  v. VICOBA vya wakulima vikishirikiana na benki za maendeleo ikiwemo hiyo ya kilimo haziwezi kujipanga ili kuhakikisha wakulima wengi iwezekanavyo:
  -wanakopeshwa matrekta;
  -wanapata mbegu, mbolea na mahitaji yao mengine kirahisi na kwa namna isiyowagharimu fedha yote kwa wakati mmoja;
  -wanasaidiwa kutafuta masoko kabla ndani na nje ya nchi;
  -wanafikishiwa hutuma muhimu vijijini kama vile maji, umeme na miundombinu kwa kutumia pia idara ya VICOBA itakayopewa jukumu la utoaji huduma muhimu kijamii na kibiashara;
  -Je, VICOBA, Benki ya Kilimo, wafadhili na serikali itawasaidiaje wakulima kuwa na nyumba bora na huduma zote muhimu ili pamoja na kilimo vijiji viweze kuendesha pia biashara ya utalii wa vijijini na kilimo;
  -Kila inapowezekana VICOBA na BENKI ya Kilimo visaidiwe uanzishwaji wa viwanda vidgo vitakavyowasaidia wakulima kuuza unga sembe badala ya kuuza mahindi; kuuza ngano iliyosagwa badala ya mali ghafi ya ngano; kuuza mchele badala ya kuuza mpunga na kuuza mafuta ya kupikia badala ya kuuza alizeti na nyonyo;
  -Je, hivi wizara ya Kilimo na chakula inatakiwa iwe na wafanyakazi wanaoishi na kuonesha mifano vijijini au wapunge upepo wa bahari kama sio wa bonde la TAZARA?

  -Na yote haya yatazungumzwa na nani kama sio mwakilishi halali na anayetegemewa kuzungumza kinachotakikana kama sio mwakilishi wa wakulima/wanavijiji;

  Jitayarisheni, jiandaeni na kujihami na nguvu za hoja kuhusu umuhimu wa kuwa na Baraza au Mkutano wa Kitaifa wa Katiba Mpya 2011 na wala sio Tume au Kikundi cha wateuliwa wachache hata kama ni mawaziri, wabunge, majaji, wanasheria na engineo kama hao, maana historia inaonesha wote hao hawawezi kutetea maslahi yako wewe na kwamba mwamba ngoma ngozi lazima avutie kwake au sio?
   
Loading...