Ndio maana tunasema, trusingependa waorodheshe matatizo. Tunataka waweke platform zao nje ya ile ya chama kwanza ili tuwajue wanasimama katika nini. Kusubiri ilani ya chama ni kutafuta namna ya kujificha, utaratibu uliozoelekaAlinda;12895286]Kama hawa watu wangekuwa wanasukumwa na matatizo ya mtanzania basi kwa nafasi zao walizonazo huko serikalini,wangekuwa wanatuorodheshea mafanikio yao, na wapi wanataka kutupeleka lakini matokeo yake kila anayetangaza nia anataka tuanze upya as if hajawahi kufanya kazi katika serikali hiyo hiyo ambayo inatakiwa ifanye anayoyasema.
Atueleze, nini alichoshindwa kufanya miaka 30 ambacho sasa anataka kukikamilishaMathalani
MH: Wassira anasema yeye ataendeleza sekta ya kilimo.. Huyu Wassira ni waziri wa Kilimo sasa ukijiuliza ni nini kilichomfanya hasiendeleze sekta ya kilimo akiwa waziri wa kilimo hila ataweza tu pale hatakapo kuwa rais hupati jibu.
Huyu Mh. hana cha kujivunia katika hiyo wizara maana kama angekuwa nacho angetwambia ni yapi mafanikio yake na anataka kutupeleka wapi na vipi tutafika huko.. Huyu mtu kafanya kazi serikalini zaidi ya miaka 30 leo hii ndo anaona makosa aliyoyafanya/waliyoyafanya na kutaka kufanya kitu kipya.. Hivi kweli hizi ni akili?
Ndio maana tumehoji tatizo ni mikopo au upatikanaji wa fedha. Nchemba amefanya nini kuhusu misamaha ya kodi? Amefanya nini kuhusu wakwepa kodi kama ile kampuni ya Shiiv iliyokwapua vocha za uani kukwepa kodi?Ukija kwa Mwigulu Nchemba naye story ni zile zile. Ukosefu wa ajira, umaskini, mikopo ya wanafunzi anavielewa sana kama anavyojinadi, lakini ana miaka 5 Bungeni, hawezi kusimama na kutwambia katika miaka 5 hiyo amefanya nini katika jimbo lake ili kuondokana na tatizo la ajira au amefanya nini katika katika swala zima la wananchi wa jimbo hilo kuondokana na umasikini, au kama Naibu wa fedha kwa kipindi kifupi alichokaa katika hiyo wizara amewasaidije hawa wanafuzi katika swala zima la mikopo.
Tunasikia vijana wa NCCR wanalalamika. Hatujawasikia wakihamasisha uandikishaji au mabadiliko.Tukirudi kwa Ukawa/wapinzani tunakumbana na tatizo ile ile ya kupenda madaraka bila kuwekeza.. Wakati baadhi ya vyama vikiwa katika mikoa mbali mbali kuhamasisha uandikishwaji katika daftari la wapiga kura, kuna baadhi ya wanasiasa wako busy na kutangaza nia. Hivi unapokaa studio kwenye viyoyozi na kutangaza nia na ukitoka hapo unakwenda nyumbani kwako kulala unafikiri ni nani atakuchangua kama husipokwenda kuhamasisha wananchi kujiandikisha?
Nilitegemea kuona vyama vyote vinne wakiwa kazini wakihamasisha watu kujiandikisha katika daftari ya wapiga kura na katika mikoa mbali mbali lakini tunachokiona ni Cuf na Chadema ndo wako kazini hali NCCR na NLD (tena bora NLD tunaweza kusema hawana fedha) wako busy na kuwapangia wanaukawa nani awe rais na kwanini awe rais (rejea thread ya Mweyekiti wa Vijana NCCR).. Hii ni aibu, huu ni jinga, na huu ndo ule usaka tonge alosema Zitto.
Hivi chama cha NCCR kinashindwa kufanya mkutano walua kwa mwezi mara moja? NCCR kina ruzuku kina wabunge wanne hivi hawa wabunge wameshindwa kubuni mkakati wa kutangaza hiki chama? Leo hii ukiniuliza ni nina Katibu mkuu wa NCCR au mweka hazina au Mweyekiti wa baraza la wanawake au Katibu wa baraza la vijana (kama yapo) hawafahamiki zaidi ya Mbatia na wabunge wake 3. Hii ni aibu kwa hawa wabunge wanatakiwa kujenga chama chao nchi nzima Si Kigoma na Vunjo tu
Bulldog kuna tatizo katika kambi ya upinzani hasa katika maono na mikakati
Adharusi ukilinganisha wapinzani na wale wa tawala kwa vigezo unavyosema upo sahihi.
Hata hivyo, huyu aliyesema anachukizwa na akatamka ni bora kuliko yule aliyejificha nyuma ya chama.
Hawa akina Wasira si ndio walikataa Escow zisichunguzwe, hivi tunaweza kuwalinganisha na Kafulila katika uchungu?
Alinda kuna mengi umeongea, nitarejea. Kwa uchache, hivi Sumaye aliyekuwa waziri mkuu miaka 10 ana kipi kipya anachotaka kufanya zaidi ya majibu aliyotoa kama tulivyoonyesha akaongezea Ritz , kwamba PM hajui BoT inafanyaje kazi!
Hajui uhusiano wa waziri mkuu na BoT. Huyu alikuwa waziri mkuu wetu!
Kitu kimoja nilichokiona kwa Watangaza nia, wote wanasema kuna tatizo la RUSHWA na UMASIKINI.
Kwa maneno mengine wanatueleza kuwa mfumo wa JK ni wa rushwa na umasikini umeongezeka.
Kumbuka hawa wapo ndani ya sytem na sasa wanatoka kutueleza wazi.
Wanajua rushwa kwa ukamilifu na jinsi serikali inavyosiamamia kushamiri kwa rushwa
Wote wametaja Rushwa.
Kwanza shukrani kwa uzi huu, ambao nafikiri unalenga kuwapa watanzania kujua uhalisia wa watanzania wenzao wanaotaka (sina hakika kama ni kwa hiari yao) kuwa wawakilishi wao katika nafasi mbalimbali za uongozi wa taifa hili. Wakisha kujua uhalisia wa watanzania wenzao hawa juu ya uhalisia wao (kiuwezo na kidhamira kwa uchache) wa kuwasaidia kupambana na kuzishida changamoto sugu (maradhi, umaskini, ujinga na sasa RUSHWA), watakuwa na nafasi ya kufanya maamuzi sahihi.Tunajiuliza, lini hawa watangaza nia wamesimama na kuhesabiwa wakikemea rushwa? Leo wanaposema rushwa ni tatizo, wapi wanapata ushujaa huo?
....
Nadhani wananchi bado hawana imani na wapinzani, bado wana imani na CCM ingawa ina mapungufu mengi na imeshindwa kuleta mabadiliko ndani ya miaka 50 kama alivyofafanua Nguruvi3 hapo juu. Ni wajibu wa vyama vya upinzani kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mabadiliko hasa katika kipindi hiki. Wengi wana hofu wakiangalia candidates wa urais katika upinzani wakilinganisha na watangaza nia wa CCM wanaona kama vile upinzani hawana watu wenye uwezo.Tanzania hatuna upinzani wa kuweza kuwasaidia watanzania kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine. Wapinzani wangekuwa na nia ya dhati wangejiunga na umoja wao kama vyama vilivyounda UKAWA na kuhakikisha wanaisimamia serikali kuandikisha watu wote wenye vigezo vya kupiga kura. Hii ingewasaidia sana kuitoa CCM madarakani. Wasimamie zoezi zima la kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo.
Nguvu ya umma.
Watanzania ni waoga na wasahaulifu sana. Ukiangalia toka JKikwete aingie madarakani hadi leo madudu mengi yamefanyika, kuna ufisadi wa wazi sana na hadi waziri mkuu kujiuzulu. Lakini sisi tumesahau kiasi kwamba huyo waziri mkuu tunamuona amegeuka lulu.
Maswala nyeti yanayohusu maslahi ya taifa tunayasahau sana. Watu wanaendelea na shughuli zao kana kwamba hayawahusu kumbe wao ndo wahanga wakuu wakubwa.
Binafsi naona dhahiri kuwa ukombozi tunaoudhania utatokea 2015 hautatokea kwasababu wananchi hatujatambua nguvu tulionayo.
Katavi, kuna hilo tatizo ulilosema. Ukisoma mabandiko tumewaeleza wazi, ni lazima wawe viongozi wa maono na kutenda na si kusubiri kuongozwaNadhani wananchi bado hawana imani na wapinzani, bado wana imani na CCM ingawa ina mapungufu mengi na imeshindwa kuleta mabadiliko ndani ya miaka 50 kama alivyofafanua Nguruvi3 hapo juu. Ni wajibu wa vyama vya upinzani kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mabadiliko hasa katika kipindi hiki. Wengi wana hofu wakiangalia candidates wa urais katika upinzani wakilinganisha na watangaza nia wa CCM wanaona kama vile upinzani hawana watu wenye uwezo.
Hapa naona unawasurubu mpaka Tundu Lissu,Lema wabunge wote kwa ujumla,kwa ufupi hawastahili kurudi mjengoni tenaHuko Majimboni, waulizeni, lini walikuja kutaka maoni yenu kabla ya kwenda bungeni?
Zile fedha za mfuko wa jimbo zinafanyiwa ukaguzi na nani?
Katavi, kuna hilo tatizo ulilosema. Ukisoma mabandiko tumewaeleza wazi, ni lazima wawe viongozi wa maono na kutenda na si kusubiri kuongozwa
Hili nitalichangia pamoja na hoja ya Bulldog kuhusu ni kifanyike, ingawa sikumwelewa ilikuwa kwa upande gani
Nitaongelea wapinzani
1. Wana bahati, agenda zimeshatangulia kwa wananchi.
Umasikini, hali ngumu ya miasha
kuzorota kwa huduma za jamii kama afya na elimu
Rushwa iliyojengewa mfumo katika nchi na wizi unaoligharimu taifa
Wananchi wanayajua hayo
2. Kuhsindwa kwa CCM, kwamba miaka 50 tupo hapa tulipo. Wananchi wanalijua hilo
3. Nchi kupoteza ushawishi katika jumuiya ya kimataifa, wanalijua hilo
4 Matatizo yasiyo na majibu kila siku, wananchi wanayajua
Orodha ni ndefu sana, ninachosisitiza ni kuwa agenda zimeshatangulia
2. Wapinzani wanapokelewa na wananchi kila wanapokwenda.
Si kuwa wananchi wanataka kuwaona, bali wana kiu ya kusikia kile wasichokipata kwa muda mrefu. Wana kiu ya mabadiliko
3. Tayari wana mfano.
Wananchi wanaona kazi inayofanywa na wabunge-upinzani. Pamoja na uchache wao lakini wanaweza kutetea hoja zao kwa mantiki
Hivyo, kazi ya Wapinzani si kuweka mezani agenda.
Tayari wananchi wana agenda. Wapinzani wanatakiwa kutumia agenda hizo kuwaondoa wananchi hofu kuhusu ukweli.
Kuwaondoa hofu kuhusu hujuma, udhaifu na uhalifu uliopo
Wapinzani watumie mifano halisi kuonyesha jinsi wanavyoumizwa kwa uzembe wa kundi dogo.
Jinsi wanavyolipa gharama kubwa za maisha yao kwasababu ya kulinda watu wachache.
Kwa mfano, ile kampuni iliyokwepa kodi za Bilioni 300 ni ya watu wachache.
Wakati serikali ikiacha watu hao waendelee kutamba, wagonjwa anakufa muhimbili kwa hosipitali kukosa Bilioni 10.
Kwamba kodi iliyokwepa ni kubwa kuliko bajeti ya Muhimbili. Waonyesheni kwa namba
Waambieni madarasa na maabara za shule wanazochangia si haki yao. Ni haki yao kuwa nazo, si haki kuchangia
Wekeni namba za CGA, kupotea kwa mabilioni ambayo yangeweza kumaliza mradi wa maabara bila mwanacnhi kutoa senti tano
Waelezani wanachi takwimu za uchumi, matatizo yanayowakabili walipo na mnaahidi nini na kwa njia zipi kwa kutumia rasilimali gani kuayamaliza.
Hoja hapa ni kuwa ipo fursa iliyotengenezwa na CCM, wapinzani wanatakiwa kuweka mbolea tu. Hoja tayari zipo
Wapinzani wasambae nchi nzima. Si lazima wote wakae vikao vya kugawana majimbo.
Kuna tech committee za kufanya kazi. Wapinzani waonyeshe UKAWA ipo kote si kwa viongozi tu
Wapinzani wafike maeneo magumu. Hivi kwanini waamini hawawezi kupata kiti mkoa wa Tanga!
Mbona waliweza kupata Mbeya, Shinyanga na kwingineko.
Ni lazima wawafikie wananchi wakiwa na ujumbe wa kuamsha matumaini, kuonyesha njia na kueleza namna gani wananchi watafika huko
Adharusi, soma kwa uyakinifu usiwe na prejudice. Nimeeleza hapo juu, waende kueleza wananchi kwanini tupo hapa, wanafikiria nini kutuondoa hapa, kwa njia gani na rasilimali ganiKwahiyo unataka na upinzani waendelee kurodhesha matatizo duu,wakati umeshasema wananchi hawataki orodha ya matatizo,naomba Nguruvi3 Sababu unakiu ya mabadiriko ungewaambia upinzani wanatakiwa kufanya nini,ili kuondoa kwwenda kuorodhesha matukio,vinginevyo icho unachofikilia wapinzani hawataweza kufanya maana wenyewe ni sehemu ya wabunge,wamekua wakiungana na CCM katika kufaidi keki ya Taifa,wanajiongezea tu mafao
Wapinzani wetu ni wasanii tu,mfano Dr Slaa wakati aliwahaidi watanzania kua akienda ikulu yupo tayali kula mihogo,wakati ndani ya CHAMA chake kawawekea masharti,uchaguzi ukiisha,sababu yeye atokua mbunge basi alipwe kama mbunge, hivi na yeye atapokea kiinua mgongo chake mwezi 7
Nguruvi :
Waelezani wananchi takwimu za uchumi, matatizo yanayowakabili, walipo na mnadhidi nini na kwa njia zipi kwa kutumia rasilimali gani kuayamaliza.
Nadhani unapaswa kuchangia hoja, unachokifanya ni vioja. Je umesoma mabandiko yote ? umeelewa?Hapa naona unawasurubu mpaka Tundu Lissu,Lema wabunge wote kwa ujumla,kwa ufupi hawastahili kurudi mjengoni tena