Nadhani wananchi bado hawana imani na wapinzani, bado wana imani na CCM ingawa ina mapungufu mengi na imeshindwa kuleta mabadiliko ndani ya miaka 50 kama alivyofafanua Nguruvi3 hapo juu. Ni wajibu wa vyama vya upinzani kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mabadiliko hasa katika kipindi hiki. Wengi wana hofu wakiangalia candidates wa urais katika upinzani wakilinganisha na watangaza nia wa CCM wanaona kama vile upinzani hawana watu wenye uwezo.
Hatusikik chochote kuhusu "Tume huru" sasa sijui wanasubiri baada ya matokeo ndo waanze zile hadithi zao za tumeibiwa kura?!
Mag3 asante sana
Hadi pale tutakapong'amua Root cause ya matatizo yetu watanzania ndipo tutaweza kujikomboa
Hapa tulipo tunajua kabisa kuwa kuna tatizo...But how comes hakuna hata mmoja kati yetu anayeonesha nia ya kupambana na hayo matatizo...sisi wenyewe tunaishia kuandika tu kwenye key board.
Watanzania tuko wazuri sana wa kulalamika na kuongea maneno mengi.,..na hicho ndicho tunachokifanya siku zote.Likija suala la kutenda wote tuko walewale hakuna kitu,...sio upinzani sio chama tawala.
Pia tukubali kuwa viongozi tunaowapata ni zao la jamii tuliyomo...tukipata viongozi wala rushwa maana yake ni jamii inapenda rushwa...Tukipata viongozi porojo wasioweza kutenda maana yake ni zao la jamii yetu.
Tutaweza kutoka hapa pale ambapo tukiweza kubadili culture yetu
(1) Ni kweli kwa kiasi fulani kwamba jamii(jamii nikiwa na maana ya watanzania) yetu ndiyo inayozaa wala rushwa lakini nadhani si kweli kuwa jamii hiyo imejaa wapenda rushwa tu kisa imezaa wala rushwa..!!. Jamii yetu imegawanyika katika makundi yafuatayo ukiingalia kupitia kona ya masuala ya rushwa:.....
.
Pia tukubali kuwa viongozi tunaowapata ni zao la jamii tuliyomo..(1).tukipata viongozi wala rushwa maana yake ni jamii inapenda rushwa...Tukipata viongozi porojo wasioweza kutenda maana yake ni zao la jamii yetu.....
JokaKuu, pamoja na yote ukweli usiopingika ni kwamba Upinzani hapa nchini unafanya kazi katika hali ngumu sana na kuwa mpinzani Tanzania kunataka moyo. Kuwa mpinzani ni sawa kutangaza vita dhidi ya utawala ulioko madarakani na hivyo kuwa tayari kuyaonja machungu mikononi mwa vyombo vya dola. Hebu shuhudia visa hivi viwili;..I am 50/50 na huu mtizamo wako.
..let me tell u the 50% that disagrees with u.
..I dont think wa-Tz wanapenda rushwa na ufisadi.
..pia sidhani kama viongozi tunaowapata ni reflection ya wa-Tz.
..nasema hivi, kwasababu siamini kama kuna chama cha upinzani Tz kinaweza kumsimamisha fisadi kuliko mafisadi wote halafu kikawashinda CCM.
..wapinzani wamekuwa wanashindwa kwasababu hawajafanya juhudi za kutosha kujitangaza kwa wananchi huko vijijini ambako ndiko kura za ushindi zilipo.
..CCM wako kitaasisi zaidi ya upinzani. Wako makini ktk hatua zote za kuelekea uchaguzi, kuanzia kuandikisha wapiga kura, kutunza vitambulisho vya kupiga kura, kufanya kampeni, na mwisho kwenda kwa wingi vituoni.
..Kwenye kila uchaguzi, wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wamewekewa malengo maalumu ya idadi ya wanachama ambao wanapaswa kuhakikisha wamekwenda kupiga kura.
..Wapinzani wanatakiwa nao kuwa na mpango kazi mzuri zaidi ya ule wa CCM kwa hatua zote za kuelekea ktk uchaguzi mkuu.
cc Bulldog, Alinda, Nguruvi3, Mag3
1. said:WAKATI Jeshi la Polisi mkoani Iringa likimkamata na kumshikilia kwa muda wa saa tano kisha kumwachia huru Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, pamoja na wabunge watatu, kiongozi huyo amesema kuwa endepo kesi hiyo itafikishwa mahakamani itakuwa ya 10 kufunguliwa na jeshi hilo.
Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na vilevile mbunge wa Hai alikamatwa jana asubuhi pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Diwani wa Kata ya Mitimirefu, Frank Nyalusi, wakidaiwa kuzidisha muda wa mkutano.
Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao, kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi, alisema kuwa walizidisha muda wa mkutano wa hadhara uliofanyika juzi katika viwanja vya Mwembetogwa kwa zaidi ya dakika 25.
..I am 50/50 na huu mtizamo wako.
..let me tell u the 50% that disagrees with u.
..I dont think wa-Tz wanapenda rushwa na ufisadi.
..pia sidhani kama viongozi tunaowapata ni reflection ya wa-Tz.
..nasema hivi, kwasababu siamini kama kuna chama cha upinzani Tz kinaweza kumsimamisha fisadi kuliko mafisadi wote halafu kikawashinda CCM.
..wapinzani wamekuwa wanashindwa kwasababu hawajafanya juhudi za kutosha kujitangaza kwa wananchi huko vijijini ambako ndiko kura za ushindi zilipo.
..CCM wako kitaasisi zaidi ya upinzani. Wako makini ktk hatua zote za kuelekea uchaguzi, kuanzia kuandikisha wapiga kura, kutunza vitambulisho vya kupiga kura, kufanya kampeni, na mwisho kwenda kwa wingi vituoni.
..Kwenye kila uchaguzi, wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wamewekewa malengo maalumu ya idadi ya wanachama ambao wanapaswa kuhakikisha wamekwenda kupiga kura.
..Wapinzani wanatakiwa nao kuwa na mpango kazi mzuri zaidi ya ule wa CCM kwa hatua zote za kuelekea ktk uchaguzi mkuu.
cc Bulldog, Alinda, Nguruvi3, Mag3
Mkuu@Mag3 katoa hojainayohitaji fikra. Kasema Watanzania ni watu wa ajabu, wameweka matumaini kwa viongozi wa siasa na si wao kuwa viongozi wa mageuzi. Maana yake nikuwa shinikizo unalosema lilipaswa kutoka kwaWananchi.Mkuu JokaKuu ahsante kwa mhango wako.
Hivi unajua huku "field " kwa sasa wananchi wameshindwa kutofautisha kati ya wapinzani na CCM.
Huku "field" mtu akipata nafasi serikalini alafu asiibe wananchi "tu/wa namwona " ni mjinga....Huchelewi kusikia kauli za "jamaa ----- kweli" kashindwa kupiga?
Mkuu..Unajua hawa wapinzani walikua na muda wa kutosha sana kuweka presha ya Tume huru,aU TUSEME mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi..Lakini kwa nini hawakufanya hivyo?
Hivi leo ukimuuliza Freeman,Lipumba au James....Wanatarajia kushinda kwa juhudi zipi walizofanya? atakujibu lipi la maana?
Nakubaliana na wewe kwamba Wapinzani hawajajipanga ipasavyo.
Tusigemee matokeo tofauti oktoba
JokaKuu, pamoja na yote ukweli usiopingika ni kwamba Upinzani hapa nchini unafanya kazi katika hali ngumu sana na kuwa mpinzani Tanzania kunataka moyo. Kuwa mpinzani ni sawa kutangaza vita dhidi ya utawala ulioko madarakani na hivyo kuwa tayari kuyaonja machungu mikononi mwa vyombo vya dola. Hebu shuhudia visa hivi viwili;
JokaKuu, katika mazingira kama haya, Upinzani wanatakiwa wafanye nini? Wapambane na vyombo vya dola? Huko Iringa mwandishi moja wa habari aliyethubutu kumhoji Kamanda wa Polisi wa Mkoa hivi sasa ni marehemu. Haya yote yanapotokea, sisi wananchi kwa kunyamaza ni kama tunawapa baraka hawa mafashisti wazidi kutunyanyasa. Kwa kweli nashindwa kuwaelewa Watanzania!
Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwashukuru wapenzi na wanachama wa CCM Wilayani Nzega kwa kumpokea vyema na kumtakia heri katika safari yake ya kukijenga na kukiimarisha chama nchini. Kinana alikuwa akiwahutubia wananchi hao saa nne usiku.
Mkuu@Mag3 katoa hojainayohitaji fikra. Kasema Watanzania ni watu wa ajabu, wameweka matumaini kwa viongozi wa siasa na si wao kuwa viongozi wa mageuzi. Maana yake nikuwa shinikizo unalosema lilipaswa kutoka kwaWananchi.
Nasi tukasema Watanzania ni mazezeta au ubinadamu umewazidi.
Unaona baada ya kushindwa kuleta mabadiliko kama ya tume ya uchaguzi,bado wanafurika kupokea wezi waliowaibia
Hoja hapa ni kuwa mabadiliko hayana mtu yana watu, watu nisisi, yule, wale na wao.
Siyosualala Mbowe, Lipumba n.k.
Kuhusu ufisadi, wananchi wanachukia sana. Kinachowakatisha tamaa ni namna unavyoshughulikiwa.
Kuna sababu gani za wao kupinga ufisadiikiwa serikali yao inalinda mafisadi tena kwa kutumia njia za sheria hata kama kuna uharamu?
Hawa wa sh 100 si tatizo ni njaa, tatizo nigenge linalohangaisha umma wa watu milioni45.
Sina uhakika unaongeleaeneo lipi, bribery, corruptions au grand corruptions and sabotage
Hii nchi kwakweli inasikitisha
Mkuu hapa kuna hoja,tutete kidogoAlinda,
..wapinzani wasitegemee hata siku moja kwamba CCM na serikali yake wataleta tume huru ya uchaguzi.
..kitu cha msingi ni kuilazimisha tume hii hii ambayo siyo huru kutangaza matokeo halali ambayo yanaiondoa CCM madarakani.
..Now, u may ask me how do u do that?? Jibu ni kwamba, lazima wapinzani wahakikishe kwamba wanapata ushindi wa kishindo. Yaani ushindi wao uwe ni mkubwa kiasi kwamba haina maana tena kwa tume au CCM kuchezea matokeo.
..Je, inawezekana? Jibu ni kwamba, inawezekana ikiwa wapinzani watawaelimisha vya kutosha wananchi. Kuna majimbo hapa Tz ambayo ktk uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa wananchi wamechagua wapinzani kwa zaidi ya asilimia 80.
..Nigeria wananchi walimpigia kura mgombea wa upinzani kiasi kwamba ikashindikana kuiba zile kura. Yaani ilifika mahali viongozi wa chama tawala wakawa wanalalamika, lakini tume ilishindwa "kufanya-fanya" ikabidi wamtangaze mshindi halali.