2015 sio mbali wenzako wameanza leo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015 sio mbali wenzako wameanza leo.

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Nduka, Feb 9, 2011.

 1. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Unataka kushinda kura za maoni na kuteuliwa na chama chako kugombea ubunge au nafasi yeyote ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015? Unataka kugombea ubunge kama mgombea binafsi na kushinda uchaguzi mkuu? Basi soma hapa.
  Tunatambua idadi kubwa ya watanzania wanaoishi nje ya nchi wana nia, uwezo na sifa za kushika nafasi za uongozi zinazotokana kupigiwa kura na nia zao huzingwa na kutofahamika kwao kwa wapiga kura na jitihada zao kuzingirwa na umaarufu wa wagombea wengine.
  Tunatambua idadi kubwa ya wafanyakazi katika sekta binafsi na sekta ya umma wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wanakwamishwa na sheria au majukumu yao katika taasisi hizo.
  Katika juhudi za kutimiza ndoto za watanzania wenzetu wanaobanwa kwa namna moja au nyingine kushiriki katika uongozi wa nchi yao kwa kushindwa kupata fursa ya kushiriki na kushindana katika chaguzi kutokana kukosa umaarufu kwa wapiga kura kampuni yetu inakusudia kukufanyia wewe yafuatayo:
  · Kufanya utafiti wa aina ya wapiga kura na mahitaji yao
  · Kujenga ushirikiano na wadau muhimu katika jimbo au eneo la uchaguzi
  · Kutafuta mianya ya uchangiaji na kuifahamisha jamii vipawa vyako na kujenga matarajio.
  · Kuanzisha, kuimarisha, na kudumisha uhusiano wa kijamii baina yako, vyombo vya taarifa na wadau wajenzi wa maoni katika jimbo au eneo.
  · Kujenga umaarufu wako binafsi na kuhuisha michango yako kijamii.
  · Kusimamia ajenda yako ya uchaguzi na kuinogesha na mahitaji/matarajio ya wapiga kura
  · Kusimamia shughuli zako za kutangaza nia,kukampeni na kusherekea ushindi.

  SISI NANI?
  Kampuni yetu imesajiliwa kama kampuni ya ushauri na uchunguzi tangu mwaka 1997, tuna uzoefu wa kusimamia kampeni mbalimbali zilizofanikiwa. Tunafanya kazi kwa usiri mkubwa na wateja wetu hubakia siri. Tuna rekodi nzuri ya kushinda kwenye kila kazi tuliyoifanya bila kuathiri sheria na maadili ya nchi. Wataalam wetu ni weledi na wana uzoefu wa chaguzi kutoka nchi mbalimbali Afrika,Ulaya na Marekani.
  Kumbuka..
  Alipoinunua club ya Rangers 1989 G.W Bush hakuna aliyedhani kuwa alikuwa ananunua tiketi yake ya white house na kilichofuata ni historia
  Najua kuna wenzetu wanauwezo na wangehitaji kuzungumza na sisi tafadhari ni PM nitakupa mawasiliano..
   
 2. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Upo JUU

  Vp una contact za Waganga ? kna watu hawaamini hizo isho bila kupiga ramli kidogo
   
 3. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mi signature yako tu ndo nimeiona.
   
 4. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Ngoja kidogo.......Una agenda.........Siyo mpya...........!!!!!Angalia utashi wa wateja wako kwanza wana hali gani?
  Kazi ni kupigiwa kura tuu na kuchaguliwa au ni kula baada na kabla ya kura??:clap2:
   
 5. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Swali:

  Katika mbinu mnazotumia kuhakikisha mteja anashinda, je huwa mnatumia "Character Assassination" kwa rivals wa candidate wenu?
  Kwa Tanzania mbinu hii huwa very effective...
   
 6. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mmmmh sidhani kama mmeteka soko la bongo bila kuathiri sheria za nchi pamoja na maadili, hasa ukizingatia kinachijiri nyakati za uchaguzi uzushi mwingi, ghilba, chuki za waziwazi, SMS za kuchafuana, mbinu chafu ( hasa chama tawala), hongo kwa wapiga kura, wizi wa vitambulisho vya wapiga kura ili mradi wasitokee siku ya kupiga kura. Chaguzi za Tanzania ni very unique ndugu, hakuna kampuni inayoweza kutumia professionalism kufanikisha hayo uliyoyasema. Lakini utawavuna watu ambao ni short sighted persons!!!
   
Loading...