Kweli Aisee, ila Naona Kwa Hawa Mafarao Inaweza Ikawa Ndo Safari Yao Wenyeji Maana Hapa Ndo Watapata Kipimo Halisi Cha Ubora Wao Maana Hawajakutana Na Vigingi Kama Alivokutana Navyo Farao...Mwanzoni Wakati Michuano Inaanza Niliwadharau Sana Hawa Mafarao Na Kiungo Wao Elneny Mpigwa Benchi Kule Arsenal
Historia Nayo Inawabeba Misri Kwenye Hii Michuano....Japo Current Form Ndo Kitu Muhimu Zaidi...Ngoja Tuone Mambo Yatakavokuwa Maana Mpira Bhn Unaeza Shangaa Burkina Faso Ya Traore Ndo Ananyayua Ndoo Hapa
Mimi nimehamia Cameroon baada ya Nigeria yangu kutolewa aisee nitaenda na Burkina Faso na Cameroon kwa sasa Ila kuhama kunaendelea Kwa kuzingatia ushauri wa madaktari humu ndani
Kuna wa2 wanakera sana, akiwachukia waarabu bac atataka wote wawachukie waarabu, akiona unashabikia timu yoyote ya waarabu/waislamu anatamani akupasue kichwa. Lakini kushabikia timu za mabeberu ni kawaida kwao. Huu ushenzi wa kubagua timu kisa rangi/waarabu cjui utaisha lini!
North Africans mara nyingi wanajiona sio Africans..., Hizo timu huwa nazishabikia World Cup tu ila sio African Nations; Na historically waarabu walikuwa na gamemanships sana; Huu Upuuzi wanaofanya Cameroon sasa Waarabu ndio ilikuwa tabia zao...
Chuki dhidi ya waarabu haitakusaidia chochote,
hebu niambie ligi ipi inashika no 1 in afrika kwa ubora na umakini kama siyo ya waarabu! Kagoogle utakutana na top 10 zimejaa za waarabu. Alafu unakuja kuwasema hapa eti hao waarabu ni wa kawaida 🤣 huku hapakufai, ni heri ukabakia jukwaa la kimataifa na udini mzee